Miili yenye afya kwenye jamii za wafugaji

Miili yenye afya kwenye jamii za wafugaji

Huwezi kubishana na takwimu boss anayekula protein ya nyama maziwa mara nyingi anakuwa mbavu
Unaweza kuwa mbavu ila ufupi na urefu ni issues za vina saba , kuna jamii za watu wadogo lakini ni mbavu kwa sababu ya lishe.
 
Wachaga wa upande wa magharibi ( wamachame ) ni wakubwa kuliko hata watu wakanda ya ziwa , na kuliko hata wenzao wa mashariki hii sio kwa sababu ya lishe ,hili ni swala la vina saba tu.
Mbona kule machame ni wanywaji wa maziwa sanaaana vyakula Kama vya wafugaji tu japo ni wakulima.Tena nyumba nyingi za watu wahuko wana mifungo nyumbani.
 
Wajapan/wachina ni wafupi lakini ndio watu wenye akili pengine kuliko watu wote duniani na ndio mataifa yenye watu kuishi miaka 100+ sio issue....Tafakari. Urefu na ufupi ni vinasaba tu na kuishi muda mrefu inategemea na chakula unachokula.
 
Ufupi si tatizo, ufupi inaweza kuwa ni muendelezo wa vinasaba (genetic). Tatizo ni huo ufupi unaotokana na kudumaa! Kuna mkoa mmoja ni moja ya mikoa vinara (big five) wanaozalisha mazao mengi kiasi cha kutegemewa na nchi yetu, lakini ajabu ni kuwa ndio mkoa unaoongoza kwa watu (watoto) kudumaa.

Sasa najiuliza, ina maana haya mazao wanayolima wanapeleka wapi?! Wengine watasema: wanadumaa kwa kuwa hawana mifugo kama Wasukuma, Wamasai, Wasandawe, nk. Hii sio kweli, kwani protein inapatikana pia katika baadhi ya mazao! Mazao kama maharage (sio mkurugenzi mtendaji wa Tanesco), choroko, mbaazi, dengu, njegere, nk; haya ni mazao yenye protein nyingi tu, pengine kukaribiana au sawa na nyama!

Sasa ndugu zetu nyie Wahehe, kwanini mnadumaa kwa kukosa lishe ilhali nyie ndie mnaozalisha mazao kupita mikoa mingine hapa nchini? Au mazao yote mnauza bila kubakiza akiba ya chakula na hivyo kula vyakula duni kama mafyulisi na ulanzi? Acheni tabia hiyo mara moja.

Nyie mliaminiwa sana enzi za Mwalimu nyerere, kiasi cha kuwaweka idara nyeti! Hii ilitokana na uwezo wenu kiakili na maadili, tunataka muendelee kuwa hivyo. Hivi mnajuwa mtoto akidumaa mwili na akili inadumaa?

Watu wengine wenye tabia mbaya ni baadhi ya makabila kutoka mkoa wa Tanga. Hawa sasa wanachofanya sio tu kuwasababishia udumavu watoto wao, bali pia ni kituko katika jamii! Eti jitu zima na midevu yake, lionamtoa mtoto kwenye ziwa la mamake (mama mwenye mtoto) halafu linanyonya lenyewe maziwa ya mtoto! Hivi nyie hamna huruma kwa watoto wenu kweli?! Wewe si ulinyonya kwenye kipindi cha utoto wako?! Babako angekudhurumu maziwa ya mamako si ungekufa au ungedumaa?

Wewe ni mtu mzima, una meno, unaweza kula, mtoto anategemea maziwa tu ya mama yake. Sasa wewe unakula chakula (ugali, nyama, nk), ukimaliza unaenda kunyonya na maziwa ya mtoto, huyo mtoto atakuwa na afya kweli?! Waachieni watoto maziwa ya mama zao, wanyonye, wakue na kuimarika kiafya. Na bahati nzuri waziri wa afya anatoka huko, hivyo msimuangushe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa unamaanisha urefu ni kutokana na aina ya chakula na ufupi ni kutokana na aina ya chakula?? INACHEKESHA EEEEEEEH KUFIKIRI HIVO,ni Sawa na wale wanaokuambia wanaukula samaki Kwa wingi wanakua na akili Sana
 
Habari zenu watu wa humu.
Moja kwa moja niende kwenye mada nisiwachoshe na salaam. Katika pitapita zangu na kuzunguka baadhi ya mikoa hapa Tanzania, nimegundua jamii za wafugaji Kama wamasai, wakurya, wasandawe, wasukuma nk.., wana asili ya urefu tena wana afya Sanaa tofauti na jamii za wakulima ni wafupi asilimia kubwa Kama waha, walugulu, wapogoro nk..

Swali langu ni je? Hizi jamii za wafugaji wanapata lishe nzuri tofauti na hawa wakulima? Au hii inatokana na nini wakati na wao wanalima wanapata mazao(mlo kamili).
Udumavu wa lishe kutokana na kukosa maziwa. Mikoa inayoongoza Iringa, Njombe, Rukwa.
 
Mwenzio kaongelea jamii ya wakulima ndiyo wanakufa sana.Tangu lini mtu anakula protein kwa wingi akawa na afya dhaifu na akadumaa?
ufupi sio kudumaa wala ulefu aletwi na maziwa na nyama
 
Habari zenu watu wa humu.
Moja kwa moja niende kwenye mada nisiwachoshe na salaam. Katika pitapita zangu na kuzunguka baadhi ya mikoa hapa Tanzania, nimegundua jamii za wafugaji Kama wamasai, wakurya, wasandawe, wasukuma nk.., wana asili ya urefu tena wana afya Sanaa tofauti na jamii za wakulima ni wafupi asilimia kubwa Kama waha, walugulu, wapogoro nk..

Swali langu ni je? Hizi jamii za wafugaji wanapata lishe nzuri tofauti na hawa wakulima? Au hii inatokana na nini wakati na wao wanalima wanapata mazao(mlo kamili).
Hujazunguka vya kutosha ukaelewa,wasukuma ni wakulima zaidi kuliko kufuga
 
Sasa unamaanisha urefu ni kutokana na aina ya chakula na ufupi ni kutokana na aina ya chakula?? INACHEKESHA EEEEEEEH KUFIKIRI HIVO,ni Sawa na wale wanaokuambia wanaukula samaki Kwa wingi wanakua na akili Sana
Kama umesoma na kuelewa nilichoandika usingesema hivyo; kuna habari ya vinasaba na chakula. Kama mtu alirithi vinasaba vya babu yake, ambaye alikuwa mfupi, lakini anakula chakula bora, huyu hatadumaa ila atakuwa mfupi. Kwa upande mwingine, ikitokea mtu karithi vinasaba vya babu yake ambaye alikuwa mrefu, lakini anakosa chakula bora, huyu atadumaa na hivyo hawezi kuwa mrefu japo alirithi vinasaba vya babu yake ambaye ni mrefu. Binadamu tunafanana na mimea katika makuzi; angalia mazao yako shambani, ambayo yameota sehemu isiyokuwa na rutuba, linganisha na yale yaliyoota mahali penye rutuba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wenye afya ni upi kwanza?, Mara mbavu sijui urefu duuuh.
 
Wanakunywa maziwa sana. Pia nimeishi katika moja ya jamii moja ya wafugaji nikapata wasaa wa kuzungumzia masuala ya kimapenzi na mwanamke wa jamii ya wafugaji. Alinidokeza kwamba kama kuna mtu giant wamempenda wanandoa wanakubaliana waipate mbegu hiyo iwepo kwenye familia yao. Mwanandoa wa kike atachepuka kumpata huyo mtu giant, watachakatana mpaka anase mimba. Hiyo mimba zao lake ni mali ya familia yao. Huyo mama anasema ni utamaduni wao na hakuna wivu kwa mume wake
 
nikiwa ndani ya daladala ukazuka mjadala wa wanawake wenye ndoa kuchepuka nje wanatafuta nini? Mchangiaji mmoja alijibu kuwa huwa wanatafuta uzao tofauti na uliopo, kwani uliopo unaweza kuwa dunya wakati uzao wa mchepuko unaweza kuwa na akili tofauti na bora. Yaani kama watoto wa ndani hawana akili nzuri zinafanana na za baba yao, wanatafuta watoto nje wenye akili zaidi kwa baba mwingine mwenye akili nyingi. Kwa hiyo tayari mama atakuwa na watoto wenye akili tofauti za baba zao
 
Habari zenu watu wa humu.
Moja kwa moja niende kwenye mada nisiwachoshe na salaam. Katika pitapita zangu na kuzunguka baadhi ya mikoa hapa Tanzania, nimegundua jamii za wafugaji Kama wamasai, wakurya, wasandawe, wasukuma nk.., wana asili ya urefu tena wana afya Sanaa tofauti na jamii za wakulima ni wafupi asilimia kubwa Kama waha, walugulu, wapogoro nk..

Swali langu ni je? Hizi jamii za wafugaji wanapata lishe nzuri tofauti na hawa wakulima? Au hii inatokana na nini wakati na wao wanalima wanapata mazao(mlo kamili).
Utafiti wako ni Uongo.Mbeya na Iringa na Ruvuma na Wazaramo siyo Wafugaji na hawana maumbo madogo.

Kumbuka pia Magufuli ni msukuma, Mbunge Msukuma ni Msukuma,
 
Sijawahi ona utafiti wa kipuuzi kama huu, haya tuelezee na wazungu inakuwaje.?? maana huko hamna wafugaji wala wakulima na wengi ni warefu na haswa Waholanzi ndio wazungu warefu ukikuta mfupi ni 5'9.
 
🙏🙏 Umeeleza vizuri Sanaa.Kuna mmoja japo amefuta comment yake et alisema wafugaji wanakuwa warefu kwasabab wanasimama mda mrefu,wanatembea kuchunga mifugo mda mrefu afu wakulima wengi wanakuwa wafupi kwasababu wanalima wameinama 😆😆😆😂😂😂🤣🤣🤣🙌🙌
double click
 
Back
Top Bottom