Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Hii mada nimeitoa mara nyingi naimba niitoe tena. Duniani sehemu kubwa ya migogoro inasababishwa na jambo hili. Huhitaji kuambiwa hili, linaonekana waziwazi. Mifano ni mingi kupita maelezo. India ilivunjika vipande vipande na kutoa nchi mbili ya Wahindu na Waislamu. Nigeria ilitaka kuvunjika na walipigana vita mbaya, na hadi leo iko katika hali tete sababu ya ukabila. Nchi zenye watu wa rangi tofauti kama SA na USA zinazidi kulemewa na migogoro kila leo. Ethiopia inataka kuvunjika sababu ya ukabila. Sudan ilivunjika sababu ya kidini na ubaguzi wa rangi. Leo Sudan Kusini haijatengamaa sababu ya watu wa makabila tofauti kutaka kuunda nchi.
Ukiangalia vyema duniani utaona nchi zinazostawi na kusonga mbele ni zile zinazoundwa na watu wa kabila, lugha na dini moja. Nchi kama Japan, Korea na nchi nyingine za Ulaya.
Afrika hali yetu ni mbaya kabisa. Maana huku ndiyo kunaongoza uwepo wa nchi zenye diversity kubwa ya watu. Wamarekani wanamsemo kuwa "diversity is our strength" ni kujipa moyo tu, diversity ndani ya taifa haijawahi kuwa strength hata siku moja. Ni udhaifu mkubwa kwa taifa kuundwa na watu wa makabila, dini na rangi tofautitofauti. Diversity hupasua na kuangusha nchi.
Tukitambua kuwa hilo ni tatizo kubwa tutakuwa tunaishi kwenye uhalisia. Na pengine tutaweka nguvu kubwa katika kulitatua au kulidhibiti.