Ndio nimeanza kusoma Peeling Back the Mask: A quest for Justice in Kenya,huyu jamaa hakika ana kipaji kikubwa cha kusimulia,nipo bado mwanzoni kuna sehemu ninaposoma hunifanya nicheke sana,ni mwandishi mzuri sana,tatizo ninaloliona ni malezi yake ya utotoni yanamfanya yeye ajione anaonewa wakati wote kwa hiyo hana budi kupambana kwa hali yoyote,pia si mtu wa kusamehe ana visasi na mwisho ni mtu ambaye sisi huko TZ tunaita mtu wa maringo lakini hiyo pia ni kutokana na mila za kabila laki ambao hupenda kujikweza huko kwetu TZ tuna kabila linaitwa Wahaya ni kama Baganda(?)wa Uganda ambao ni watu wa kujisifu.Kwa sisi waafrika kimila kuna mambo ambayo hata kama unayajua huyaweka chini ya zuria,MM ni lafi/mroho ndio maana alirudi nyumbani akitegemea madaraka makubwa hata hayo aliyopewa aliona hayatoshi,kwa sasa abaki awe mtunzi wa vitabu tu poor MM tamaa ilimponza fisi.Pamoja na yote jamaa ni mwandishi mzuri na anajua kupamba uandishi wake ambao hufurahisha sana na ila akikasirika haoni mbele.