Mavipunda
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 7,072
- 7,891
Kuna jamaa yangu tokea majuzi alikuwa akishinda Makao Makuu ya Uhamiaji pale Kurasini kufuatilia passport ya mwanawe anayetakiwa kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya masomo ila leo aliwasikia baadhi watumishi pale wakinong'onezana kwamba mitambo hiyo leo tokea asbh imegoma kufanya kazi.
Ikumbukwe wadau wengi waliwahi kuunyooshea kidole mradi huu ambao kimsingi ulisimamiwa kwa kila kitu na Ofisi ya Rais Ikulu(TISS) sasa hata mwezi bado tokea uzinduliwe kwa mbwembwe tayari umeanza kuonyesha matokeo hasi. Niliwahi kumsikia jamaa yangu mmoja kule Zanzibar nae aliwahi kuniambia kwamba hata kule nako hio mifumo imekuwa ikisumbua.
Nahisi kukosekana ushindani katika kutafuta mzabuni ndio kumefanya Mzee kuingizwa chaka.
Ngoja tuone wahusika wakikanusha au kutupa maelezo ya kiufundi