Mifuko Ya Jamii

lnspector CP

Member
Joined
Apr 28, 2016
Posts
76
Reaction score
30
Habari,
Ndugu wanajukwaa, nategemea wengi wetu tunaifahamu hii mifuko hasa tuliopo kwenye soko la ajira, watu wengi hasa tulio kwenye kampuni binafsi huwa tunapigia mahesabu michango unayoweka kwenye PPF ama NSSF kwa ajili ya kufanyia biashara au kwa mambo mengine ya kiuchumi mara tu utapoacha au kuachishwa kazi.

Lakini kwa tetesi zilizopo ni kwamba mwachama hutochukua michango yako hadi ufikapo miaka 55.

Je hili lina ukweli wowote maana nimeangalia magazeti na kusikiliza habar hii taarifa haipo,kwa anaefaham naomba anipe ukweli
 
Kuna mifuko unapewa hela yako muda wowote kuna mingine ni longo longo mwanzo mwisho usijaribu hata kuikaribia.....
Wanasema wana mikopo ya shule, mafao ya uzazi n.k hawana lolote uongo mtupu inaonekana hataki hiyo miaka 60 tukijaaliwa inakua ni dana dana tu
 
PPF unachukua ndan ya mwez 1 sema hiz tetes za mpaka miaka 55 ndo znanitia kizunguzungu
 
PPF unachukua ndan ya mwez 1 sema hiz tetes za mpaka miaka 55 ndo znanitia kizunguzungu
Hizo sheria zipo lakini ukiwa na sababu ya kuhitaji pesa yako kama vile umeacha kazi sahivi, unapewa tu ila ni kwa mifuko isiyo na longo longo
 
Hiyo tetesi kakwambia nani? Hakuna kitu kama hicho wewe nenda kachukue, lini wadau walishirikishwa? lini ilisomwa bungeni huo muswada? lini magufuli alisaini huo mswada?
 
Hizo tetesi huenda ni za kweli.
Angalia website ya PPF wameshaondoa fao la kujitoa.
 
Hizo sheria zipo lakini ukiwa na sababu ya kuhitaji pesa yako kama vile umeacha kazi sahivi, unapewa tu ila ni kwa mifuko isiyo na longo longo

Labda sio PPF....
Wameondoa fao la kujitoa kwenye website yao.....

 
Hiyo tetesi kakwambia nani? Hakuna kitu kama hicho wewe nenda kachukue, lini wadau walishirikishwa? lini ilisomwa bungeni huo muswada? lini magufuli alisaini huo mswada?
Mambo yalibadirishwa wakati wa JK.
 
it is true, effective from this week, nilimsikia mhusika wa PPF jana kwenye Clouds akisema kuwa kifungu walichokuwa wakitolea mafao kimefanyiwa marekebisho tangu tarehe 12/May/2016. Hivyo hatutaweza tena kuchukua hela yetu. Kuna watu walikuwa wanalamika ikabidi clouds wamhoji mhusika. MM pia ni muathirika (labda) nilipeleka fom yangu tar 15/May ikapokelewa ila kifungu kilikuwa tayari kimeshafanyiwa marekebisho.

Marekebisho ya kifungu hicho yanakinzana na sheria mama ya hifadhi za jamii kwani mswada mpaka upite bungeni. hivo nafikiria kama wataniandikia barua rasmi kunijibu basi nitachukua hatua za kisheria kuomba tafsiri ya sheria hii iliyofanyiwa marekebisho na sheria za nchi. May be sometimes later we can team up and see what comes in!
 
Safi mkuu kwa initiatives ila SSRA na Joni wamefanya uhuni hapa sikumbuki lini wamefanya marekebisho baada ya hoja binafsi ya jafo 2012?
 
Kama watazuia hyo pesa watatuumiza vijana hasa walio kwenye sector binafsi......mikataba yenyewe ni ya muda mfupi na kuachishwa kaz ni nje nje na hii mifuko ndo kimbilio lao kwa kuanzishia biashara na mambo mengine.Mm mwenyewe ni muhanga na nahic kama pesa yangu imetaifishwa kwasab kufika hyo 55years .....ni shidaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…