Mikasa gani umeipitia Jf ambayo hutoweza kuisahau kamwe

Mikasa gani umeipitia Jf ambayo hutoweza kuisahau kamwe

Kwenye jukwaa letu pendwa kila mtu amekumbana na mikasa majanga na vituko mbalimbali ambavyo haviwezi kumtoka kwenye mind yake, mi naanza na hivi:

1. Sitosahau siku najiunga jf niliambiwa na member mmoja humu kuwa eti mimi ndio mmiliki wa JF nilishangaa sana yani iweje mi mgeni ndo niwe mmiliki. Jamaa ikawa kila nikicomment ananijia kwenye comment huku akinipamba " sawaaa boss" aisee siwezi sahau lile jamaa sijui alikuwa na nia gani.

2.Sitasahau nilivyokutana na avatar moja hivi jamvini ina dada mmoja hivi wa kiarabu kipindi hiko mimi mgeni sasa mate yakawa yananidondoka nikaanza harakati za kumlia timing PM kumbe alikuwa wa kiume jamaa alivoona namsumbua sana aliniporomoshea mitusi balaa kuanzia siku hiyo alibadilisha avatar

3.Siwezi kusahau siku moja tuliongea mambo ya kibiashara na jamaa mmoja hivi humu jamvini sasa siku tumekutana tuweke sawa plan yetu daa jamaa akawa ananitazama kama haamini vile huku kapigwa na butwaa mpaka nikawa naona soo. jamaa akawa anauliza mara mbilimbili kwamba wewe ndo babumawe namjibu akawa haamini kabisa aisee tangu siku iyo nikaona kumbe wewe unaweza ukawa unapost vitu humu kuna watu wanakuzingatia na wanakujengea picha yao.

4. Sitasahau jamaa mmoja simkumbuki aliandika thread humu kuwa yeye katembea na mademu 500 kwahiyo anatafuta wa 501, aisee ile post ilinifurahisha sana kila siku ikinijia huwaga najiuliza jamaa alikuwa anawazaga nini mpaka akaposti vile.
Wew una damu gani mzee yote hayo yakukute wew tu?
 
Mimi figganigga topic yake ya kupeleka mahari hahaaaaaaaaaaa sijui Kama nilishawahi kucheka humu JF Kama siku niliyosoma huo mkasa Hahaaa ... ishu ya kambuzi kalikopotea sio ndogo, sitasahau Kamwe 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nilitaka kuandika kitu kinachoelekeana na hiki pia

Naona kama hii ID imekuwa na maneno mengi sana siku hizi....ama ni mimi sikunotice uwepo wake kabla
Maybe he/she tryin hard to build up 'jeiefu sivii'...just maybe!
 
Mimi figganigga topic yake ya kupeleka mahari hahaaaaaaaaaaa sijui Kama nilishawahi kucheka humu JF Kama siku niliyosoma huo mkasa Hahaaa ... ishu ya kambuzi kalikopotea sio ndogo, sitasahau Kamwe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Naomba link ya huo uzi
 
Back
Top Bottom