Huyu jamaa huwa ananikosha sana, sio kwa ujeuri wake huu. Ila jamaa mwenyewe ni 'very brilliant', na ni 'alumni' mwenzangu na alikuwa kiongozi pia, ndani ya SONU, kwenye 'alma mater' yangu The UoN. Mwezi uliopita nilimaliza kusoma kitabu chake cha pili, Kidneys For The King, ambacho alikiandika alipokuwa 'senior adviser' wa RAO. Alimponda kweli kweli swahiba wake wa zamani Raila Odinga na akafichua 'siri' nyingi za kisiasa ndani ya serikali ya muungano, GNU. Hakuna aliyesazwa kwenye kitabu hicho, ambacho alikibatiza 'Book of Revelations', kutoka kwa rais mstaafu Mwai Kibaki hadi CJ wa enzi hizo Willy Mutunga. Ukisoma vitabu vyake, kando na ujeuri wake wa kawaida, utaelewa kwamba Miguna Miguna sio mnafik na huwa anaamini anachokihubiri. Anyway, welcome back Mr. Am not boarding this plane! Long live democracy! Rais Uhuru akimuhakikishia Miguna Miguna kwamba ni haki yake kurejea na kwamba haki yake ya kujieleza italindwa pia.