Mihemko na kupanic ndio tatizo mtambuka la vijana wa Kitanzania

Mihemko na kupanic ndio tatizo mtambuka la vijana wa Kitanzania

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Imekuwa ndio utambulisho wao, na vyama vyao. The tone of their articles, styles of their replies and comments, the languages they use in conversations and engagements, represents fully their political blocks they belong.

Mihemko, panic, ghadhabu na hasira miongoni mwao zimekua zikiwachochea kuhitimisha hoja zinazo ibuliwa dhidi ya masula mbalimbali humu nchini, kwa kutukana na kuporomosha matusi yasiyo na tija, maana wala faida yoyote kwa mustakabali wao.

Bali kuchochea migawanyiko zaidi miongoni mwao kwasababu mtukanaji na asie mtukanaji hawawezi kua na umoja, lakini pia kua na lengo au nia moja. 🐒

Kumpambania malengo na vipaumbele vya vijana na ili vifanikiwe panahitajika umoja, nidhamu na heshima ya kiwango cha juu sana miongoni mwao.

Hali ya kundi fulani kujiona ndilo bora zaidi kwa matusi bila hoja, na kwamba wanachoibua wao hata kama hakina maana yoyote, wanataka kisi hojiwe au kuwa challenged kwa hoja, bali kiwe hivyo hivyo kadiri watakavyo wao.

Hii si sawa na haina afya kwa umoja miongoni mwa vijana.

Hali hii isipobadilika, itawachelewesha sana vijana kupiga hatua mbele, na kusababisha mahitaji yao ya msingi kutotambuliwa kama ambavyo yanatambuliwa mahali pengine, Africa Mashariki 🐒

Ni muhimu zaidi kujifunza kujadiliana au kujibu hoja kwa hoja kiungwana, na sio kwa mihemko, matusi au kutukana.

Ni muhimu zaidi pia kujifunza kuwa wastahimilivu, kujizuia na hali hiyo ya fedheha inayoashiria ukomo wa fikra na kukata tamaa 🐒
 
Vijana wamepoteza dira.

Hawajui kesho yao.

Wamesoma hawana kazi wala hawategemei kuajiriwa.

Watajiajiri na nini, wengi ni familia za uwezo wa kati na mdogo.

Wanaishia kunywa gongo,

Watakosaje mihemko?
 
Hahaa! Kiutafiti nilichofanya...mtu asie na pesa hua na hasira saana!😅😅....mihemuko itakuwepo tu mpaka watu wajipate.
 
Ni matunda ya shule za Kata
mmh gentleman,

binafsi nimesoma shule ya kata tena ni second selection candidate..

nakumbuka nilijiunga form one tar 13.7.2000s hadi Dec nimeshamaliza kidato, na January mwaka ulofuata nikaendelea na form Two kwa usongo mkubwa...

sikuwahi kufundishwa mihemko wala panic huko au ni shule za kata zipi 🐒
 
Vijana wamepoteza dira.

Hawajui kesho yao.

Wamesoma hawana kazi wala hawategemei kuajiriwa.

Watajiajiri na nini, wengi ni familia za uwezo wa kati na mdogo.

Wanaishia kunywa gongo,

Watakosaje mihemko?


Kuingia katika uraibu wa pombe na kuwa malaya ni ukosefu wa kujitambua maana MTU makini hawezi kuangukia huko .

Elimu ingeongezewa kitu cha kuwafanya vijana wajitambue na wawe na uwezo wa kuji-control

Kuna watu wametoka broke family na hawana Elimu kabisa Ila wamejitambua na wanaendesha maisha vizuri.


Kumtegemea mwanasiasa wa ccm au chadema kukubadilishia MAISHA ni kukubali kujipoteza.
 
Back
Top Bottom