Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Utangulizi
Kanuni za Tiketi Mtandao za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za mwaka 2024, zilizotangazwa na Serikali (Tangazo la Serikali Na. 23 la tarehe 12 Januari, 2024), zinaweka sharti kwamba mifumo yote ya Tiketi Mtandao inapaswa kujaribiwa, kuidhinishwa, na mmiliki wake kupata kibali cha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) iii itumike rasmi kutoa huduma kwavyombo vya usafiri wa umma.
Aidha,viongozimbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Mhe. 0kt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakisisitiza juu ya azma ya Serikali kuhakikisha malipo ya miamala yafanyika kupitia mifumo. Katika hotuba ya Mheshimiwa Rais ya kuuaga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka rrpya 2026 aieleza kuwa "Tunaanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ambapo Serikali itaendelea kutekeleza Mkakati wa muda wa Kati wa miaka mitatu toka mwaka 2026 hadi 2028 kwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kie/ektroniki katika kukusanya mapato, kufanya malipo na kuongeza umakini katika kukusanya fedha na raslima/i za umma"
Vigezo vya Kuidhinisha Mfumo wa Tiketi Mtandao
Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya Kanuni hizo, Mfumo wa Tiketi Mtandao unaostahili kupewa kibali unapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:-
uwe unamilikiwa na taasisi ya Serikali, chama cha ushirika au kampuni iliyosajiliwa Tanzania;
uwe umeunganishwa na mfumo wa usimamizi wa malipo ya mapato wa kielektroniki;
uwe una uwezo wa kuunganishwa na mifumo ya Mamlaka, Mfumo Mkuu wa Tiketi Mtandao, na mfumo wowote kama inavyohitajika;
uwe umeidhinishwa na mamlaka zinazohusika;
Utekelezaji wa vigezo hivi vya kisheria unalenga kuwawezesha wasafirishaji kupata mapato ya mauzo ya tiketi kwa ufanisi bila kupitia watu wa kati, kuwasaidia abiria kununua tiketi kwa uwazi, urahisi, bila ulanguzi, na kuiwezesha Serikali kusimamia sekta ya usafiri kwa ufanisi zaidi, huku kila mdau akitimiza wajibu wake ipasavyo.
Hatua Zilizochukuliwa na Mamlaka Kuidhinisha Mifumo ya Tiketi Mtandao Mamlaka imeendelea kutoa elimu na kushirikiana kwa karibu na wadau wa usafirishaji ikijumuisha wajengaji wa mifumo ya Tiketi Mtandao (E-Tickets Vendors) iii kuhakikisha utekelezaji kamili wa Kanuni hizi, kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri zilizo bora, salama, zenye kuaminika na kuongeza ufanisi kwa wasafirishaji
watumia huduma (abiria) na Serikali. Utekelezaji huu unafanyika kwa ushirikiano wa wamiliki wa mifumo ya tiketi mtandao na wataalamu wa mifumo wa Serikali, hususani, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Tangu kuanza kwa uekelezaji wa Kanuni za tiketi mtandao mwezi Oktoba 2024, Mamlaka imekaa vikao zaidi ya 7 na watoa huduma wa mifumo ya tiketi mtandao vikilenga kuwapa elimuna kuwakumbusha Matakwa ya usajili yanayotakiwa kutekelezwa iii kuruhusiwa kutoa huduma. Katika vikao hivyo, pamoja na mambo mengine, Mamlaka na watoa huduma walikubaliana kuwa, hadikufikia tarehe 31 Juni 2025 watoa huduma wote wawe wamekamilisha matakwa yote yanayotakiwa kutekelezwa iii kuruhusiwa kutoa huduma. Hata hivyo, hadi kufikia 30 Disemba 2025 ni watoa huduma 5 tu kati ya 15 ndio waliokuwa wamekamilisha matakwa hayo. Tarehe 30 Disemba 2025 Mamlaka ilitoa taarifa ya muda wa mwisho wa kukamilisha matakwa kuwa tarehe 14 Januari 2026.
Kampuni na Mifumo ya Tiketi Mtandao lliyoidhinishwa na LATRA
Hadi leo, tarehe 30 Januari, 2026, jumla ya mifumo 10 ya tiketi mtandao imekidhi vigezo vya kisheria na kuidhinishwa kuendelea kutoa huduma.
Kampuni na Mifumo yao ya Tiketi Mtandao iliyoidhinishwa na LATRA ni kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 1 lifuatalo:
SN JINA LA MTOA HUDUMA JINA LA MFUMO
1 AB Courier Express Limited AB Connect
2 Busbora Company Limited Busbora
3 Hashtech Tanzania Limited MySafari tiketi
4 lyishe Company Limited lyishe Company Limited
5 Logix Company Limited Msafiri
6 Mkombozi lnfotech Company Baspoa
7 Otapp Agency Company Limited Otapp
8 Sepatech Company Limited Afritech
9 Voltic Tanzania Limited Voltic Tanzania Limited
10 Web Corporation Limited Web e-ticketing
Chanzo: LATRA 2026
5. Kampuni na Mifumo ya Tiketi Mtandao lliyozuiliwa kutoa huduma
Mlfumo mingine yote ya tiketi mtandao, tofauti na ile illyotajwa hapo juu, imeshindwa kukidhi matakwa ya kisheria Iicha ya kupewa muda wa kutosha kurekebisha mapungufu yaliyoainishwa. Kwa mujibu wa sherla, mlfumo hiyo haltambuliki na Mamlaka na hairuhusiwi kuendelea kutoa huduma. Mifumo hiyo ni pamoja na ifuatayo:
Jedwali Na. 2: Makampuni na Mifumo ya Tiketi Mtandao lliyozuiliwa kutoa huduma
SN JINA LA MTOA HUDUMA JINA LA MFUMO
1. Exabytes Africa Ltd Exabytes Tiketi
2. Global Light & Company Limited Tiketi Rafiki
3. Duarani lnnovat limited Safari Yetu
4. ltule Company Limited Safiri Tiketi

Attachments
-
623360252_1388484026650893_6645664632659086433_n.jpg146.5 KB · Views: 34 -
624570427_1388483973317565_3883085917872037030_n (1).jpg157.1 KB · Views: 26 -
625126404_1388484076650888_4009979831591209390_n (1).jpg98.1 KB · Views: 35 -
625126404_1388484076650888_4009979831591209390_n.jpg98.1 KB · Views: 32