Pre GE2025 Mikakati ya vyama vya siasa katika kuongeza Uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi

Pre GE2025 Mikakati ya vyama vya siasa katika kuongeza Uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Oct 8, 2024
Posts
8
Reaction score
5
Na Thuwaiba Habibu, Zanzibar.

"Wanawake wamekuwa wakilalamika wakichukua fomu wanaanza kufatwa kwamba wao' si mna viti vyenu Maalumu ' tuachieni sisi huko ( jimbo), ndio maana tuna sema kuna ubinafsi kwenye vyama vya siasa.

Ni maneno ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la wanawake katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (Wildaf) Anna kulaya akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya democrasia yaliyofanyika 20 september 2024.

Kauli hii inaonesha kuwa wanawake wanakabiliwa na changamoto kubwa kutoka katika vyama vya siasa na ipi mikakati yao kwa vyama hivyo kuhakikisha uwakilishi wa wanawake unaongezeka katika siasa.

Msemaji wa masuala ya afya wa chama cha Act Wazalendo Nassra Nassor Omar Amesema mipango mikakati ya chama hicho tumewezesha kuanzisha ngome ya wanawake,vijana ambao wanauwezo wa kugombea uongozi na wapo tayari kulifikia hili ili kuhakikisha tunaongeza uwakilishi kwenye vyombo mbali mbali vya maamuzi.

Kuna program ambazo zimeandaliwa na nyengine zishazinduliwa zinazomkuza mtoto wa kike katika uongozi mfano program ya Binti mzalendo ambayo humuwezesha mtoto wa kike kuingia katika uongozi na kuwa kiongozi bora na wamfano.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Kwani tunaamini ukimsaidia mwanamke mmoja ushasaidia taifa zima na maendeleo yatapatikana kupitia mwanamke huyo"

Uwepo wa viongozi wanaotaka mabadiliko na sera yetu ya jinsi imekuja kuondoa hofu kwa watoto wa kike na wanawake kuingia kwenye chaguzi kwa nafasi mbali mbali za uongozi.

"Hii imepekea ndani ya chama chetu kupewa nafasi za Uongozi wanawake kuonekana kama ni utamaduni"

Mueka Hazina Kanda ya Unguja Chama Cha Chadema na Mwenyekiti wa Wanawake jimbo la kikwajuni (BAWACHA). Asiata Said Abuubakar amesema kwa kuwa baadhi wanaume ndio kikwazo kikubwa kwa wanawake kuwazuiya kuingia katika uongozi Chama chetu hutoa mafunzo sana kwao watoe uhuru huo na kuondokana na dhana potofu.

"Sisi tumeamua kukaa na wanaume kuwapa nasaha kuhusu wake zao ushiriki katika uongozi kwani baadhi yao ndio kikwazo"

Kutokana na Wanzanzibari mila na desturi zetu zinazonesha kuwa mwanamke hawezi kushiki nafasi za uongozi kwa kusimama mbele za watu kuhubiri tunazidi kulisemezea na sasa kuna mifano ya viongozi wanawake wanaofanya hivyo linaonekana kueleweka kwa wanaume maana wanawake idadi inaongezea tofauti na 2015.

"Tutahakikisha mila na desturi sio kikwazo tena kwa wanawake zanzibar kushiriki nafasi za uongozi "
Tanzania imeingia katika mikataba tofauti, matamko na itifaki yote ni kuhakikisha suala la uchumi na democrasia inakuwa
Kupitia tamko la jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC la mwaka 2005 na itifaki ya Maendeleo ya jinsia mwaka 2008 imetekeleza kuwango cha chini cha ushiriki wa wanawake asilimia 30% na baadae kuimarishwa hadi 50%.

Katibu mkuu UWT Chama Cha CCM Zanzibar Tunu Juma Kondo amesema tunahamadisha wananchi kugombea nafasi mbali mbali za chama kila baada ya mda tunapita matawini na majumbani kutoa hamasa hiyo.
Tunawapa mafunzo kwa kufanya semina maeneo tofauti kuelimisha jamii zinapokuja chaguzi kuingia katika siasa na tunatumia mitandao ya kijamii kuhakikisha walikosa mafunzo anapata elimu kupitia huko kwani wengi hutumia mitandao hiyo na ujumbe unafika kwasababu asilimia ya wanawake kushiriki Uongozi kila siku unaongezaka na kwa 2025 tunatarajia itakuwa kubwa zaidi.

"Hatutaki kumuacha mwanamke hata mmoja kukosa fursa ya kugombea nafasi za uongozi katika mwaka huu wa Uchaguzi"

Mafanikio yameanza kuonekana kutoka na elimu tunayotoa kwani wanawake wamekuwa wakigombea zikitokea nafasi watu 50 hadi 20 hakuna inayogombewa na watu 3 dalili hiyo inatupa tumaini la kufikia 50 kwa 50 katika uongozi.

Soma Pia kwa taarifa zaidi zinazowahusu wanawake kipindi hichi cha uchaguzi: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?

"Sasa wanawake wanaulewa, hawana hofu na wamekuwa washajihishaji wakubwa wa wenzao kuingia katika nafasi za uongozi kuliko miaka ya nyuma."

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Ada Tadea Ali Makame Issa amesema chama chao wameeka usawa kwa jamii na usawa hauwezi kukamilika kama utamtenga mwanamke tunahamasisha wadau kuwapa nafasi wanawake kwa kuwasaidia sehemu inayohitajika msaada na kuwawezesha ili wasionekane dhaifu .

"Wadau wetu waliwasaidia sana wanawake uchaguzi uliopita wengi waliweza kugombea na hata uchanguzi huu tayari washajipanga kwa ajili ya uchaguzi"

Nataka watu wafahamu thamani ya mwanamke sio katika uongozi tu lakini kwenye Maendeleo ya aina yoyote bila kuwepo mwanamke hakuna mafanikio

"Sasa ni wakati mzuri wa vyama kuwapa nafasi nyingi za Uongozi ili kuweza kusaidia taifa letu"

Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915 ,492 huku wanawake ni 974 ,281 hii ikimanisha wanawake ni wengi.

Kwa wingi huu ipo haja ya wanawake kupewa fursa sawa na wanaume ili kupata watetezi wa kike katika ngazi za maamuzi na kuwasilisha changamoto zao

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania upande wa Zanzibar, Dk Mzuri Issa Ali, alisema umefika wakati kuondoa vikwazo vyote vinavyo kwamisha usawa wenye hadhi sawa kwa wanawake ili kwenda sambamba na mikataba hiyo.

Aidha aliomba viongozi wa vyama vya siasa kuweka sheria rafiki zitakazo toa muongozo wa bayana wa nafasi za uongozi sio kuwapa nafasi za uteuzi ambapo zinakuwa kama zawadi.

"Bado vyama vya siasa havijazingatia usawa kwa wanawake katika nafasi, kuanzia kwenye sheria, uchaguzi wa ndani ya vyama, na hata nafasi za majimboni, pia kuacha kuwabeza, badala yake kupokelewa vizuri sio kwa uadui"

Afisa sheria muandamizi wa vyama vya siasa Abdul- razak Said Ali amesema kuwepo kwa asilimia 50 baina ya wanawake na wanaume ni harakati za muda mrefu na sasa zinaendelea ili kuwepo kwa uwino sawa.

Harakati za wanawake kushiriki katika siasa na Uongozi ni suala linalofanyiwa kazi na serikali na taasisi zake ndani na nje ya nchi kwa kueka makongamano na semina za mara kwa mara kumuwezesha mwanamke kushika nafasi za Uongozi

Katiba ya Zanzibar ya 1984, imeweka wazi kuwa kila Mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu na yanayohusu taifa lake na katika marekebisho ya 2010 imeeleza kutakuwa na wajumbe BLW kwa idadi ya asilimia 40 wa wajumbe kwa kila jinsia.

IMG-20250124-WA0003.jpg
___.jpg
 
Back
Top Bottom