binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
Mhhh what happened to baba wa Demokrasia? Wapiga zumari wa kibongo humpamba sana huyu baba.Hakuukana uraia wa Kenya wakati alisajili uraia wa Kanada kipindi hicho tukiwa kwenye katiba ya zamani, ambayo haikuruhusu uraia pacha. Baada ya kuzinduliwa kwa katiba mpya, alifaa kuomba uraia wa Kenya ili awe raia wa nchi zote mbili, sasa kaichukulia poa na kuendelea na harakati zake.
Kwa kifupi serikali ya Uhuru sasa hivi imepanic baada ya tukio la Raila kujiapisha, huu ni wakati hatari kwa mtu yeyote anayeichokonoa serikali, bora uhakikishe stakabadhi zako zote ziko poa, mamlaka ya kodi wasiwe na issue na wewe, yaani uwe msafi kama pamba maana sasa hivi usalama wa taifa wanazunguka kote kote na wapo tayari kufanya lolote, hatari sana. Hata wanakiuka amri za mahakama bila kupepesa macho.
Wabongo wanapenda sana kujidharau wakati Africa ni ile ile.