Kimsingi ni kweli soko la Muhogo ni kubwa sana japo kunachangamoto kiasi hasa soko likiwa linahitaji muhogo mkavu(UNGA,CHIPS,Starch) kwa kiwango kikubwa sana, kiasi kwamba wazalishaji wengi bado hajafikia hapo.
kwa mahitaji yako nafikiri kama unauwezo badili huo muhogo mbichi uwe mkavu (unga au chips ), ilikukusaidia kupata soko rahisi zaidi, na kama utapenda kuuza mbichi wapo wanunuzi kwenye masoko Ya tandale na Temeke sterior japo bei zao zinafuatana na size ya Muhogo,aina ya muhogo, kipindi cha uvunaji na Umri wa muhogo.
Na kama upo Pwani, tembelea Mkuranga kwa habari zaidi.