GE2025 Mihayo: Kila chombo cha habari kuwa kiungo cha ukweli, siyo propaganda, hasa katika kipindi cha mitazamo tofauti

GE2025 Mihayo: Kila chombo cha habari kuwa kiungo cha ukweli, siyo propaganda, hasa katika kipindi cha mitazamo tofauti

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Vyombo vya habari nchini vimeaswa kusimamia ukweli na kuepuka propaganda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, katika kipindi ambacho jamii ina mitazamo, sera na itikadi mbalimbali.

Wito huo umetolewa leo Septemba 25, 2025 jijini Dar es Salaam na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, aliyewahi kuwa Rais wa nne wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa baraza hilo.

“Ninavisihi vyombo vya habari vibebe ujasiri huu, maana huo ndio ushahidi wa uhuru wake. Ujasiri gani huo? Ni wajibu wa kila chombo cha habari kuwa kiungo cha ukweli, siyo propaganda, hasa katika kipindi cha mitazamo tofauti,” amesema Mihayo.

 
Ni msimu wa mavuno. Vyombo vya habari ni biashara kwanza; na waandishi wake ni machawa wanaotegemea uteuzi.
Kwa kifupi, hakuna vyombo vya habari, wala waandishi wa habari wa kutegemewa.

Kuyabadili yote haya ni kuwaondoa watawala wanaotengeneza muundo wa kuwabakisha madarakani kwa kutumia njia mbalimbali, kama hivyo vyombo vya habari na waandishi wake.
 
Back
Top Bottom