SoC04 Mifumo ya kielektroniki iboreshwe ili ifanye kazi kwa ufanisi

SoC04 Mifumo ya kielektroniki iboreshwe ili ifanye kazi kwa ufanisi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Dhengo

New Member
Joined
May 30, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Matumizi ya mifumo ya kielekroniki katika taasisi mbalimbali za serikali yamekua na matokeo mazuri hasa kwa upande wa kupunguza msongamanokupunguza rushwa na hata pia kwenye suala la ukusanyaji wa mapato imerahisisha.

Lakini pamoja na mafanikio hayo mifumo hii ya kielektroniki Kuna muda inashindwa kufanya kazi ipasavyo na hivyo kusababishia usumbufu kwa watumiaji.

Unaweza ukaenda kwenye taasisi ya serikali kupata huduma lakini unafika pale unaambiwa mtandao hamna kwa Sasa Hadi baadae unaporudi baadae pia unaambiwa haujarudi,Sasa kwa Hali kama hiyo mtumiaji au mteja anakua amepoteza muda wake pengine hata pesa za kwenda Kila mara kuuliza kama mtandao umerudi.

Mfano sehemu kama hospitali taratibu zote zinaingizwa kwenye mfumo Hadi unakuja kupata majibu lakini utakuta magonjwa anaumwa Yuko kwenye foleni anazidi kupata maumivu lakini anaambiwa mfumo unashida kwahyo ataendelea kuumia pale Hadi mfumo utakapokaa sawa.

Ni kweli mifumo ya kielektroniki imerahisisha sana huduma kwenye nchi yetu lakini kama tunataka Tanzania yenye maendeleo na iliyo Bora zaidi basi tutumie wataalamu wetu ili kuweza kuona namna ya kuboresha hii mifumo yetu ikafanya kazi kwa ufanisi mkubwa bila kusuasua,hapo tutafika mbali kama taifa kiteknolojia na kimaendeleo pia.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom