MKASA WA PILI - Sehemu ya 21.
Inaendelea.............
Wakati nikiwa geto kwangu nilisikia sauti ikiniambia niende mkoa wa Mbeya,nikifika Mbeya nitapewa ishara ya nini cha kufanya!.Kwakuwa tayari nilikuwa nimeshaizoea ile hali ya kutoa kafara,kiukweli nilikuwaga siogopi hata kidogo wala sikuwa na wasiwasi.Wakati ule sikuwa kabisa na akili nyingine zaidi ya kuona nilikuwa nina faidi maisha,kila nilichokitaka nilikipata kwa wakati sahihi.
Basi nilijiandaa nikaweka mambo yangu sawa,nilipohakikisha kila kitu kipo sawa,niliushika mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na irizi nikatamka "Ninataka niwe Mbeya eneo lililokusudiwa muda huu",ilikuwa ni kitendo cha kufumbua na kufumbua nikajikuta nipo Uyole,mkoa wa Mbeya!.Kiukweli ile irizi ambayo iliwekwa mkononi mwangu na yule Malikia ilikuwa na nguvu za ajabu,kipindi hicho ilikuwa ikinipa kiburi sana mpaka nikawa nawaoana binadamu wenzangu kama takataka.Namshukuru sana Mungu kwa kunitoa huko,Mungu wetu ni mwema sana,uwezo,upendo,rehema na fadhili zake hazina mwisho.Basi nilipofika hayo maeneo ya Uyole,kuna gari niliiona ilikuwa costa,hiyo costa ndiyo niliyoambiwa kwamba,waliomo ndani hapaswi kupona mtu,ndiyo gari ambayo ilipaswa nikaiangushe ili nitoe kafara,hiyo gari ilipofika maeneo nilipokuwa nimesimama,konda akawa anasema "Kyela hiyooooo,twenzetu Tukuyu mpaka Kyela hiyoooooo!".
Nilipanda ndani ya ile costa na kama kawaida sikulipa nauli,yule konda hata hakuniuliza kuhusu nauli.Sasa ile gari ilifika kwenye mji mmoja ulikuwa unaitwa Kimo,huo mji wa Kimo ulikuwa kabla ya kufika Tukuyu!,ile sauti iliniambia nishuke kwenye gari halafu niendee mbele ya Tukuyu kuelekea Kyela nikaisubiri.Nilifanya kama ile sauti ilivyonitaka nifanye,niliposhuka tu kwenye ile gari nilipotea ghafla yale maeneo na hapo Kimo nikajikuta nipo eneo la tukio,Kiukweli hilo eneo ambalo ilipaswa nitoe kafara kulikuwa na mteremko mkali sana,sikumbuki yalikuwa maeneo gani maana kulikuwa na miti mingi sana ya mbao hilo eneo,nadhani ilikuwa ni hapohapo Tukuyu,sikuweza kupafahamu kwasababu ya ule msitu.Ila mkoa ulikuwa ni Mbeya,wilaya ya Rungwe,mji wa Tukuyu.
Basi nilipofika hilo eneo niliweka tego kama kawaida,mkononi wakati huo nikiwa nimeshika kibuyu kwa ajili ya damu,baada ya kusubiri kwa muda niliiona ile costa ikiwa inakuja kwa mwendo wa kasi sana,ilipofika lile eneo nililoweka ile dawa ya tego,ile gari ilihama njia ikaelekea kwenye lile shamba la miti ndipo ilipopata ajali mbaya sana.Nilisogea taratibu kwenda kuanza kuchukua kilichonipeleka huko,lakini nilipotaka tu kuanza kuchukua damu za watu waliyokuwa wamekufa,ghafla niliwaona akina mama wawili ndani ya ile gari wakiwa wananiangalia sana,kisha wakaanza kuniambia "Wewe mtoto unafanya nini?".
Wale kina mama walikuwa wachawi na watu wengine walipokuwa wamelaliwa na viti wao walikuwa wamekaa wakinikodolea macho,na yaelekea huko walipokuwa wakienda walikuwa wanaenda kwenye mikutano ya kichawi,waliniita mimi mtoto si kwamba umri wangu bado ulikuwa wa kitoto,la hasha! bali walionyesha dharau kwamba mimi sikuwa na chochote cha kuwafanya,kwa maana nyingine ni kwamba uwezo wangu ulikuwa mdogo.Niliwaambia kwakuwa waliniita mimi mtoto,wao ndiyo ningekuwa wa kwanza kuchukua damu zao na kuweka kwenye kibuyu,walidhani natania lakini nilikuwa siwatanii hata kidogoo,nilitaka niwaonyeshe ya kwamba sikuwa mtoto kwenye ile kazi,Kama nilivyosema hapo awali kwamba nilikuwa nina uwezo wa ajabu na kiburi kilikuwa kimenijaa sana kipindi hicho.Niliwasogelea na kuanza kushindana nao kichawi,nilipoona wanataka kunipotezea muda,nilitamka ya kwamba "Naomba mkauke muwe kama mkaa",haikuchukua muda walikuwa wamekauka kama mkaa,Wao ndiyo niliyoanza nao,baada ya hapo nilianza kukusanya damu za abiria wengine na kuzitia kwenye kibuyu,nilipomaliza kufanya lile zoezi nilipotea yale maeneo,nikatokezea lile eneo nililokuwepo mwanzo la Uyole!.
Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa,niliingia kupata chakula kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa mkubwa kama hoteli,sasa ile nimeingia ndani ya huo mgahawa niliona kuna mama na binti walikuwa wakitoa huduma hapo hotelini wakiwa uchi kama walivyozaliwa,alikuwa mwanamke mmoja mnene na binti yake ambaye pia alikuwa uchi.Sasa kitu kibaya zaidi ni kwamba,huyo binti yake yeye alikuwa akivuja damu kwenye sehemu yake ya siri (uke),zile damu alikuwa akizichukua na kuzipakaza kwenye vile vyakula vya wateja walivyokuwa wamemwagiza!.Aisee ile hali sikuwahi kuiona mahali popite pale,ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kushuhudia ule uchafu,kwa bahati mbaya sana hakuna mteja ambaye alikuwa akiona yale matukio yote isipokuwa mimi niliyekuwa na uwezo huo.
Huo mgahawa ulikuwa umechangamka sana maana hadi madereva wa magari makubwa niliona walikuwa wakiingia kula pale!,ukimuondoa yule mama na yule binti niliyewakuta uchi,pia kulikuwa na wahudumu wengine wawili,mmoja alikuwa mpishi na mwingine pia alikuwa akihudumia lakini hawa wao walikuwa wamevaa nguo zao za kawaida,na walikuwa hawaelewi chochote,wateja wengi walikuwa wakiingia kwenye ule mgahawa wao walikuwa wakiwaona wamevaa nguo,kumbe haikuwa hivyo.Sikupata shida kuelewa kwamba yule mama ndiye alikuwa mmiliki wa ule mgahawa na yule aliyekuwa akivuja damu ukeni alikuwa binti yake wa kumzaa!.Yule mama aliponiona alinifanyia ishara ya kidole mdomoni,kwamba nikae kimya!Yule binti aliyekuwa akivuja damu alikuwa akinitolea macho sana,nilimuona anakuwa na wasiwasi mkubwa!,uenda alidhani nilikuwa nimeenda pale kuwafichua.Basi nilimuita yule mwanamke nikamwambia aniletee chakula ila kiwe kisafi,tofauti na hapo ningemuumbua!,alimuita yule binti aliyekuwa kavaa nguo akamwambia "Mpe yule kaka chakula".
Zilikuja ndizi na nyama zikiwa zimejaa sahani,kabla ya kula nilianza kukiangalia kile chakula kama kilikuwa kisafi ama la!,baada ya kujiridhisha kwamba kilikuwa kisafi kwa maana kwamba hawakuweka mambo yao ya kishirikina nilianza kula!.Wakati nakula watu wengi walikuwa wakiingia kupata msosi wakiamini ni msosi mtamu kumbe yule binti alikuwa akichanganya na damu zake zilizokuwa zinatoka ukeni!.Sasa Wakati nikiwa bado naendelea kupata msosi aliingia jamaa mmoja akiwa na mwanamke,bila shaka alikuwa mtu na mke wake,walipotengewa chakula kabla ya kula walifanya ishara ya msalaba,nadhani walikuwa wakiombea kile chakula,ile ishara ya msalaba haikusaidia kitu kwani walilishwa uchafu kama wenzao!.Ule mgahawa ulikuwa na wateja wengi sana,yule mama kama ni pesa basi alikuwa akizipata ki kwelikweli!.
Ndugu zangu ukiamua kuwa mfuasi wa Kristo basi achana na mambo mengine ya duniani vinginevyo unaweza ukadhani Yesu anakulinda kumbe hakuna,yule jamaa aliyeingia kwenye ule mgahawa na mkewe,ilionekana walikuwa wakimpenda sana Yesu kwa maneno ila matendo hakuna!,Kiukweli wangekuwa watu wa maombi wasingelishwa ule uchafu,lakini kwasababu wengi wetu dini tumezifanya kama fasheni ilikuwa haijawasaidia kitu,ukiamua kuwa mtu wa dini,ni vema ukawa mtu wa dini,lakini ukiamua kuwa mtu wa kidunia,ni vema ukawa mtu wa kidunia.Inapaswa uchague moja ambalo utasimama nalo,mimi mwenyewe kuna wakati nilishindwa kufanya tukio lolote la ushirikina kwasababu kuna watu niliyokutana nao wakiwa na nguvu ya Mungu,nilishindwa pamoja na ujanja wangu wote!.Hivyo watu wengi waliyolishwa kile chakula chenye uchafu,hawakuwa na ulinzi wa Mungu hata kidogo.
Baada ya kumaliza kula niliondoka zangu bila kulipa,yule mama aliniita kabla ya kuondoka akaanza kuniuliza "Vipi mwenzetu wewe niwa nchi gani?".
Nilimwambia "mimi natokea Kigoma na hapa nilipo nipo safarini kurudi kigoma?".
Yule mwanamke alikuwa akinishangaa sana namna nilivyokuwa jasiri,wakati huo naongea naye alikuwa uchi kama alivyozaliwa ila watu wengine walikuwa wakimuona amevaa nguo!.Nipomaliza kuzungumza naye nilimwambia mimi naondoka zangu.Basi niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi nikatamka kama ambavyo nimekuwa nikifanya,ndani ya sekunde nilijikuta nipo geto kama kawaida,ndipo nilikiweka kile kibuyu chini ya uvungu,nilijipumzisha kidogo kisha baada ya kuamka nilielekea nyumbani kwa mama kupata chakula.
Itaendelea......................