Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Kufungwa kwa chuo kikuu mapema wiki jana ni mwendelezo wa kile kilichozungumzwa mapema tu na wanafunzi wa Elimu ya Juu wakati huo ilipoanzishwa sera ya Mikopo ya Elimu ya Juu wenyewe wanaiita sera ya uchangiaji wa Elimu ya Juu.
Watu hawa ambao wazazi wetu wanahenya kufanya kazi na kuwapa uwezo wa kiuchumi wasomi hawa ( ambao ndio viongozi wa sasa) wanaoongoza serikali ambayo haina uwezo wa kusomesha watu wake hivi leo sasa je tunaweza kusema Ellimu ni ukombozi wa maisha ya wanadamu au ni ukandamizaji wa mwanadamu?. Wakati tulipokuwa na wasomi wachache kwenye nafasi za juu serikalini serikali ilikuwa na uwezo mkubwa kabisa wa kusomesha wananchi wake lakini sasa serikali ina rasilimali watu ya kutosha hali tunaambiwa ni mbaya.
Sasa hivi haishangazi professa wa afya kudai usingizi si muhimu kwa mwanadamu na kwamba la muhimu ni kusoma tu nina maana tamko la Mkuu wa chuo cha afya muhimbili wakati wanachuo walipokuwa wanadai huduma za hostel. Vihivyo Professa Maghe'mbe Waziri wa elimu na mafunzo ya Utamaduni ambaye kama professa ni mtu anyechambua mambo lakini badala ya kwenda chuo kikuu Dsm kuwaeleza wanafunzi umuhimu wa sera hiyo kama hata yeye anaiamini lakini lakini badala yake alitumia media kuwaonya wanafunzi badala ya kuwashawishi. Mwanasiasa yeyote bora ni lazima awe na ushawishi kwa wapiga kura wake sasa inakuwaje hojazako uziogope mwenyewe?. Ipo mifano mingi sana ambayo wasomi wa sasa wamevuruga na wala hawajawahi kukiriudhaifu huo sasa je ni elimu gani watu hawa waliipata?
Ni elimu ya ukombozi kweli au ni ya unyonyaji ? yako mengi mno lakinininachoweza kusema Adui wa wanafunzi wa elimu ya juu ni sheria hivyo mapambano yao ni sahihi kabisa aluta continua.
 
Mitihani ya mwisho wa mwenzi ndio sababu ya kuwagomesha?Maana taarifa zinasema ni sababu ya kudai kulipiwa mkopo aslimia 100.

Achana na huyu anaeongea asichokielewa.Kwani kuna mitihani gani inafanyika kipindi hichi?Namshauri akatafute ratiba!Mitihani ni mwisho wa semister na kwa wengine ni mwisho wa mwaka sasa hapa vinahusianaje!
 
Watanzania kweli hali ni ngumu,,sasa hawa mawaziri na nduguzao wanasaidia nini ???hawa ni takataka kabisa huwezi funga kila chuo bila kujua ama kutafuta sababu ninini???
Matokeo yake unashabikia funga funga ,,watawafunga mpaka wake zao!!watanzania tuandamane kuwalazimisha hawa watu wajiuzulu
kuliko kucheza na elimu ya tanzania

magembe gooo gooooooooooooooooooooooo
mkandara go goooooooooooooooooooooo
 
Kevo, tunakuaminia sana usijishushie hadhi. Maana mchango wako hapa hauko sawa na hadhi ya michango yako ninayoiona humu.
 
Kwa vile wanafunzi wanaosoma kwenye vyuo vya serikali tu ndio wamegoma kuashiria kutorudhika na kiwango cha mkopo wanachopewa, wanafunzi katika vyuo binafsi wao hawajagoma kuashiria wameridhika.

Serikali iwafikirie hawa ambao hawajaridhika na kiwango cha mkopo na wawape kwa kiwango cha asilimia mia moja. Hao wanaosoma katika vyuo binafsi waendelee kupewa mikopo kwa mafungu kwani wameridhika.
 
Watanzania kweli hali ni ngumu,,sasa hawa mawaziri na nduguzao wanasaidia nini ???hawa ni takataka kabisa huwezi funga kila chuo bila kujua ama kutafuta sababu ninini???
Matokeo yake unashabikia funga funga ,,watawafunga mpaka wake zao!!watanzania tuandamane kuwalazimisha hawa watu wajiuzulu
kuliko kucheza na elimu ya tanzania

magembe gooo gooooooooooooooooooooooo
mkandara go goooooooooooooooooooooo

Supported mama, I have many things to write here, kindly watanzania tuungane ktk hili, by the waym,is those solutions that professors has to take??????

Magembe--goooooooooooooooooooooooo
Mkandara-gooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

waberoya
 
What about Kikwete and Mkono?
 
hehehe wakati yote haya yanatokea...serikali yetu tukufu teule tuliyoiingiza madarakani sisi wenyeweee iko kimyaaaaaa sio waziri husika,wala waziri mkuu or raisi..!!labda tusubiria tume husika iundwe if not hotuba ya mwisho wa mwezi ya raisi atakayoitoa akiwa njiani kuelekea........kwa mijihela yetu
 
Sio Vyuo bali ni chuo kikuu kimoja. Lazima tujiulize je ni kwanini hiki chuo pekee ndiyo kina migomo?
 
Chadema yahusishwa na migomo vyuoni
Waandishi Wetu, Dar na Iringa
Daily News; Sunday,November 16, 2008 @20:11

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetajwa kuhusika katika vurugu za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, kikidaiwa kuwa mfadhili wa vurugu hizo zilizotokea wiki iliyopita na kusababisha vyuo kadhaa kufungwa.

Hata hivyo, chama hicho cha siasa cha upinzani, kimekanusha kuhusika na ufadhili huo ambao unadaiwa kufanywa kwa wasomi hao wa elimu ya juu.Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema, John Mnyika alikanusha madai hayo juzi akiwa kwenye kongamano la wasomi na vijana lililofanyika kwenye Ukumbi wa Community Centre mjini Iringa.

Mnyika alikanusha madai hayo kwamba Chadema ndiyo inayofadhili, kuratibu na kuhamasisha migomo vyuo vikuu.Hata hivyo, alisema Chadema iko nyuma ya wasomi hao na inaunga mkono harakati zao za kudai haki zao.

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, Chuo Kikuu cha Elimu Chang’ombe (DUCE), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa Iringa, vimefungwa au kusimamisha wanafunzi wake wiki iliyopita kwa sababu ya kufanya vurugu wakiishinikiza serikali kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi hao.

Aiwa kuwa wanafunzi hao wakiwamo wale wa vyuo vya Dar es Salaam waliosimamishwa, wamekuwa wakifadhiliwa na Chadema kufanya vurugu hizo na yapo madai ya kukodiwa magari kwenda Iringa kushiriki katika vurugu Mkwawa.

a upande wake, akizungumza katika kongamano la Iringa juzi, Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (Chadema), aliwataka wanafunzi wa vyuo hivyo kutorudi nyuma katika kupigania haki zao na kuwahamasisha wajiunge na chama hicho alichodai kinalenga kuwatumia vijana zaidi kuleta mabadiliko nchini.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), alisema migomo inayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu na idara nyingine za kiserikali nchini inadhihirisha jinsi Watanzania walivyoanza kuzitambua na kuzidai haki zao za msingi ambazo wanaamini serikali yao inaweza kuwatatulia.

Katika hatua nyingine, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, amewataka wanafunzi wa vyuo nchini, kuheshimu na kufuata taratibu zilizopo, katika kuwasilisha malalamiko, maoni na mapendekezo yao sehemu husika, ili kuepusha misuguano inayojitokeza mara kwa mara, baina ya uongozi wa vyuo na wanafunzi.

Amesema kama misuguano iliyopo itaendelea, itaathiri mfumo mzima wa upatikanaji wa elimu kwa vyuo hivyo sanjari na kusababisha vyuo kufungwa na wanafunzi kufukuzwa.Waziri Kiongozi, aliyasema hayo kwenye mahafali ya tatu ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho, Dar es Salaam juzi.

“Watanzania hawapendi kuona hali kama hii inaendelea vyuoni, nawasihi wanafunzi kwa kupitia jumuiya na serikali za wanafunzi na waendeshaji wa vyuo kwa pamoja kushirikiana ili kuepukana na matatizo haya yanayojitokeza mara kwa mara,” alisema Nahodha.

Pia, aliwashauri viongozi wa vyuo kuwa karibu zaidi na wanafunzi kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua matatizo yao kwa wakati na kwa njia mwafaka, kabla ya tatizo kuwa kubwa na kupelekea madhara kwa taifa.

Aliwasihi wanafunzi kutojihusisha na fujo au maovu mengine, na kuzingatia zaidi masomo, na alisisitiza kuwa, kuhitimu kwa ufanisi kutatoa fursa kwa wao kufungua mlango wowote katika maisha, sambamba na kulisaidia taifa katika kutatua matatizo mbalimbali ya kimaendeleo.

Aidha, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya changamoto zinazokikabili Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, alisema katika kukabiliana na ongezeko la udahili kwa wanafunzi chuoni hapo, serikali zote mbili, zimejidhatiti kushirikiana na uongozi wa chuo, kujenga tawi la chuo hicho eneo la Bububu, Zanzibar, ili kutoa fursa kwa Watanzania walio wengi zaidi kupata nafasi ya kujiendeleza.

“Nimefurahi kusikia idadi ya wanafunzi wanawake ni kubwa kwa wastani wa asilimia 54.01, kuliko wanaume, wastani huu unaendana na azma ya serikali ya kuwa na uwiano ulio sawa wa kijinsia, katika nyanja zote,” alisema. Nahodha.

Alisema elimu ndio njia pekee ya kumuwezesha mwanamke kupata fursa sawa ya ushindani katika soko la ajira, hivyo alitoa mwito kwa vyuo vingine vya elimu ya juu kuiga mfano huo kwa kuongeza idadi ya udahili kwa wanawake pasipo kuathiri daraja za elimu au sifa za kuingia vyuoni.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Dk. John Magotti, alisema wanafunzi 300 wamehitimu katika mahafali hayo katika ngazi ya Cheti katika Kazi za Vijana, Stashahada ya Masuala ya Jinsia katika Maendeleo, Stashahada ya Taaluma za Jamii na Stashahada ya Maendeleo ya Uchumi.
 
Huku ni kufilisika kisiasa kwa CCM. Badala ya kukaa chini ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo chungu nzima yanayowakabili wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Tanzania, wanataka kuwabambikia CHADEMA kama wao ndiyo wanaofanya uchochezi wa matatizo haya. Sitashangaa kusikia kwamba CHADEMA pia inahusika na migomo ya Waalimu, malalamiko ya Wastaafu wa EAC na matatizo ya ndani ya CCM. Inaelekea CCM wanawahofia sana CHADEMA ambao pia wameshaitwa 'chama cha kikabila' na CCM.
 
Sidhani kama kuna Jipya, Wanafunzi wamekaribia Mitihani hao na wamestuka hawajasoma sawa sawa ndio maana imekuwa sababu tulipita huko. Kuhusu Mvungi; nafikiri asiwe Mnafki kwasababu suala la uchangiaji wa Elimu upo pote duniani na suala la mikopo linaeeleweka duania nzima hasa ukizingatia muda huu wa Credit Crunch.
 
Tatizo letu watanzania siku zote, huwa hatuwezi kutenganisha siasa na mambo mengine.
Sasa huyu mweshimiwa wetu anayeingiza siasa na masuala ya wanafuzi mi nashindwa kumwelewa kabisa.
Tatizo kama hilo limejaribu kujitokeza hapa uk lkn maprofessor wa vyuo vikubwa hapa nchini kama wa un of london wamelikemea na likafanikiwa kwetu maprofessor wetu sijui hawasikilizi au ndio akina Lipumba?
 
La kufadhili migomo kwa Chadema kama chama naunga mkono sio kweli ila la kuhamasisha hili linaweza kuwa na ukweli kidogo kwa sababu Mnyika amemaliza chuo juzi juzi na yuko mstari wa mbele katika harakati zinaowahusu wanachuo.

Naunga mkono mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa asilimia 100. Lakini pia wale wazazi wenye uwezo kama mlivyosomesha wanenu hizi shule za Academy na ma sekondari
Kama Agha Khan ambazo ni ghali kuliko Chuo Kikuu si ni mchangie!.
 
aiseee kama kweli chadema inahusika itabidi nihamie chadema maana malalamiko haya yanaakili kabisa wale wote wenye vijisenti hawawezi kuelewa haya lakini kamuulize mzee wa kule kwetu Kidali kuchangia asilimia 40 ya shilingi elifu hamsini ni issue kubwa, sasa hawa chadema wameshaelewa hilo kwa maana hiyo tukiwaunga mkono wataweza kurudisha usawa katika nchi yetu tutarudi kwenye enzi zile ambazo professor alikuwa akielezea jinsi alivyokua akienda shule bila kunywa chai akafanya bidii katika masomo akachaguliwa kwenda chuo kule alivyokuwa anasoma aliweza kutumia hela kuwasomesha wadogo zake. sio siku hizi yani kama mzazi mkulima mwishoooooooooo wako form six..... na hawa wanaoingia wanabebwa bebwa tu ndo maana nchi hii sasa haifikirii maskini maana wengi hawaujui mimi naomba kama kuna mtu huku anayewajua hawa watu tuwasiliane kwa PM nataka kutia nguvu mpaka kieleweke
 
Tatizo la uchangiaji wa elimu ya juu limesababishwa na serikali kucopy sera zinazoundwa na IMF bila kuangalia applicability yake katika mazingira ya TAnzania.
 
Tatizo la migomo limechangiwa na vitu vingi sana.Kwanza watu wamechoka kuona wizi wa fedha za umma na very poor allocation of available resources tulizonazo.
Maadili ya kisiasa yameshuka maana watu wapo ofisini kujinufaisha wao na familia zao.Wanafunzi wa vyuo vya umma ndio wanaadhirika sana ila angalia private universities shida ndogo kama hizi hawana!
Mfumo wa kielimu uliowekwa tangu siku nyingi ni mbovu sana na unahitaji marekebisho makubwa sana maana sekta ya elimu ni sekta mihimu sana katika ujenzi wa taifa lolote liwe.
 
•

Na Francis Godwin, Iringa

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema hakuna sababu ya serikali kuendelea kuwabagua wanafunzi wa vyuo vya juu katika madaraja wakati kuna rasilimali chungu mzima ambazo zinatumika isivyo halali yakiwemo madini ambayo yangeweza kabisa kusaidia kulipa ada za wanafunzi hao.

Kabwe ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Kikwete kuchunguza Sekta ya Madini nchini amesema wakati umefika kwa Watanzania kufanya tathimini ya kina ili kuepuka kuendelea kufanya kosa kwa kuchagua viongozi wa CCM.

Kiongozi huyo, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema alisema hayo jana alipotoa hotuba kwenye kongamano la wasomi Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Community Centre mjini hapa.

Kabla ya kongamano kuanza, Kabwe alipata mapokezi makubwa kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mkwawa ambao juzi walisimamishwa chuoni hapo baada ya serikali kukifunga huku akiwataka wasisikitike na yaliyowakuta ya kufukuzwa chuoni.

Pamoja na mapokezi hayo makubwa aliyoyapata na kupelekea umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa ambao walifukuzwa chuoni hapo toka juzi na kulazimika baadhi yao kurudi makwao na wengi wao kuendelea kusota mjini hapa pia viongozi wa vyama vya upinzani na wanachama wa CCM walifika kwa wingi katika ukumbi huo.

Katika hotuba yake alisema kuwa Chadema imepokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa serikali wa kuvifunga vyuo vitatu hapa nchini kwa kisingizio cha wanafunzi kushindwa kutii agizo la serikali la kuwataka wasigome.

Alisema kuwa huo ni uonevu wa hali ya juu ambao kwa chama chake kimepokea kwa masikitiko makubwa na kuwataka wanafunzi hao kujifunza ubabe wa serikali yao inayoongozwa na CCM.

Akihotubia huku akishangiliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu hasa wanafunzi wa chuo cha Mkwawa ambao kwa sasa wanaishi maisha ya kuhangaika mjini hapa kutokana na baadhi yao kukosa nauli za kurudi kwao, Zitto alisema kuwa wakati umefika kwa wanafunzi hao kurudi katika vijiji vyao na kwenda kuhamasisha wananchi kusaidia kutoa hukumu kwa serikali iliyopo madarakani kwa kutowachagua viongozi wa CCM.

Alisema kuwa baadhi ya kata na majimbo wananchi wake wameanza kutoa hukumu kwa CCM kutokana na mambo yanayofanyika na hata kufanya mabadiliko ya viongozi wake kwa kuwachagua viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakiwajibika ipasavyo kwa wananchi tofauti na wale wa CCM ambao wengi wao wanajinufaisha.

Wakizungumza katika kongamano hilo, wanafunzi hao walisema kuwa pamoja na baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere kukemea kwa nguvu zote suala la ubaguzi, bado serikali ya awamu ya nne inayoongozwa imeendelea kuwabagua wanafunzi kwa kuwatenga katika madaraja hasa katika suala la mikopo ya elimu ya juu na mbolea.

Walisema kuwa hivi sasa wanasubiri viongozi wa CCM wamalize muda wao mwaka wa miaka mitano tangu wachaguliwe mwaka 2005 na baada ya hapo wawapishe viongozi wa upinzani waweze kusimamia nchi ili isiyumbe zaidi.

“….Ujue kabisa Rais Kikwete nchi hii imemshinda kutokana na hali ya huruma aliyokuwa nayo na kupelekea wasaidizi wake kuendelea kufanya vile watakavyo…kwanza hata hawa mafisadi wa EPA waliofikishwa mahakamani ni kiini macho wapo vigogo hasa ambao tulitegemea watafikishwa mahakamani ila wamefichwa,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Majira Mobile
 
Serikali bila kujua inaongeza ukubwa wa jeshi la ukombozi. Kazi inazidi kuwa rahisi kweli kweli.

Tatizo kubwa linabaki kuwa ujinga wa WaTz, ambao kesho wanaweza kuandamana kuipongeza serikali kwa kitendo cha kuwafukuza watoto wao vyuoni. Tukimalizana na hilo kazi itakuwa imefikia kikokomo. Wanafunzi warudi vijijini wakaifanye hiyo kazi na hii itawahakikishia kuwa wakirudi madarasani kazi yao itakuwa ni kusoma tu badala ya kukimbizana na mamluki wa Bodi ya mikopo!
 
Back
Top Bottom