Mihogo mibichi inayouzwa barabarani Mwenge hadi Africana ina sumu!

Mihogo mibichi inayouzwa barabarani Mwenge hadi Africana ina sumu!

Buyaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
1,705
Reaction score
1,953
CYANIDE iliyotumika na Adolf Hitler kuuwa Wayahudi ipo kwenye MIHOGO MIBICHI!

Na mpaka leo bado inatumika kwenye hukumu za vinyongo kwenye nchi kama Marekani jimbo la Arizona.

Sisi tukitaka kuua mtu tunampiga na mawe, petroli, viberiti... taharuki. Lakini njia moja ya kuua mtu bila kuzua taharuki ni kumpa CYANIDE.

Mihogo mibichi ni hatari. Chemsha, kaanga, pikia ugali, tengenezea pombe (fermantation degrades cyanides)

....do something!

Ukichemsha dakika 15 unaharibu enzyme ya linamarase ndani ya mihogo mibichi ambayo ndio inayo release hizo cyanides mwilini kama ukiila mibichi.

Tuache kutafuna mihogo mibichi.

LA MWISHO: Mtu asikudanganye kwamba maziwa ni dawa ya sumu. HAKUNA mahala popote duniani pameandikwa maziwa yana neutralize sumu mwilini. Tafuta, hutapata!
 
1658559482460.png
 
Mleta uzi ebu tueleze, Ni research gani iliyo fanyika na ika conclude kuwa content ya cyanide iliyopo kwenye mihogo imefikia leve ya ‘usumu’ wa kuweza kuathiri afya za walaji?. Ma babu zetu walikula sana mihogo na waliishi zaidi ya miaka 80!,
Siku nyingine muwe mnauliza kwanza kabla ya ku post craps
 
Kuwepo tu haimaanishi itadhuru

Hata mbegu za ma apple machungwa limao zinayo cyanide........ lakini sio kigezo Cha kututishia kuwa ni sumu. Dozi, Namna ya kuipewa inahusika sana
 
CYANIDE iliyotumika na Adolf Hitler kuuwa Wayahudi ipo kwenye MIHOGO MIBICHI!

Na mpaka leo bado inatumika kwenye hukumu za vinyongo kwenye nchi kama Marekani jimbo la Arizona.

Sisi tukitaka kuua mtu tunampiga na mawe, petroli, viberiti... taharuki. Lakini njia moja ya kuua mtu bila kuzua taharuki ni kumpa CYANIDE.

Mihogo mibichi ni hatari. Chemsha, kaanga, pikia ugali, tengenezea pombe (fermantation degrades cyanides)

....do something!

Ukichemsha dakika 15 unaharibu enzyme ya linamarase ndani ya mihogo mibichi ambayo ndio inayo release hizo cyanides mwilini kama ukiila mibichi.

Tuache kutafuna mihogo mibichi.

LA MWISHO: Mtu asikudanganye kwamba maziwa ni dawa ya sumu. HAKUNA mahala popote duniani pameandikwa maziwa yana neutralize sumu mwilini. Tafuta, hutapata!
...Watafuna Mihogo mibichi Wameisha kufa Kwa Cyanide Yako? Hivi Cyanide unaijua kweli ama Unaisikia TU?
 
Ndugu bandiko lako ni la maana na ni la kimantiki ingefaa uliongezee maelezo ya kitaalamu ili wadau tupate elimu....
 
Chizi hili,babu yangu anamiaka 96 tokea mdogo anatafuna hiyo mihogo mpaka wa leo anapumua na hana tatizo la afya
 
kijijini tumekula sana mihogo mibichi wakati tunasubiri ugali uive, tulipoza njaa kwa mihogo.....sasa wewe umemaliza chuo juzi tu jamani ndio unatuambia tusile mihogo?
 
Back
Top Bottom