SoC02 Mifumo ya Elimu ndiyo kikwazo vijana kushindwa kujiajiri

SoC02 Mifumo ya Elimu ndiyo kikwazo vijana kushindwa kujiajiri

Stories of Change - 2022 Competition

Albashiri

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
2
Reaction score
1
MIFUMO YA ELIMU YETU TANZANIA HAITUANDAI KUJIAJIRI
Elimu yetu ya Tanzania hasa ya darasani iliyo rasmi haijawa katika kuwaandaa vijana kujitegemea baada ya kumaliza elimu ,nitazungumza maeneo ya hiyo mifumo ya kielimu.

1)MITAALA ,mitaala ya kuendeshea elimu haipo kwa ajili ya kuandaa mhitimu ambaye atakuwa na uwezo wa kujitegemea mana elimu inaendeshwa kwa mfumo wa nadharia kuzidi vitendo ,vinafundishwa vitu vya kufikirika tu ambavyo kiuhalisia havipo ,wakati mwingine havina uhalisia katika mazingira yetu ,mfano unapomfundisha mtu kuwa binadamu alikuwa nyani usipomuajiri unahisi hayo maarifa atayatumia wapi ?kwa nini usimuelezee hata historia ya nchi yake ilikotoka na inakoelekea angalau hata ajue kinachoendelea mtaani?

Kinachofundishwa shuleni na vyuoni asilimia kubwa hakipo katika uhalisia ,unafundishwa juu ya changamoto zinazokabili kiwanda cha kutengeneza magari japani ,mwishowe huyu mhitimu wa maarifa haya ataenda wap asipoajiriwa? Kwa nini tusijifunze hata changamoto zinazokabili kilimo cha Mchele au mahindi au hata alizeti ?

Ili huyu mtu anapomaliza usipomuajiri sio mgeni na jamii yake, na hii itamrahishia kuielewa jamii haraka na hata kutowaza serikali imuajiri, mifumo yetu ya elimu iko nadharia na vitu vinavyofundishwa kwa vitendo ni ili ufaidike navyo lazima uwe muajiriwa ,na elimu yetu inachukua muda mrefu sana kijana anamaliza umri wa kuingia katika familia na haelewi afanye nini mana amesoma kitu ambacho kiuhalisia anapomaliza asipoajiriwa anakuwa mgeni wa mtaani na huku mtaani anaanza upya ,ifike wakati elimu yetu izungumze hata vitu vya kawaida tu kama kilimo ,siasa ,michezo na TEHAMA , tuzungumze vitu vilivyo kwenye jamii yetu na ambavyo dunia ipo kama TEHAMA.

2)WASIMAMIZI ELIMU SIO WATU WA ELIMU ,unakuta waziri wa elimu na wizara ndo wanafanya maamuzi juu ya elimu yetu ilihali wenyewe hawajawahii kuwa walimu na wala hawajui chochote kuhusu elimu, wanafuata ushauri wa watu wachache walio na vyeo ambao wengi sio wataalamu wa elimu, tunahitaji elimu iendeshwe na walimu wenyewe na wanaosimamia wizara ya elimu wawe wamesomea elimu na sio taaluma nyingine kusimamia na kufanya maamuzi katika elimu, hapo nimezungumza ngazi ya juu ya usimamizi.

Kwa ngazi ya shule na vyuoni, mazigira ya elimu kama madarasa ,vitabu ,walimu hawatoshi na kama wapo mazingira, maslahi na makazi yao yamepuuzwa na ndo mana wanatumia muda mwingi kuwaza maisha yao kuliko kuandaa vijana wetu kwa ajili ya kesho ,kwa kifupi usimamizi wa elimu kwa ngazi ya chini walimu bado hawajafanya kazi ipasavyo ni kwa sababu hawatoshi na mazigira ya kazi hayawaruhusu kufanya kazi zao ipasavyo ,wamesahaulika kila jambo yani kila kitu wanaletewa na kuambiwa watekeleze na wala hawasikilizwi.

Tufanye nini katika hili ? Hebu wizara ya elimu isimamiwe na wenye taaluma ,waziri hata kama hana taaluma lakini yeye asiwe mtu wa kufanya maamuzi awaachie wakuu vya vyuo vya elimu ,wakuu wa shule maafisa elimu ndo wapange kila kitu kuhusu elimu ,naamini haya yapo ila kiuhalisia yanayopangwa na wataalamu wa elimu yanaingiliwa na ambao sio wataalamu wa elimu, kwa huku hatuwezi kufika ,wataalamu wa elimu kama maprofesa katika ualimu wanatakiwa kusikilizwa na wafanye tafiti zinazohusu ipi ni elimu sahihi ya kupewa watanzania, sio unapendekeza mtoto asome historia ya binadamu kuwa nyani, baada ya hapo hiyo elimu inamsaidia nini?

Kwa nini hicho kipengele tusiweke hata kuzungumza tu binadamu tumetoka kwa mungu na tunatakiwa kumuogopa mungu na kumtegemea kwa kila kitu angalau hata hii tunaandaa watu wenye hofu na mungu tunawatengeneza vijana kitabia na kupunguza maovu katika jamii inakuwa afadhali kuliko vitu hivo vingine, wataalamu wa elimu vyuoni hizi changamoto ya elimu yetu mnaijua badilisheni mifumo imuandae mtu akimaliza hata usipompa ajira halalamiki mana alichofundishwa kipo katika mazingira ya kawaida ,tuweni na elimu ambayo inamsaidia mtu binafsi ,ni kawaida kumukuta kijana akichosomea hata mazoezi (field ) ya alichokisomea hajui ni wapi ,manake alichokisomea hakioni katika jamii yake kama kipo.

(3)Uwekezaji mdogo katika elimu ,bajeti siamini kama ya kutosha mana vifaa vya shule kila mwaka havitoshi ,wafanyakazi mishara iko chini ,mazigira ya kazi hovyo na tunataka tupate wataalamu wazuri baadae ,kweli tukitaka kuandaa vijana tuandae mazingira yao na wanaowasomesha hapo naamini tutaandaa vijana ambao hata alichokisomea hakipo katika jamii ila anakielewa

NINI KIFANYIKE ILI TUANDAE VIJANA WENYE UWEZO WA KUJIAJIRI
(1) Tubadilishe mifumo ya elimu, wekeni mifumo ya elimu ambayo ipo katika kumuandaa kijana kutumikia jamii alikotoka, tunahitaji kuona jamii inasoma hata ushonaji wa nguo ,kuwepo shule za michezo na Sanaa, tunategemea watu wasomee kilimo sio kilimo tu ,kilimo cha mazao yaliyoko nchini kwake ,haitakuwa jambo la ajabu kuwa na mada ya kilimo cha alizeti singida na changamoto zake na ikibidi atakayetaka kubobea hilo suala aende akasome kwa vitendo singida na kufanya tafiti huko singida ,tufundishwe uvuvi bahari ya hindi, visiwa vya unguja na pemba, ziwa Victoria, tanganyika na nyasa na changamoto zake, kilimo cha mahindi ikiwemo soko lake na changamoto ,wasome mambo ya computer, teknolojia mana huku ndo dunia iliko ,tusimpotezee mtanzania muda anakaa darasani anachosoma kwa jamii yake hakioni kama uvuvi Norway kwake unamsaidia nini, utengenezaji wa magari nchini japani hapa Tanzania unamsaidia nini? Tuje na vitu vyetu sisi bila kusahau sayansi na teknolojia inasemaje mana ndo dunia jumuishi au dunia kijiji tuliyopo sasa.

(2) Elimu isimamiwe na wataalamu wa elimu na sio vinginevyo, tuanze kwa kuboresha utawala wasimamizi na wanaofanya maamuzi wawe ni watekelezaji wenyewe ambao ni maafisa elimu na walimu wenyewe hawa watu ndo wasikilizwe ,boresheni mazingira ya kazi kwa maslahi na madarasa yetu ,vitabu viwepo vya kutosha pia
 
Upvote 2
Back
Top Bottom