county _adjustment _tz
New Member
- May 21, 2024
- 3
- 1
MIKAKATI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA MWAKA 2025
USIMAMIZI WA RASILIMALI ( rasilimali watu, rasilimali fedha na maliasili zetu ) NA UADILIFU .
Swala la rasilimali watu, kwa sasa Tanzania haina uhaba sana wa wafanyakazi katika maeneo mbali mbali ukilinganisha na mika ya 1990s hivyo nguvu kazi tunayo , tunao wapa watu kusimamia miradi yetu , tassisi zetu pamoja na halimashauri zetu hawapasi tena kufichwa na kuamishwa vituo vya kazi kwa sababu ya kuto kuwa waadilifu pale tulipo wa kasimisha au kuwapa kazi kwa niaba ya nchi yetu swala la kufanya kazi ndani ya umma ionekane kama swala la kinidhamu na mfano wa kuingwa ukiangalia mashirika binafsi wanavyo fanya kazi kwa kujituma na kwa si ili kulinda kula yao lakini ukija kwa huu upande wtu wa serekalini tumejiona kama ni shamba la bibi watu hawawajibiki na kuoneana haya , mfano ni mashirika ya umma kufa sababu tu ya watu tulio waamini na kuwapa kuya endesha bila kujali yamekufa .
Suala la rasilimali Asilia , Angalia watu wanao zunguka migodi mbali mbali , gesi asilia , maliasili za utali na mapori yetu tengefu bado haya leti tija ya moja kwa moja kwa mwanchi hususa ni wale walio karibu nao bado pia serikali haipati kile kilicho sawa kutoka kwenye rasilimalii hizi sababu ya kutokuwa wadilifu katika maeneo ya usimamizo .
Suala la rasilimali fedha za umma , hapa ndipo sehemu nyingine inatuchelewesha kufika tunapo pataka kwa sababu hatuna usimazi mzury hasa hizi halimashauri zetu na taasisi zake ndani ya mkoa na wilaya , makusanyo ya kodi tunazo pata kutoka vyanzo mbali mbali hatuna mikakati mizuri ya kuzisimamia na kuziendeleza kwa kuleta tija ya maendeleo ya mwanchi na taifa kwa ujumla . kuwa na sharia ya fedha za umma inayo weka kanuni zake bayana yaani ( PUBLIC FINANCE MANAGEMENT ACT ) hii italeta uwadilifu na kulinda vyema kazi za umma na mapato yake kutumika palipo kusudiwa na umma kwa maendeleo
Uadilifu , hii huanzia moyoni kwa mtu mwenye kujali na kupenda kulinda na kusimamia mali za umma kwa msilai ya umma , kushindwa kupata watu wa namna hii au kutokuwa na kanuni na njia nzury ya kulinda uwadilifu kuta tudhoofisha na kutuacha bila maendeleo yetu .
Rushwa na sheria kwa ujumla, Rushwa imekemewa toka enzi za awamu ya kwanza hadi sasa lakini imekuwa ndiyo kama silaha kwa kutokomeza ndoto za walio wengi katika maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla hususa ni wanawake ndiyo jinsi inayo athikika sana kulinganisha na jinsi ya kiume katika elimu , kazi, sehemu za kutolea haki , utu wao na kadhalika ni maeneo ambayo wanawake wngi wameshindwa kupata usawaa na haki yao sababu ya ukandamizaji kwa njia ya rushwa , Hata hivyo bado hatuna sheria nzury sana na pengine zimesha piatwa na wakati katika kutoa haki na kuisima mimia iyo haki kujiletea maendeleo katika jamii na nchi kwa ujumla
TEKINOLOJIA NA UTAFITI , Dunia ya sasa na kwa maendeleo endelevu kuna haja pia ya kuweka nguvu ya pamoja katika maswala ya tekinolojia pamoja na utafiti maeneo haya yatachangia kwa haraka sana ukuwaji wanchi na watu , tuweke asilimia 2- 5% kutoka kwa bajeti kuu ya serikali ili kukuza maendeleo ya tekinologia kwa kiasi chake , kama tukiweka juhudi katika eneo hili kwa ujumla ni rahisi sana kuongeza na kupunguza gape la ajira katika nyanja mbali mbali katika mnyoro wa uchumi na biashara kwa ujumla wake tuna weza kutumia pia rasilimali zetu kikamilifu kuleta maendeleo
Siasa safi na viongozi bora, kuwa na vyam aambavyo vitafanya siasa za kiustarabu na kwa mujibu wa kufwata na kuti sharia na miiko yake kutaleta Zaidi utulivu wa nchi na ustawi wa maendeleo kila chama cha siasa kiwe na ustarabu ambao hauta chochea uasama na hila miongoni mwa wanachama hata hivyo kuleta viongozi wasafi nawajibikaji ndani na nje kwa masilahi ya umaa na situ maslai yao binafsi kama ambavyo wachache hufanya kwa sasa.
HITIMISHO; katika robo ya pili ya karine 21 na ambapo pia itakuwa nusu ya kwanza ya karne natamani Tanzania iache kufanya vitu kwa mtazamo wa kujiona nchi ndogo na kadhalika , ila ijikite zaidi katika TEKNOLOJIA NA UTAFITI , USIMAMIAJI WA RASILIMALI ZETU NA UWADILIFU , KUPINGA RUSHWA NA KUWA SHERIA STAHIKI SAHIHI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU SIASA SAFI NA VIONGOZI BORA MIAKA 25 IJAYO
Upvote
4