Mifuko ya Hifadhi iwe hiari na sio lazima

Mifuko ya Hifadhi iwe hiari na sio lazima

Ricky Blair

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
463
Reaction score
1,009
Hii mifuko yote iwe ya hiari tu na sio lazima sababu wote ni wezi; kujiunga ni rahisi lakini kutaka pesa zako ni mlolongo mrefu kama nini!

Mimi nilikuwa PSPF kabla haijajiita PSSSF, tukaambiwa sisi private twende NSSF, sasa nikasema hela yangu vipi inaenda kule au mnanipa? Hawataki eti mpaka uzeeke au sijui NSSF wenyewe ndio wanajua when.

Sasa mifuko ni tofauti na hata ukideclare unemployment 33% na mpaka hiyo 33% uipate utajuta. Jamani hebu imagine; uweke mil. 1 CRDB uende kuitoa upeleke NMB au utumie ukataliwe, huu ni utumwa.

Sisi Bongo tumezubaa sana, hebu ona huko Ufaransa wazee wameliwasha, Macron anavyojiroga aongeze miaka ya ustaafu kutoka 62 to 64 sisi hata wakisema 100 tutabaki tu hivi hivi kama konokono, ushoga tu ndio tuna hasira nao.

Hii mifuko ifutwe kabisa kila mtu ale lake. Hakuna cha SDL, cjui worker compensation, nothing, ibaki PAYE tu basi. Hawafai sana hawa, yaani siku tetemeko la ardhi likija lianze na majengo yote ya NSSF au PSSSF na majengo yao mengine wanaojenga na kupangisha au kuuza kwa bei ya kitajiri wakati hela wanatuibia sisi.

Yaani mpaka mzee anakufa hapati haki yake upuuzi wa wapi huu? Na hizo procedures uwiii, natamani nijilipue kabisa.
 
Wasioajiriwa ambao ni wengi sana kuliko waajiriwa ni nani anawawekea mafao yao ya uzeeni, tuanzie hapo kwanza.

Hii ni janja janja ya serikali kuendelea kuwanyonya wafanyakazi. Kwanza mishahara wanayowalipa ni kiduchu, hapohapo wanaendelea kuwanyonya damu kwa ulaghai wa kuwasaidia uzeeni.​
 
Back
Top Bottom