Katika kuthibitisha kuwa wanadamu wameendelea kuwa na kila mbinu chafu ya kuiba haki, Kijana mmoja alipita akiwa na mfuko wenye chakula na kujaribu kuingia nao katika mojawapo ya ukumbi wa majimbo yanayongojea kutangazwa matokeo yake huko Dar.
Wananchi waliokuwepo nje wakiamua kumepkua na kukuta amebeba chakula.
Hata hivyo wananchi hawa hawakuridhika, waliendelea kumpekua na zaidi na kukuta chini ya kile chakula kulikuwemo na fomu zilizo na matokeo ya kura za wagombea.
Hii ilikuwa ni majira ya usiku. Alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi.
Huko nyuma alikuwa amekamatwa kijana mwingine aliyekuwa ameingia akiwa na alichodai kuwa ni mihogo na alikuwa akiipeleka kwa waliokuwa ndani ya ukumbi wa kuhesabia kura. Walipopekua walimkuta akiwa na mihuri ya tume ya uchaguzi.
Source ITV. Usiku Nov 2.