Migogoro ya Ardhi Tanzania nini Ufumbuzi wake?

KISUKALI

Member
Joined
Feb 28, 2010
Posts
70
Reaction score
8
1. Wakulima na Wafugaji.
2. Wenyeji (Watanzania) na Wawekezaji toka Nje.
3. Wenyeji (wa TZ) na Wawekezaji wa Ndani (Wa TZ wenzao).
4. Wenyeji (waTZ) na Viongozi Wastaafu/Waliopo madarakani.
5. Wenyeji (waTZ) na Taasisi mbali mbali.
6. Wenyeji (waTZ) Wao kwa Wao. Na
7. Wenyeji (waTZ) Na Watumishi wa Wizara ya ARDHI.

Nadhani orodha hiyo hapo juu inaweza kuongezeka, hivi nini kifanyike ili migogoro hii ikome? Tumeona au kusikia Maisha ya Watu yamepotea, Watu wameumizana na Hasara za Mali kutokea.
Chanzo na sababu ni ARDHI.
Tuna Wizara Maalum kwa ajili ya ARDHI inawatumishi Nchi nzima chini ya idara zake na
naamini wamesoma na kusomeshwa katika taaluma husika ya maswala ya ARDHI na bila shaka wanalipwa mishahara stahili kwa kazi Waliyoomba na wakatunukiwa.
Sasa tatizzo/Matatizo yanaanzia/yanatokea WAPI???
Naomba tuelimishane:


 
Kisu, ningeomba mwenye e mail ya mama Tibaijuka au ya naibu/katibu wake awarushie hii hoja wakati na sisi tunaendelea kuijadili. nadhani kubwa k linalozusha migogoro ya Ardhi ni:
A. Kutozingaiwa kwa sheria
B. Rushwa
C.Uzembe (Kwa wafugaji) naomba mniwie radhi ni maoni tu.
Kuna mengine bila shaka.
 

Kisukali.
A. unamainisha kutozingatiwa kwa Sheria naamini.
Na hilo ndio kiini cha yote, huko"kutozingatia Sheria" ndiko kunakozaa Rushwa na mengine.
Uzembe wa Wafugaji, ntaomba ufaufanuzi. Ni vipi unachangia hii migogoro?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…