Miguel Gamond ni kocha aliyekuja kuvuruga maana halisi ya "kikosi kipana"

TUSINGE PIGA MAKELELE TUSINGEMUONA FARIDI MUSA, KIBWANA SHOMARI, MOLOKO NK.
Kwani kocha kawapanga sababu ya kupiga kelele kwenu au sababu kaona Mtibwa timu nyepesi, yupo kwenye uwanja wenye pitch nzuri na jumanne ana mechi ngumu dhidi ya klabu bingwa hivyo ni muhimu kufanya rotation. Wewe unadhani angecheza na Azam au Simba au Namungo ungeona jambo kama hilo? Au zile mechi za Asas, Al Mereikh, JKT Tanzania, Kmc,Ihefu, ni nyie ndio mliopigia kelele akawa anafanya zile rotation kila mechi? Acheni nongwa jamani
 
Sisi Furaha yetu ni kuona wanacheza
 
Hayo Mambo ya mchezo mwepesi yeye hajazungumza Ila wewe ndiyo umekuja kuyazungumza.
 
Sisi Furaha yetu ni kuona wanacheza
Furaha zenu na ya kocha huenda zikawa zinatofautiana, wakati nyie mnafurahia kuona wachezaji wanacheza, kocha yeye furaha yake ni kuona timu yake inashinda, Na hapo ndipo mnapopishana kiu ya kuona.
 
Sio kila kitu lazima uambiwe, vingine unatumia akili na utashi kung'amua. Kwani ya kupigiwa kelele alizungumza napanga kwasababu ya kelele?
Nenda kasikilize press yake kabla ya mchezo alizungumza Nini kuhusu mashabiki kutaka ROTATION
 
Nenda kasikilize press yake kabla ya mchezo alizungumza Nini kuhusu mashabiki kutaka ROTATION
Alisema nini, wewe uliyesikiliza mnukuu hapa alichosema. Wabongo mnapenda kujifanya wajuaji kwa kila kitu. Hata mechi ya leo, ilipotoka tu wachezaji walioanza kikosi cha kwanza wachambuzi uchwara na wanga wakaanza "Hii mechi Gamondi hatoboi, watu walitaka rotation lakini sio kwa wachezaji wengi hivyo" wengine walishaanza kumtafutia sababu ya kufungwa leo. Nabi alipigwa vita na maneno maneno ya wajuaji hivi hivi ila bila uongozi kusimama katika malengo yao na katika kile wanachokiamini basi Nabi angeshatimuliwa muda mrefu tu kwa nongwa za wacha mbuzi wa kibongo.

Ni sawa na Ganondi kwasasa watu ambao hajawahi kufundisha hata timu za mtaani kwao wanaojifanya wanajua kufundisha Yanga. Yanga haikuwahi kuucheza soka la hivi hata alivyokuwa Plujim wala Nabi. Hili soka la Gamondi hutamani mpira uishe nyie endeleeni kupiga kelele tu ila huyu hafukuzwi ng'oo. Hapo tu straika tegemeo ni Mzize.
 
KUNA MAHALA NIMESEMA AFUKUZWE??

JENGA HOJA ACHA MIHEMKO.
 
Nabi tulimpenda, lakini sasa tupo na gamond.
Shabiki bora siku zote lazima awa support kocha, na wachezaji waliopo lakini kocha lazima aaminiwe zaidi kwa maamzi yake na sio kumpinga au kumkosoa.
niko na gamond 100% hata tusipofuzu robo final CAF
 
Mimi pia nimefurahi kumuona Faridi Musa, Kibwana Shomari, Moloko nao wakipata Nafasi.
Farid musa sawa upo sahihi , lakini moloko amecheza sana chini ya gamondi vuta kumbukumbu, mechi ya belouzidad na ya Al ahly alikuwa anaumwa .
Mechi ya ihefu kibwana na sureboy walicheza .
Yote kwa yote yanga ina kikosi kipana 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…