KAPUNGU DICKSONI
New Member
- Feb 23, 2024
- 1
- 1
Mifumo ya Kikodi katika Mpaka wa Tunduma ni tatizo, inasababisha foleni kubwa. Kwanini Tanzania haitumii mfumo sawa na Zambia?
Mpaka wa Tunduma ni shida na kero kubwa kwa Wasafiri na Wasafirishaji. Katika eneo hili panatarajiwa kila kitu kifanyike kwa haraka, ili watu waendelee na safari zao, lakini hali ni tofauti, kwani Mifumo ya kikodi ni kikwazo. Mifumo inayotumika Tanzania haisomani na ya Zambia, hivyo huchelewesha uvushaji wa magari na kusababisha foleni kubwa.
Mpaka wa huu ni moja ya mipaka mikubwa Tanzania, Malori 600 hufika kila siku katika mpaka huu yakiwa njiani kuelekea katika nchi za Kusini mwa Afrika. Kukinzana kwa mifumo ya kikodi, kunachangia kwa kiasi kikubwa, kukaa kwa muda mrefu mpakani Tunduma kwa mizigo inayokwenda katika nchi za Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
Mizigo hiyo ni takriban asilimia 70 ya mizigo inayoshuswa katika Bandari ya Dar es Salaam kuelekea nchi hizo za Kusini mwa Afrika
Wakati mwingine Malori haya hujipanga hadi umbali wa Kilomita 5, upande wa Kusini mwa mji ambako ni barabara ya Tunduma-Mbeya na Kilomita 5 Kaskazini Magharibi mwa mji, barabara ya Tunduma-Sumbawanga. Foleni hizo huziba barabara za ndani ya mji na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara.
Shida iko wapo katika mifumo ya Kikodi?
Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatumia mfumo wa TANCIS. Mfumo unaotumiwa na Jumuiya za Afrika Mashariki (EAC), katika uhamishaji wa mizigo kutoka nchi moja kwenda nyingine na kutoza kodi. Zambia kupitia ZRA inatumia mfumo wa ASCUDA WORD, unaotumiwa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mifumo hii, imeendelea kutumika hata baada ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hakainde Ichilema, kukutana Agosti mwaka 2022, jijini Dar es Salaam na kuzitaka mamlaka za kibiashara kukutana, ili kubaini na kutatua changamoto zilizopo.
Katika vikao vya ujirani mwema vya Wizara za kisekta, kati ya Tanzania na Zambia vilivyoanza mwaka 2022 vilibaini kuwepo kwa vizuizi 15 vinavyokwamisha biashara katika mpaka wa Tunduma. Miongoni mwa vuzuizi hivyo ni mifumo ya kikodi, inayochelewesha uvushaji wa magari na kusababisha foleni ya malori na msongamano wa magari ndani ya mji wa Tunduma.
Tanzania ni mwanachama wa EAC na pia ni mwanachama wa SADC, hivyo inaweza kutumia mfumo wowote, TANCIS au ASCUDA WORD katika kurahisisha biashara za mipakani, kulingana na eneo.
Serikali inazungumziaje suala hili?
Kamishna wa Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha ma Mipango William Mhoja amebainisha kuwepo changamoto 15 zinazoikabili sekta ya usafirishaji katika mpaka wa Tunduma na kwamba Aprili, 2024 kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Zambia, kimetatua changamoto nne.
Katika changamoto hizo nne zilizotatuliwa mbili ni za upande wa Zambia na mbili za Tanzania. Kwa upande wa Zambia walikuwa na vituo vingi vya kutoza ushuru katika kila wilaya, pamoja na uwezo mdogo wa ukaguzi wa Kidijitali kutumia Scanna mpakani, ambapo serikali ya Tanzania imeahidi kuipatia Scanna, Zambia.

Upvote
0