komoakomesha
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 285
- 407
Mkuu hiko kitabu nataka kwa Dodoma nitakipata wap ,Wakuu habarini za mchana?,bila shaka Mungu amewajaalia afya njema.Poleni pia kwa majukumu ya haya masumbufu ya maisha,Mungu ni mwema atafungua njia kwa wote wasumbukao na wenye kulemewa na haya maisha.
Kitabu kimetoka na kiko tayari kabisa,ila kutokana na maboresho kukifanya kuwa bora,gharama za uchapaji ziliongezeka kidogo na hivi sasa kinapatikana kwa gharama ya Tsh 10000/=tu,hivi sasa nipo Morogoro kuna jambo lilinileta huku linalohusu vijana namna ya kujitambua ambapo msimamizi mkuu ni ELIMIKA TANZANIA,hivyo niwaombe mlioko Morogoro na mnahitaji kitabu cha UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA - Sehemu ya 1,tafadhali nifahamisheni ndugu zangu. Watu wa Dar es salaam na mikoa mingine ambako nilikuwa nimepewa oda,kuanzia Jumatatu nitawafikia.
Watu wa Morogoro nipo kuanzia leo Ijumaa tarehe 5 mpaka tarehe 7 siku ya jumapili.
Kwa mawasiliano zaidi nipigie hapa +255683588226
Kwa Sasa Mimi nitapigwa ban ,nitakula sahani moja na wakosoaji humu Kama huwezi kufatililia story utoke humu sio kumkwamisha magere asisimulie story wengi tunajifunza hapaMkuu hivi kweli uko serious?,aliyekwambia mtu aliyetubu dhambi alizofanya hapendi pesa ni nani?,hujui pesa ndiyo inayoendesha maisha ya mahitaji yetu ya kila siku?,na aliyekwambia kwamba nimesitisha masimulizi ni nani?,Mimi nimetoa tangazo la namna ya watu kupata vitabu,wewe unaleta ujuaji mwingi usiyokuwa na faida,Quran na Biblia ni vitabu vitakafu lakini bado vinauzwa,hata hao wanaovigawa bure unakuta wamevinunua mahali.
Hiki kisa hapa nitaendelea kukisimulia lakini lazima na watu wanaotaka kopi za vitabu wajipatie maana kwanza kuna kisa humu sikukimalizia lakini kwenye kitabu kitakuwepo,pia kuna mambo ya kikatili niliyafanya ambayo hapa sitaweza kuyazungumza lakini kwenye kitabu yapo,pia wengine huwa wanataka kitabu kama kumbukumbu,hivyo mkuu msiwe mnapenda kupotosha.
Mimi mwenyewe ndiye niliamua kusimulia historia ya maisha yangu,hukunituma wewe,hivyo muda mwingine ni vema ukatulia wanaoweza watanunua.
ShunieOoh pole sana dear
Basi lwanda jamani usije ukasusa tupo tunakusubiri hata ukirudi kutoka morogoro tupo sisi
Audio ya nyoka au makengeza?Changeni buku buku niwatumie audio.
Mkuu hivi kweli uko serious?,aliyekwambia mtu aliyetubu dhambi alizofanya hapendi pesa ni nani?,hujui pesa ndiyo inayoendesha maisha ya mahitaji yetu ya kila siku?,na aliyekwambia kwamba nimesitisha masimulizi ni nani?,Mimi nimetoa tangazo la namna ya watu kupata vitabu,wewe unaleta ujuaji mwingi usiyokuwa na faida,Quran na Biblia ni vitabu vitakafu lakini bado vinauzwa,hata hao wanaovigawa bure unakuta wamevinunua mahali.
Hiki kisa hapa nitaendelea kukisimulia lakini lazima na watu wanaotaka kopi za vitabu wajipatie maana kwanza kuna kisa humu sikukimalizia lakini kwenye kitabu kitakuwepo,pia kuna mambo ya kikatili niliyafanya ambayo hapa sitaweza kuyazungumza lakini kwenye kitabu yapo,pia wengine huwa wanataka kitabu kama kumbukumbu,hivyo mkuu msiwe mnapenda kupotosha.
Mimi mwenyewe ndiye niliamua kusimulia historia ya maisha yangu,hukunituma wewe,hivyo muda mwingine ni vema ukatulia wanaoweza watanunua.
thnx babeOoh pole sana dear
Mm ninazo zoteChangeni buku buku niwatumie audio.
[emoji23][emoji23][emoji23]upo vizuri sekta ya ubembelezaji
Shusha vitu mkuuMKASA WA PILI -Sehemu ya 42.
Inaendelea.............
Usiku huo nilikuwa nina na mawazo mengi sana lakini nilijipa moyo maana sikuwa na namna nyingine ya kufanya!.Kwakuwa yule Malikia alinipa ndani ya wiki niwe nimetekeleza lile agizo nilituliza kwanza akili ili nione cha kufanya.Niliendelea na ujenzi wa apartment zangu na sikuwa na presha kabisa maana kama ni kuua nilikuwa nishazoea.Basi nakumbuka siku moja yule shemeji alinipigia simu akaniambia kwamba alienda kupima akagundulika ni mjamzito,kiukweli yeye kwa upande wake alifurahi sana akawa anasema nimemrudishia furaha ambayo siku kadhaa nyuma ilikuwa imetoweka,wakati huo ilikuwa ni mwezi wa 11 mwaka wa 2014.
Nilimwambia "Sawa mke wangu mzuri nami pia nimefurahi maana ndiye atakuwa mtoto wangu wa kwanza na vile nilikuwa napenda kuzaa na wewe nimefurahi sana".
Nilikuwa najifanya kumwambia yule shemu ili asijisikie vibaya maana ukweli nilikuwa naufahamu mimi kwamba hata hao watoto ambao wangezaliwa walikuwa si mali yetu bali walikuwa mali ya wenye mali!,pia huyo hakuwa mtoto wangu wa kwanza kama nilivyomdanganya,maana mwanamke ambaye nilikuwa nimempatia mimba tayari alikuwa Zainati.
Aliniambia "Sawa baby mimi sitoweza kukaa peke yangu nataka nije huko tuishi wote ".
Nilimuuliza "Hapo nyumbani utamuacha nani?".
Aliendelea kuniambia "Yupo mdogo wangu na wanaye wawili walikuja kutoka Arusha sema sikukwambia mapema".
Niliendelea kumuuliza "Kwahiyo watakaa hapo siku zote?".
Aliniambia "Nilimwambia aje akae huku maana jamaa waliyekuwa wakiishi naye alimpata mwanamke mwingine akaoa akamtelekezea watoto,hivyo yupo yupo tu nataka nimtafutie kazi awe anafanya".
Nikamuuliza "Kwahiyo mke wangu unakuja lini?".
Nilimuuliza anakuja lini niweze kujiandaa maana kule chumbani kwangu sikuruhusiwa kumuingiza mwanamke yeyote,na yeye asingekubali nimlaze vile vyumba vingine alale mwenyewe halafu mimi nikalale chumbani kwangu mwenyewe.
Aliniambia "Nitakujulisha baby uje unichukie ngoja kwanza kuna mambo niyaweke sawa hapa nyumbani nadhani next week nitakujulisha".
Basi siku moja usiku chumbani kwangu nikiwa nawaza hapa na pale,nikapata wazo la namna ya kumuua yule binti ili isiwe rahisi mimi kufahamika na nilihakikisha nawapiga misumari ya ushirikina ndugu zake akiwemo mama yake ili wasiwe na akili ya kwenda kwa waganga kuangalia chanzo cha kifo cha binti yao.Asubuhi kulivyokucha niliingia chumba cha siri,kuna dawa ambayo nilianza kuitengeneza ile dawa ilipaswa ifanyike kwa umakini mkubwa sana maana ningekosea kidogo tu,yule binti anageitumia alikuwa anakufa na kukauka palepale kama mkaa!.Sikutaka afe kawaida bali nilitaka nisababishe chanzo cha kifo chake.Nilipomaliza kuitengeneza nilienda nikaiweka kwenye majani ya chai nikaichanganya vizuri nikiwa na lengo kwamba akiisha amka cha kwanza kushughulika nacho ilikuwa ni chai halafu ndiyo mambo mengine yanaendelea,nilisema akiisha itumia ile dawa ningeitupa maana haikupaswa mtu mwingine aitumie!.Ile dawa niliyoitengeneza ilikuwa na sifa ifuatayo,nilitaka nimuwekee mimba ya uongo tumboni mwake na akienda kupima hospitali ionekane ana mimba,nilitaka ile impelekeshe hatimaye apoteze maisha!.Wakati huo nilikuwa nina roho chafu sana,kiukweli kuna muda huwa nikikaa najiona nilifanya dhambi nyingi sana kuliko hata Ibilisi alizozifanya ila kwakuwa hivi sasa nilishajisalimisha kwa Yesu hiyo ndiyo inayonipa tumaini jipya kwenye maisha yangu.
Hivyo ndivyo nilivyofanya,baada ya kupika chai na kuinywa,nilichukua yale majani nikaenda chumbani kwangu nikayamwaga chooni kisha nika-flash na maji mengi.Ilpofika jioni alianza kutapika kama mtu mwenye mimba,alikuwa hajui kilichokuwa kinaendelea masikini ya Mungu!.
Nilijifanya namuuliza"Wewe leo unatatizo gani maana nakuona kila mara unakimbia chumbani".
Aliniambia "Hapana kaka niko vizuri tu".
Nadhani pia na yeye alishajua zile ni dalili za mimba maana alikuwa mtu mzima ila akawa kama ananificha nisijue kitu wakati kumbe mimi ndiye nilikuwa chanzo.Ile hali iliendelea kumsumbua sana,siku iliyofuata nilimpigia dada yangu mkubwa nikamwambia amueleze Shangazi kuhusu huyo binti yake hali aliyokuwa anaipitia,nilijiwahisha mapema ili kuanza kujiondoa kwenye lawama.
Nilimwambia "Sista hebu mwambie mama yake aje kama vipi ampeleke hospitali maana huyu dogo kuna mambo siyaelewi,yawezekana akawa na mimba maana kwa dalili hizi,mmh sijui!".
Dada aliniambia "Eeeh jamani mbona mapema sana,hivi huyo mtoto kakutwa na nini?,mbona alikuwa mstaarabu sana?".
Nilimwambia "Wewe unasema alikuwa mstaarabu kwani ulikuwa ukiongozana naye kwenda shule?,hivi wewe watoto wa siku hizi unawajua vizuri kweli?".
Dada aliniambia"Ila hilo nalo neno mwenzangu,ngoja basi nimwambie mama yake".
Haukupita muda mrefu mama yake alinipigia simu nikamweleza kila kitu akasema nimwambie binti yake aende!.Baada ya siku mbili yule mdogo wangu kuwa ameenda kwa mama yake ambaye alikuwa Shangazi yangu sikutaka kabisa kucheza mbali maana nilitaka nifuatilie kila hatua.Nilienda mpaka kwa Shangazi nikamkuta ila binti alikuwa ndani!.
Nilimuuliza Shangazi "Mlimpeleka hospitali?".
Shangazi aliniambia "Ndiyo mwanangu nilimpeleka afanyiwe vipimo".
Niliendelea kujifanya namuuliza "Ni nini kilichokuwa kinamsibu".
Shangazi akaniambia "Itakuwa nini zaidi ya mimba mwanangu,nilimkanya sana huyu mtoto kuhusu wanaume akiwa bado anasoma lakini alikuwa anielewi".
Nilimuuliza Shangazi "Kwani mpaka sasa kesha waambia hiyo mimba kampa nani Shangazi?".
Nilimuuliza shangazi nikiamini atakuwa alimwambia mtu aliyempa mimba maana kwa binti mzuri kama yule aikuwa rahisi kukosa mtu ambaye niliamini ndiye angebebeshwa zigo la lawama.
Shangazi aliniambia "Aseme wapi?,nimejaribu kumuuliza hasemi,toto limechukua akili ya baba yake lina kiburi kama nini!".
Nilimwambia shangazi "wakati alipomaliza shule nilitaka kuna mahali nimpeleke akafanye kazi lakini sasa kwa hali hii itabidi kwanza ajifungue ndiyo tuangalie utaratibu mwingine".
Nilimuuliza Shangazi "Kwani yuko wapi?".
Shangazi aliniambia "Yuko ndani huko".
Shangazi akaanza kumuita "wewee........njoo huku unaitwa".
Daaah! kiukweli nilipo muona nilitamani kulia maana tumbo lilikuwa kubwa kama mimba ya miezi 5,nilianza kumuhurumia nikijua kabisa mimi ndiye niliyesababisha!.
Nilijifanya namuuliza "Hebu nieleze mdogo wangu nani ni muhusika wa hii mimba,mimi nitakusaidia ,wewe niambie ukweli usinifiche".
Alianza kuniambia "Hii mimba itakuwa ya ......... maana nilitembea naye kabla hata ya kuanza mitihani,mara ya mwisho kufanya naye mapenzi ilikuwa kabla ya mitihani,nakumbuka tulipimwa shuleni kabla ya mitihani lakini sikuwa na mimba sasa na mimi nashangaa kaka".
Alikuwa akieleza yule binti huku machozi yaki mlenga lenga machoni,nilimuhurumia sana na nilijiona nimefanya kitendo cha kikatili sana,sikuwa na namna nyingine ya kufanya ilipaswa iwe hivyo.
Nilimwambia "basi sawa kwakuwa umeniambia ukweli wewe kaa nyumbani ukishaa jifungua mimi nitakupeleka shule za kulipia ukasome A - level".
Aliniambia "Sawa kaka nimekuelewa".
Basi nilimuaga Shanghazi nikaondoka zangu,kuna kiasi cha pesa nilimpatia ili kiwasaidie hapo nyumbani kwa ajili ya matumizi.Siku iliyofuata kama saa 8 mchana alinipigia simu dada yangu akanimbia yule binti kafariki,sababu za kufariki kwake ilikuwa tumbo limemuuma sana,sasa wakati wakiwa njiani kumpeleka hospitali akawa amekufa kabla hata ya kufika hospitalini,nilihuzunika sana lakini sikuwa na njia nyingine ya mimi kuepuka adhabu zaidi ya kufanya kile nilicho ambiwa nikifanye na Malikia.Ule msiba niliugharamikia siku zote,baada ya siku hiyo kumaliza kuzika kama kawaida usiku nilisikia sauti ya Malikia ikiniita kwenye kile chumba cha siri,niliamka kitandani nikaelekea huko,nilipoingia desturi ilikuwa ni ileile ya kusujudu na kuanza kusikiliza maelekezo nitakayoambiwa!.
Malikia aliniambia "Umenifurahisha sana kijana wangu mtiifu".
Aliendelea kuniambia"Wewe ni mtiifu sana na ndiyo maana nakupenda sana,hebu omba chochote utakacho nitakupatia".
Nilimwambia "Yule mwanamke ambaye anataka tuishi wote amesema anataka kuhamia hapa,sasa itakuwaje Malikia?".
Malikia aliniambia "Usiwe na wasiwasi kijana wangu,atakuja na utaweza kumdhibiti".
Nilimuuliza "Sasa si atataka tuwe tunalala wote chumbani kwangu na moja ya maelekezo niliyopewa ziwani ni kwamba mwanamke yeyote asiingie chumbani kwangu?".
Ndipo Malikia aliniambia "Huyo mwanamke ni mali yetu si yako hivyo wewe lala naye popote utakapo".
Baada ya kusikia hivyo nilishituka kidogo sikuelewa ile kauli alikuwa akimaaniaha nini aliposema ya kwamba yule shemeji alikuwa Mali yao.Baada ya yale maelekezo yule Malikia aliniambia "Shika hii".
Alinipa kadude fulani kalikokuwa kadogo kama goroli,kisha akaniambia "Kesho saa 6 usiku nenda mpaka pale kwenye apartments yako unayojenga uchimbe katikati ya uwanja na uweke hiko kitu nilichokupatia na nitakupatia maelekezo baada ya wewe kufanya hivyo".
Nikamjibu "Sawa Malikia".
Baada ya maelekezo hayo alitoweka mle chumbani kama upepo.Kiukweli mara ya kwanza mimi nilikuwa nikiogopa sana lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga hofu ilikuwa ikiinisha,nilipokuwa najua nimekosea ndiyo mkojo ulikuwa unakaribia kutoka maana nilijua fika nitakavyo muona Malikia sivyo nilivyomzoea,nilipofanya vizuri alichokuwa akiniambia nilikuwa naingia chumbani bila hofu kabisa!.Basi nilifunga zangu mlango wa kile chunba cha siri na kuelekea chumbani kwangu kulala.
Itaendelea....................
hawa ndio wanawake wanaokulaga hela zangu yan wanajua kubembeleza wanawake wa hivyo hatari sana
Mikasa hii inasikitisha sana,mpaka mwili wangu unasisimka kwa hofu.MKASA WA PILI -Sehemu ya 42.

we sasa ulichokereka nn mtoto wa kiume? kitabu tutanunua,kule alikoenda tulikipia...na hapa aflow tu...We jamaa utakua na homoni za kike wewe ,mwanaume unakua Kama demu ,umetukera sana
We mchaga nini maana ndio mnapenda kubembelezwa hatarii
Hahhaha niachee[emoji23][emoji23][emoji23]upo vizuri sekta ya ubembelezaji