Mifumo mibovu ya Kodi ndio inafanya Serikali kukosa mapato na watu kukwepa Kodi

Mifumo mibovu ya Kodi ndio inafanya Serikali kukosa mapato na watu kukwepa Kodi

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
Siku zote serikali inabidi kukaa na wananchi wake kupata mawazo mazuri ambayo kila mtu yata mgusa.

Mifumo ya kodi kwa nchi yetu ni mingi na ina msululu usio kuwa na sababu ukimuumiza mtu wa mwisho.

Huu ni moja wa mfano tosha:

- Unapopanga fremu ya kufanya biashara TRA wanataka kujua mkataba uliopangisha kiasi gani wakate kodi yao, bado biashara yako, bado tozo ya umeme, bado tozo za manispaa, bado tozo za mabango na n.k

- Unapoagiza gari au kitu chochote meli au ndege iliyoleta italipa kodi, mzigo wako utalipa na n.k

- Unasafirisha mazao hapa ndo usiseme yani mpaka mzigo unafika ukijumlisha na faini za trafiki ni kama unasukuma maisha tu.

Tuje kwenye mada.

Mifumo hii inasababisha hata kupotea kwa mapato ndani na nje kutokana na kuwa na mtiririko lukuki wa kodi ambazo hata leo ukimuuliza TRA naye anaweza kushangaa mpaka CAG aje kujua pesa zilipotea wapi.

Kwanini kodi zimekuwa utitiri na zote zina kwenda sehemu mmoja.

Wajuzi!
 
Kodi ni uhuni mzee, ukijifanya wewe ndo unajua kulipa itakula kwako fanya biashara kwa akili mzeee otherwise utakuwa unafanyia serikali kazi.

Mimi nalipa makadirio provision, nalipa Withholding, nalipa manispaa, bado taka, bado fire asee mtatuaaa ndomana sitoi risiti aseee [emoji28].

Kwanza watanzania raha sana unamwambia hiyo bidhaa na vat 600,000 bila vata 550,000 uyo anakwambia sitaki risiti[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wanajua ila "wameacha ikae hivyo"
 
Hayo mambo yanahitaji akili na sisi hatuna akili.
 
Ukianzisha biashara yako kihalali ukafuata taratibu zote za kisheria za kulipa kila kodi kila tozo ya serikali utafikisika kabla hujakata mwaka. Kodi za Serikali sio rafiki kbs kwa wafanya biashara. Utitiri wa kodi.
-kodi ya mkataba wa upangishwaji
-mapato, wanachukua hujafanya biashara wao washabeba.
-service levy
-wapo kwenye taka
-wapo kwenye umeme
-leseni ya biashara nk
HUCHOMOKI
 
Ninadiriki kusema kodi wanalipa wafanyakazi tu! Mifumo yetu ya kukusanya kodi kutoka katika sekta zisizo rasmi ni mbovu sana ambapo ni wachache sana wanalipa.

Hata EDF machines ni kama serikali ilitaka tu kuuza mashine na karatasi ya kuchapishia. Au kuunganishwa kwa intanet.

Bado kuna VAT 0% katika risiti nyingi!
 
Back
Top Bottom