Mijadala ya mabaraza ya rasimu ya katiba vituko - Bukoba

Mijadala ya mabaraza ya rasimu ya katiba vituko - Bukoba

Mudhakiru

Senior Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
175
Reaction score
29
Leo ikiwa ni siku ambayo mchakato wa mabaraza ya kujadili Rasimu ya Katiba mpya unaendelea nchini, leo ni zamu ya Manispaa ya Bukoba ambapo kituo ni Rugambwa Sekondari.

Chakushangaza ni hali ya sehemu kubwa ya wajumbe waliochaguliwaa kama wajumbe wa Baraza kuonekana ni watu wenye uwezo mdogo wa kuisoma rasimu na kuichambua.

Pamoja na wajumbe wengi kuwa ni Madiwani wa CCM na wafurukutwa wengine wa CCM kikubwa zaidi kuwa ukiachana na hao Madiwani waliobaki ni vijana na mabinti wa mtaani ambao walichaguliwa kimizengwe na kuwaacha wasomi wengine wakiwemo hata walimu.

Ukizingatia kuwa zaidi ya walimu Watatu wa shule hii waligombea na kupitishwa katika mtaa na Kata lakini wakaondolewa kimizengwe Wilayani.

Hii inaonesha kuwa jambo hili lilipangwa ili kuweka watu watakao kuja kusoma waraka wa CCM kama mapendekezo yao katika katiba.

KWA HILI HAKUNA KATIBA MPYA BALI KATIBA YA CCM
 
Hilo lishasemwa sana na wabunge wa CDM bungeni ila walionekana wanafiki, sasa tunaenda kuizika Tz yetu iliyokwisha kuuwawa na ccm
 
......."wasomi wengine hata walimu"..... Kama ndio Notion ya wengi iko hivyo, basi walimu wansafari ndeeeefu.
 
Ndugu yangu hapo hakuna mabaraza kuna mawazo ya kagasheki na Amani.
Juzi huko Zanzibar wajumbe wa CCM wanasoma maoni kwenye kabrasha rasmi, ilionekena mjumbe wa Kamati ta Katiba kukerwa akawaambia wanataka maoni wala siyo maneno kwenye makabrasha toka kwenye VYAMA. Jaji Warioba na wajumbe wake walileta maoni ya watu tofauti na mabaraza yanapeleka maoni ya vyama. Bora tuendelee na Rasimu hiyo kwa mabadiliko kidogo tu.
 
Leo ikiwa ni siku ambayo mchakato wa mabaraza ya kujadili Rasimu ya Katiba mpya unaendelea nchini, leo ni zamu ya Manispaa ya Bukoba ambapo kituo ni Rugambwa Sekondari. Chakushangaza ni hali ya sehemu kubwa ya wajumbe waliochaguliwaa kama wajumbe wa Baraza kuonekana ni watu wenye uwezo mdogo wa kuisoma rasimu na kuichambua. Pamoja na wajumbe wengi kuwa ni Madiwani wa CCM na wafurukutwa wengine wa CCM kikubwa zaidi kuwa ukiachana na hao Madiwani waliobaki ni vijana na mabinti wa mtaani ambao walichaguliwa kimizengwe na kuwaacha wasomi wengine wakiwemo hata walimu. Ukizingatia kuwa zaidi ya walimu Watatu wa shule hii waligombea na kupitishwa katika mtaa na Kata lakini wakaondolewa kimizengwe Wilayani. Hii inaonesha kuwa jambo hili lilipangwa ili kuweka watu watakao kuja kusoma waraka wa CCM kama mapendekezo yao katika katiba. KWA HILI HAKUNA KATIBA MPYA BALI KATIBA YA CCM
acha kupotosha watu mabaraza hayahitaji watu wenye digrii kinachotakiwa ni kusema nini wanakitaka kiwemo kwenye katiba.
 
Mudhakiru watawala, si viongozi, CCM ni wakoloni weusi. Wamerithi katiba ya Muingereza. Hawataki kabisa mabadiliko. Hata bunge letu ni la muundo wa Westminster.

Kweli. Wanataka katiba yao. Si ya wananchi. Tuko kubaya. Jehanam yanukia.

Watafanya chochote kubaki madarakani. Wamesahau ni nani aliyewapa dhamana hiyo kwani cheo ni dhamana.

2015 haiko mbali. Kadri watakavyotubana kwa katiba yao mbovu, Mungu ndivyo atakavyozidi kuwaumbua!
 
Last edited by a moderator:
Vioja vya masisiem ni vingi walichakachua katika hatua ya kwanza ili kulinda maslahi yao na sasa wanatekeleza hilo, kwao maslahi ya nchi na watanzania sio muhimu muhimu kwao ni nambari one. MAJANGA MAJANGA MAJANGA
 
Back
Top Bottom