Miiko na Maadili ya Mtanzania

Miiko na Maadili ya Mtanzania

Mkandara

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,806
Reaction score
9,011
Nimesoma pahala maneno mazito ya kufikirisha, yakisema hivi:

"Utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili ni sawa na nyumba isokuwa na mume" Je, unakubaliana na maneno haya? Tujadili...
 
Hapa ndio nyumbani Kwa usalama wa taifa wanalinda MAADILI kulinda taifa ndio maana Jinga la chatorindabad waliliondoa kule India kulilinda taifa la Tasmania!
 
Je, kuna sheria zozote zilizoainishwa za maadili hayo? Miiko hiyo?

Wapi huko?

Chaka kubwa kweli! Itabidi utufyekee fyekeee mkuuu, tulishe tu hayo majani bila magugu!🧐

🤔
 
Ngoja kwanza,
Unataka kuwasema singo mazas au unataka kuisema serikali ya Dakta Samia?

Tujue tunaenda endaje hapa
 
Simsemi mtu yeyote ila nimenukuu usemi huo. Je, una Uhalisia katika Utawala na maisha ya unyumba? Iwe singo mazas, Je, kuna kweli nyumba asokuwa na mume huondokewa miiko na maadili? Nadhani hoja hapa ni watoto! Tujadili sote..

Kiutawala binafsi naafiki hoja na kwamba Katiba inayokosa Miiko na Maadili hujenga sheria mbovu na chanzo cha Ufisadi (Uharibifu) nikujibu swali lako, Katiba haikuandikwa na Mama Samia..
 
Nimesoma pahala maneno mazito ya kufikirisha, yakisema hivi: - "Utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili ni sawa na nyumba isokuwa na mume" Je, unakubaliana na maneno haya? Tujadili...
Hatuwezi kulijadili hili swala linahusu Shule ya Uongozi. Umtafute Polepole awepo ndiye atatanzua hili kwani ndiye mtaalamu. Japokuwa walimbeza sana Sasa tunarudi kulekule.! TanzaGiza!!
 
Nimesoma pahala maneno mazito ya kufikirisha, yakisema hivi: - "Utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili ni sawa na nyumba isokuwa na mume" Je, unakubaliana na maneno haya? Tujadili...
Maoni ya msemo huo ni "mfumo Dume", ambao baadhi ya watu wa leo duniani hawauamini.

Kuna "nyumba zilizo na waume", lakini hazina maadili; baba mlevi kupindukia, na mama naye anafanya yake kivyake , na watoto hali kadhalika.

Huu "utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili", unawezekana huo? "Miiko" ni nini? na " Maadili" maana yake ni nini?

Utawala ukose kuwa na "Miiko" yote, au baadhi ya miiko? Ni hivyo hivyo na "Maadili", labda iwe ni baadhi ya maadili, haiwezi kuwa maadili yote. Huo hautakuwa "utawala", itakuwa ni vurugu.
 
Maoni ya msemo huo ni "mfumo Dume", ambao baadhi ya watu wa leo duniani hawauamini.

Kuna "nyumba zilizo na waume", lakini hazina maadili; baba mlevi kupindukia, na mama naye anafanya yake kivyake , na watoto hali kadhalika...
Nakubaliana na wewe.

Huu msemo unatukuza mfumo dume na hivyo unapoteza mantiki.

Kwani nyumba zote zilizo na waume zina maadili na nyumba zote zisizo na waume hazina maadili? I dout it big time!
 
Hata kama mume aweza kuwa ni mlevi, nyumba yaweza kuwa na nidhamu kuliko nyumba isiyo kuwa na mume kabisa
 
Nimesoma pahala maneno mazito ya kufikirisha, yakisema hivi: - "Utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili ni sawa na nyumba isokuwa na mume" Je, unakubaliana na maneno haya? Tujadili...
Mkuu kwa 100% nakubaliana nawe.

Ukiangalia awamu ya 5 utawala haukuwa na miiko hata kdg, miiko iliyokuwa ikifuatwa na ya mtu mmoja! na MAtokeo yake tuliona, nchi ilikuwa ktk kipindi kgumu mno !
 
Je, kuna sheria zozote zilizoainishwa za maadili hayo? Miiko hiyo...
Miiko na maadili hukaa kwenye matendo na vichwa vya watu , sheria maudhui ndani yake imebeba miiko na maadili.

Kimsingi huhitaji kulist miiko na maadili maana hukaa katika vichwa vya watu.
 
Nimesoma pahala maneno mazito ya kufikirisha, yakisema hivi: - "Utawala usiokuwa na Miiko wala Maadili ni sawa na nyumba isokuwa na mume" Je, unakubaliana na maneno haya? Tujadili...
Swali zuri. Miiko ni mambo ambayo yasipozingatiwa yataathili ukoo, kizazi au jamii husika. Maadili ni mambo mema ya heri katika jamii yanayotakiwa kukuzwa.

Miiko na maadili ni maswala yanayohusu muktadha au mazingira ya jamii husika. Katiba na sheria husimamia taratibu zinazolinda mahusiano katika nchi.

Katiba na sheria ni za kitaasisi lakini miiko na maadili yanatokana na mapokeo, mazoea na uelewa wa jamii husika.

Kwa mfano mwiko wa kula nyama mbichi au maadili ya kuto oa mwanamke ambaye kwa umri wake angeweza kuwa binti yako ni mifano ya mwiko na maadili, kwa mfuatano, ambayo kukubalika kwake inategemea muktadha unaohusu jamii au kipindi gani katika historia; na si katiba wala sheria.
 
Miiko na maadili hukaa kwenye matendo na vichwa vya watu , sheria maudhui ndani yake imebeba miiko na maadili.

Kimsingi huhitaji kulist miiko na maadili maana hukaa katika vichwa vya watu.
Kwa maana hiyo, kila mtu anaweza kuwa na "miiko na maadili" yake, tofauti na wengine au siyo?
 
Maadili ya kitaifa au ya Mtanzania ni porojo tu za wanasiasa na minions wao
 
Swali zuri. Miiko ni mambo ambayo yasipozingatiwa yataathili ukoo, kizazi au jamii husika. Maadili ni mambo mema ya heri katika jamii yanayotakiwa kukuzwa.

Miiko na maadili ni maswala yanayohusu muktadha au mazingira ya jamii husika. Katiba na sheria husimamia taratibu zinazolinda mahusiano katika nchi.

Katiba na sheria ni za kitaasisi lakini miiko na maadili yanatokana na mapokeo, mazoea na uelewa wa jamii husika.

Kwa mfano mwiko wa kula nyama mbichi au maadili ya kuto oa mwanamke ambaye kwa umri wake angeweza kuwa binti yako ni mifano ya mwiko na maadili, kwa mfuatano, ambayo kukubalika kwake inategemea muktadha unaohusu jamii au kipindi gani katika historia; na si katiba wala sheria.
Kwa kawaida uwepo wa Miiko na Maadili ni kuhifadhi Tamaduni, mila na desturi za jamii na umuhimu wake katika Katiba na sheria ni kulinda UTU wa Jamii husika.

Ndio maana hata Siasa zilipotungwa zilikidhi kwanza Uhafidhina (conservative) kulinda jamii hiyo Kitaifa. Na hata ulipokuja Uliberali (Liberal) ulilenga kupingana na baadhi ya miiko na Maadili Kisheria kabla kabisa ya maswala ya mrengo wa Kiuchumi kuwa sehemu ya Siasa.

Kwa hiyo Umuhimu wa Miiko na Maadili katika Taifa unaenda sambamba na Utunzi wa sheria za nchi laa sivyo mtapokea mila na tamaduni kinzani kabisa na UTU wenu.
 
Nakubaliana na wewe.

Huu msemo unatukuza mfumo dume na hivyo unapoteza mantiki.

Kwani nyumba zote zilizo na waume zina maadili na nyumba zote zisizo na waume hazina maadili? I dout it big time!
Hata Utawala wanasema ni mfumo Dume. Je, mfumo Jike ukoje? Hivi kuna kosa gani kuwepo mfumo dume ikiwa pasipo mbegu hutapata mavuno.

Majuzi tu nilikuwa nazungumza na binti mmoja akisema "Hakuna kama Mama" (Siku ya wanawake Duniani) Je, huo ni mfuko jike? Je kuna ukweli wowote kuwa Mama ni mbora kuliko Baba? Na katika vitu gani, uja uzito au malezi? Je Kwa nini hakuna msemo Hakuna kama Baba? Alishindwa kunijibu maana Anajua Babake alisha fariki.
 
Simsemi mtu yeyote ila nimenukuu usemi huo. Je, una Uhalisia katika Utawala na maisha ya unyumba? Iwe singo mazas, Je, kuna kweli nyumba asokuwa na mume huondokewa miiko na maadili? Nadhani hoja hapa ni watoto! Tujadili sote..

Kiutawala binafsi naafiki hoja na kwamba Katiba inayokosa Miiko na Maadili hujenga sheria mbovu na chanzo cha Ufisadi (Uharibifu) nikujibu swali lako, Katiba haikuandikwa na Mama Samia..
Mkandara wewe kama ni second generation basi Tambua wewe ni tokeo la huo ufisadi, kiasi unakosa Authority ya kuukosoa au kuzungumza vibaya kama Ambavyo muandishi alipotray kwenye kitabu "The Beautyful Ones Are Not Yet Born" Ayi Kwei Armah credit kwake
 
Daaah ,sasa First generation ndio kina nani? Adam na Hawa au?!!
 
Back
Top Bottom