Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne


Kamundu, nimekupata. Nadhani unalaumu zaidi badala ya uhalisia. Mimi kama mbunge wa upinzani kazi yangu ni kusema, sina mamlaka ya kutenda. Kutenda ni kazi ya wenye mamlaka. Nilipotoka usa niliuliza swali bungeni kuhusu watz waishio nje. Nimesema sana kuhusu bandari zetu. Nimesema sana. Kuhusu email upo sahihi, nina uzembe huo. Ni udhaifu ambao inabidi niuondoe. Nimekiri. Tatizo kubwa nipo vijijini muda mwingi na sina blackberry. Asante kunikumbusha. Sipigi porojo, nafanya kazi.
 
Japo sina full data but I hope ntaongeza kitu.Kwa taarifa nilizozipata ni kuwa leo kuanzia saa mbili asubuhi,wanafunzi wa hapo Muhimbili watakutana kujadili namna wanavyoweza kuishinikiza 'serikali' kuwaachia wale ambao wamesemekana kuwa eti ni vinara wa mgomo UDSM mlimani.Walio Dsm wanaweza kutuletea habari zaidi.
 
Yes Mwakyj this is all we can tell our government

THOSE WHO MAKE PEACEFUL REVOLUTION IMPOSSIBLE,WILL MAKE VIOLENT REVOLUTION INEVITABLE
 
 
Mh Zitto;

Kwanza; Kwa utandawazi chukua Blackbery moja; wanazo voda naona ziko safi kabisa;popote unawasiliana ndg maana tunakutegemea sana vijana;

Pili Nashukuru kwa ufafanuzi huo; watu hawakuelewi; mie nilikuona tangu ukiwa mlimani; always uko on the respect wa matatizo ya watu; i do respect that; ila kuna kitu kimoja ambacho nafikiri inabidi kifanyike; nacho ni Chadema kuahamasisha wananchi kuhusu ni kitu gani mtafanya; mfano kampeni ya majimbo itakavyoleta faida kwa WATZ; kampeni ya rasilimali; ina utofauti gani na CCM; kampeni ya vijana na ajira inatofautiana vipi na CCM; uchangiaji elimu ya juu- chadema inasemaje?Walimu je watatuzwa vipi( maana hapa kuna watu mhimu hapa walimu) n.k. Niliziona slide za mbowe wakati ua uchaguzi kuhusu muundo wa serikali ya Mbowe kama angeshinda; was real nice; sema kwa watu ambao hawajasoma sasa mpaka ukomae sana kuwaeleza; msichoke na kukata tamaa; pia watu walikuwa wako ktk tensio hawakuzielewa maana madawa ya JK yalikuwa bado yamewashika; sasa ni muda muafaka; ni kuacha kulumbana na hawa CCMwalioshindwa kabisa sasa bali kusonga mbele kimkakati zaidi; itafikia wakatyi watakuwa wanatoa mapovu huku wengine wakisonga mbele kimkakati

Tatu; Hongera kwa kutafuta vijana kugombea nyadhifa; mkakati huo unaweza kabisa kuongeza idada ya wabunge kwa asilimia 30 zaidi toka kwa vijana tu; so hima kampeni hiyo iendelee nchi nzima;
 



Long ass post...I ain't reading all this shit...
 

...kwani wanaosoma vyuo binafsi sio watanzania? watu wana haki ya kusoma popote sio lazima vyuo vya umma tuu na wote watakuja kuijenga Tanzania,as long as chuo kinatambulika na kukubalika kwa standard za elimu ya juu sioni ubaya wa watu kujichagulia wanataka kutumia mikopo yao wapi,standard ambayo wanaweza kuweka ni kiasi cha pesa ambacho mtu anaweza kukopa kwa kutumia expenses za vyuo vya umma lakini sio lazima vile vile....kumbuka hii ni mikopo sio bure na elimu ya hao wanafunzi ni kwa faida ya Taifa zima haijalishi wamesoma wapi na serikali ijiondoe kwenye hii mikopo au iunde independent agency ya kutoa hii mikopo na kuikusanya kuliko kuwapa watu wa wizarani ambao wengi wao najua hawajui chochote na wana kazi muhimu na nyingi zaidi za kufanya
 
Kimsingi serikali imeshindwa kuwa na vipau mbele! Inazofedha tena nyingi sana lakini inashindwa ama kwa makusudi kabisa au kwa uzembe kuona kipi cha muhimu katika ujenzi wa Taifa. Wakati ni zaidi ya wiki moja sasa toka vyuo hivi vifungwe,bado serikali imekaa kimya kuhusu migomo hii.
Nilitegemea kuona ama waziri au mkuu wa kaya akitoa tamko na msimamo wa jambo hili badala yake wamekaa kimya na kama wakinong'gona ni kwenye kashughuli flani utasikia wamegusia.
Cha ajabu ni jinsi mkuu wa kaya anavyoshughulika na na maswala ya nje!Mara leo Misri,kesho states, juzi india! Loh!
Kama tunaweza kutenga bilion 4 za warsha na semina kwa wizara moja,bn 40 za ndege,mabilioni ya sh ya rada mbovu,na kama tuliweza kuilipa richmond mil 152kwa siku, kama bado tunaweza kuilipa IPTL,kama tunaweza kukopesha wawekezaji wakihindi wawalipe wafanyakazi waliowaajiri wenyewe,kama tunaweza kushuhudia mamilioni ya sh kwa ziara za siku kumi kumi mikoani ukiacha zile za mkuu wa kaya nje ya nchi,kama CCM iliweza kutoa magari kwa kila wilaya katika uchaguzi wa 2005, na kama vijisenti vya EPA havina mwenyewe vikapelekwa kilimoni,BASI,TUNAWEZA PIA KUPATA BIL 21 ZA HAO WANAFUNZI!
 


Long ass post...I ain't reading all this shit...

Mods!!! Hivi matusi yanaruhusiwa hapa jamiiforums?? Wapo watu wanadiliki kuita forums tukufu sasa kwa matusi haya huo utukufu utaendelea kuwepo nasi humu?? Some times tunajitafutia laana pasipo wenyewe kujua na tukianza kuandamwa na wana usalama tunaona tunaonewa kumbe laana tunatengenezeana humu humu ndani..... Hili halijatulia kabisa GT grow up sasa wewe ni mtu makini na wa siku nyingi humu lakini kuwa na vigezo hivyo doen't mean uvuke mipaka na kuanza kutoa lugha za ajabu namna hii, chuki zako binafsi andikianeni kwenye PM ambapo wengine hatutaona haya madudu yenu pls
 
Mkuu Koba, Hoja yangu ilikuwa hii:

Karibu kila mwaka kuna chuo kikuu kipya kinaanzishwa nchini. Serikali haiwezi kumudu kutoa ufadhili kwa vyuo vikuu vyote kwa 100%.

Sasa tuendelee!
 
Sasa basi kama hatuna uwezo wa kuvitunza vyuo vyetu vyote hivyo, kuna haja gani basi ya kuwa navyo vyote? Ni bora tukaboresha vichache ambavyo vitakuwa na vifaa vyote muhimu, kuliko kuwa na utitiri wa vyuo ambavyo hatuvimudu kuviendesha. Tusikimbilie kuwa na idadi kubwa ya vyuo bila kwanza kuweka mazingira bora ya elimu.
Ni mtazamo tu!
 
Badala ya kusafiri safiri kwenda nje ya nchi, it is high time Jakaya akatapika hiyo miguu ya kuku nakutulia nyumbani akashuhulikia matatizo; kukwepa matatizo kwa kwenda nje si suluhu ni kuyachelewesha matatizo kupata ufumbuzi. Jakaya ni lazima asome alama za nyakati wapambe wake wanamdanganya kuwa amevaa nguo!!
 
Kauli ya JK kuhusu elimu yakoroga wapinzani
Exuper Kachenje KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa serikali yake haikubaliani na matakwa ya wanafunzi kudai wakopeshwe asilimia 100 ya gharama za masomo, imepokelewa kwa hisia tofauti na wanasiasa wakieleza kuwa kwa msimamo huo taifa linaelekea gizani na kwamba athari zake hazitakawia. Serikali imefunga vyuo vyake saba kutokana na wanafunzi kugoma kuingia madarasani wakishinikiza sera ya uchangiaji elimu ibadilishwe na kama itaendelea, basi wanafunzi wakopeshwe kwa asilimia mia badala ya mpango wa sasa (means testing) ambao huchambua uwezo wa familia ya mwanafunzi na kuwapanga kwa makundi. Vyuo vilivyofungwa ni Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (Duce), Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCOBS), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT). Rais alikuwa akitegemewa kuingilia kati sakata hilo, lakini alipoingilia hakutoa nafuu kwa wanafunzi na wazazi baada ya kusema kuwa sera ya uchangiaji haitaondolewa, akifafanua kuwa enzi za serikali kutoa elimu bure zimeshapita. Msimamo huo wa Rais Kikwete umepokelewa kwa hisia tofauti. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa alisema kuwa hatua hiyo inaonyesha jinsi serikali isivyotilia maanani suala la elimu na kwamba nchi yoyote isiyotoa kipaumbele kwa elimu, ipo katika giza. Dk Slaa alisema iwapo serikali haitawekeza katika elimu kuna hatari kubwa ya kuongeza tofauti kati ya watoto wa walala hoi na wale wa vigogo ambao aliwaelezea kuwa wanapata mahitaji stahili kutoka kwa wazazi wao, hivyo kuibua matabaka na kuyakuza. "Matunda ya kauli ya Rais Kikwete yataonekana muda mfupi ujao... nchi yoyote isiyotoa kipaumbele kwa elimu, 'future'(hali yake ya baadaye) yake ipo katika giza. Kama haiwekezi kwenye elimu itaongeza matabaka ya wenye nacho na walala hoi," alisema Slaa. Aliongeza kuwa matokeo ya sera mbovu katika elimu na matabaka ya wenye nacho na wasio nacho yameonekana pia hivi karibuni wanafunzi wa vyuo vikuu, walipofukuzwa kutokana na watoto wa matajiri kufuatwa na magari ya kifahari kama Toyota Land Cruiser (shangingi), huku walalahoi wakiachwa vyuoni na hata kutafuta mikokoteni. Alisema nchi hivi sasa ipo kinyume na alivyotaka Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere na kuwa hali hiyo ni hatari na kwamba, viongozi wasitafute visingizio vya matatizo yaliyopo, badala yake wawe wabunifu ili kuinusuru nchi isiangamie. Alishauri serikali itumie rasilimali zilizopo na fedha inazokusanya ili kuboresha elimu, afya na miundombinu. Naye mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba alisema kauli ya Rais Kikwete, ni matokeo ya mpango mbaya wa matumizi katika serikali yake na kwamba hali hiyo inadhoofisha elimu nchini. Alisema tatizo ni kwamba Rais Kikwete hajatulia wala kukaa ofisini na kufanya uchambuzi wa mambo yanayolihusu taifa na kwamba akitulia na kutafakari, anaweza kupata ufumbuzi kwa manufaa ya Watanzania wote. Alisema iwapo Kikwete na serikali yake ingekuwa na mipango mizuri ya kutumia vizuri maliasili za taifa, migogoro kama hiyo ya wanafunzi isingetokea. "Hayo ni matokeo ya mpango mbaya wa matumizi ya serikali ya Kikwete. Hajatulia, hakai ofisini akafanya uchambuzi wa mambo... yeye kila siku safari na mikutano tu. Akitulia, kufanya uchambuzi wa mambo, akatafakari, atajua nini la kufanya kwa manufaa ya Watanzania," alisema Lipumba aliye safarini mkoani Mbeya. Aliongeza kuwa sera ya kuchangia elimu ya juu haitekelezeki na kuwa ni bora Kikwete akatumia fedha zilizorejeshwa na watuhumiwa wa wizi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kuondoa tatizo hilo la wanafunzi wa elimu ya juu. Alisema zinahitajika Sh23 bilioni ili kujazia katika fungu la Sh117 bilioni ambalo Bodi ya Mikopo imetengewa mwaka huu, ili kukopesha wanafunzi wote kwa asilimia 100 ya gharama za masomo. Naye, Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Mrema alimtaka Rais Kikwete na serikali yake kuangalia upya sera hiyo ya uchangiaji ambayo imekuwa ikikumbana na vikwazo tangu mwaka 1994 ilipoanzishwa. "Naona Kikwete analiweka pabaya taifa kutokana na kauli hiyo. Ni busara kwake na serikali kuangalia upya sera ya uchangiaji kwa maslahi ya taifa," alisema waziri huyo wa zamani wa serikali ya awamu ya pili. "Mfumo mzima na sera ya uchangiaji elimu ya juu una dosari nyingi na umegubikwa na harufu ya rushwa kwa sababu wanaostahili mikopo wanakosa na wasiostahili wanapewa, wasiostahili alisema ni watoto wa vigogo na watu wenye uwezo kiuchumi. Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Anthony Machibya alisema serikali yake itatoa tamko rasmi dhidi ya kauli hiyo ya Rais Kikwete. Wakati huohuo, serikali imesema uamuzi wa kufunga vyuo vikuu utaisababishia serikali hasara kubwa. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Gaudensia Kabaka alikiri hayo wakati akitoa msimamo wa serikali kuhusu sera ya uchangiaji wa elimu ya juu na hatua zilizochukuliwa na serikali. "Zipo hasara zitokanazo na kufungwa kwa vyuo vikuu hapa nchini ambazo serikali imezipata, lakini ni vigumu kubashiri kwa sasa ni kiasi gani hadi hapo tutakapofanya uchunguzi na kugundua kiasi hicho na ndipo tutaueleza umma wa Watanzania upate kuelewa," alisema Kabaka. Alidokeza kuwa moja na hasara inayoonekana dhahiri ni mishahara ambayo inalipwa kwa wafanyakazi wa vyuo hivyo bila ya wao kufanya kazi. Alisema kutokana na serikali kutambua hilo imeziagiza kamati za vyuo kufanya uchambuzi wa majina ya wanafunzi wanaokubaliana na sera ya uchangiaji na kuwarudisha haraka vyuoni, ili waendelee na masomo. Kutokana na kufungwa kwa vyuo hivyo, polisi inamshikilia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (TAHLISO), Julius Mtatilo na imemfukuza nchini mwanafunzi kutoka Uganda, Odong Kefa Odwar, ambaye amedaiwa kuvunja sheria za nchi kutokana na kujihusisha na siasa na uchochezi wa migomo vyuoni.

Source: Mwananchi Jumatatu 24th November 2008

My Take:

TUMEKWISHA!!!! Tusubiri miujiza tu katika nchi hii, lakini taifa limeanza kupoteza mwelekeo
 
,,..nilitazama hotuba aliyokuwa akiisoma rais...alijitahidi..au walijitahidi kumuandikia hotuba kwa tahadhari sana ....lakini nilichokiona kwa hadhira ya wasikilizaji hasa wale wanafunzi wa SAUT.....Ni dharau za wazi dhidi ya rais wakati anasoma hotuba....wengi walionekana wamelala..,wengine wanaendelea na mazungumzo ...ili mradi kila mwanachuo alikuwa busy na lake...ukiachilia mbali wazazi na ndugu ambao kidogo walionekana kusikiliza hotuba....mood ya hadhira kwa jumla ilikuwa chini sana....pamoja na jk mara nyingine kwenda off speech kwa kuleta story za hapa na pale wapi....

....watu pekee walioonekana kumsikiliza kwa makini ni maaskofu ..aliokuwa nao pale ...na ndio waliokuwa wakimpigia makofi ya hapa na pale kumtia moyo.....

...
 
Takrima ime-backfire!

Rais alikuwa akitegemewa kuingilia kati sakata hilo, lakini alipoingilia hakutoa nafuu kwa wanafunzi na wazazi baada ya kusema kuwa sera ya uchangiaji haitaondolewa, akifafanua kuwa enzi za serikali kutoa elimu bure zimeshapita.



Wakati mnatoa hizi hela, mbona hamkusema kuwa hii ni takrima? Kwa kauli ya Raisi, maana yake huu sio mkopo tena, au?

Ni dhahiri kuwa hela hii ikitolewa, serikali haikuwa na mipango yoyote ya ukusanyaji, maana kwa ufahamu wao, hii haikuwa mikopo bali ni takrima (lambalamba, toto isipige kelele).




.
 
Watanzania tunashangaza sana. Hawa jamaa wa CCM waliweka wazi kwenye ilani yao, tena mapema kabisa, kuwa watakuwa na sera ya uchangiaji elimu. Tukawafurahia, tukawapigia makofi, tena wanafunzi wa mlimani wakambeba JK juu kwa juu, na kisha tukamchagua kwa mbwembwe. Leo anatekeleleza hizo sera ambao tulimchagulia, tunamgomea. Nani hamnzao hapo, sisi au CCM?
 

Si wote walioipigia kura CCM na/au JK. Si wote walioipigia kura CCM na/au JK walikubaliana na yote waliyoahidiwa. Vile vile ni haki ya wananchi kubadilisha mawazo.

Ni haki ya mwananchi kugoma, kuandamana kama hakubaliani na anayotendewa na walio juu yake. Ni haki ya mwananchi kusinzia wakati wa hotuba ya yeyote ile. Si haki ya mwananchi kuwasumbua wenzake wanaotaka kusikiliza hotuba. Hili lakini si kosa la jinai. Kama kuongea kwa hao wanafunzi kulikuwa kunamsumbua mtoa hotuba, ange-pause na kuwaomba wanyamaze. Kama wangeendelea basi wasimamizi wa shughuli wangekua na haki ya kuwatoa nje ya chumba cha mkutano.
 


Kitila Mkumbo:

Wewe ni Kadra wa CHADEMA. Mpaka sasa hujasema wewe ungekuwa madarakani ungefanya nini?

Mimi sio mwanasiasa. Ninalipa kodi na nimejisomesha mwenyewe kwa ku-flip burger Marekani. Na sioni sababu yoyote mwanafunzi kukubali na kutia sahihi kuwa anaweza kujisomesha kwa mkopo wa 60% na baadaye kubadili kibao na kusema anataka 100%.

Kuwalipia gharama wanafunzi gharama 100% ni kuongeza kodi na kama kodi haitaongezwa basi bajeti za huduma zingine kama vile elimu ya msingi au sekondari itabidi zipunguzwe.

Basi mkija hapa mtupe alternatives na kama ni kulaumu CCM tu bila kutoa alternatives tutaendelea kuchagua CCM.
 

mkuu KITILA,
Acha ku-generalize mkuu.JK ana miaka 3 sasa Ikulu.hii ina maana kuwa walioko mwaka wa kwanza hadi wa tatu kwenye hivyo vyuo hawakuwa vyuoni wakati huo na hivyo HAWAKUBEBA.Wakati huo wa vyuo kama DUCE na Mkwawa hawakuwepo bado.sasa una maana gani kuwawekea vijana wenzio maneno yako midomoni mwao??kuwa specific tafadhali,hasa hayo maneno niliyo bold hapo juu
 
...well,hii hii kitu ya kudai serikali lazima itoe 100% nafikiri ni kukosa kufikiria vizuri,yaani kwa nini mtu wa elimu ya juu asomeshwe kwa 100%,nafikiri hiyo haki ya 100% iishie secondary school lakini mpaka college?kwa nchi maskini kama Tanzania ni kujidanganya tuu na haitawezekana..lazima wengine wajisomeshe sio kudai bure tuu,acha maskini wasiojiweza ambao wana akili wapate hiyo 100% lakini nina uhakika wengi wana uwezo wa kuchangia kidogo na lazima wachangie,JK naye lazima awe mkweli sio ubabaishaji tuu either wape 100% na kata idadi ya wanafunzi au wape only tuition & fees,books,fees then board & meal wajijue kuliko kufunga vyuo na poor education ya kujaza madarasa kupita uwezo bila vitabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…