Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
MWANAMUZIKI Miguel Jontel Pimentel (33) kutoka San Pedro amefunga pingu za maisha na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Nazanin Mandi, toka California Santa Susan (32), California, Jumamosi Novemba 24, mwaka huu.
Kupitia akaunti zao za instagram, wawili hao waliwatangazia rasmi mashabiki tukio hilo ambapo kwa upande wa msanii huyo wa Miguel aliandika, “Kumbukumbu zisizosahaulika timeshare na familia pamoja na marafiki wa karibu. Shukrani kwa kila mtu ambaye ameifanya siku yetu kutosahaulika. Tunawapenda wote”.
Miguel na mpenzi wake Nazanin walijuana toka walipokuwa na umri wa miaka 18, walianza ku-date pamoja mwaka 2005 na walivishana pete za uchumba Januari 2016.
Staa huyo aliwahi kutamba na kibao cha ADORN na SKYWALKER akimshirikisha Travis Scott ambazo ziliwahi kushika chati za juu za Billboard