Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Nilichogundua ni kwamba kuna nyomi kubwa sana linatufuatilia msije shangaa Mara baada ya stori kuisha huko mtaani ukakutana na maneno haya "Shipa la kimkakati" yakiwa yametamalaki
IMG_20201223_210736.jpg
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 23.


Inaendelea.............



Asubuhi nilipanda zangu gari kurejea Mwanza na wembe ulikuwa ni ule ule wa kusafiri bila kulipa nauli.Niliingia Mwanza mida ya saa 2 usiku,kwakuwa nilikuwa nimechoka niliingia geto kulala mpaka asubuhi ambapo niliamka na kuelekea kule kibaruani kwangu kama kawaida!.Ile shule niliyokuwa nafundisha haikuwa ya serikali bali ilikuwa ya private,kwakuwa nilikuwa nalipwa kutokana na vipindi nilivyokuwa nahudhuria,hivyo haikuwa taabu sana na haikunizuia kuendelea kufanya mambo yangu mengine!.Baada ya siku mbili nilielekea nyumbani Nyegezi kumsalimia mama,sasa wakati naondoka kwa mama,nilikutana na binti mmoja ambaye alikuwa jirani yetu hapo nyumbani Nyegezi,yule binti alikuwa ni mzuri sana!.Kuna wakati nilikuwa nikimtongoza lakini sikuwahi kuambulia kitu,nyumbani kwao kulikuwa na uwezo sana,nakumbuka alikuwa akisoma St.mary enzi hizo.Kwa namna ambavyo wazazi wake walivyokuwaga na uwezo na kwa jinsi alivyokuwa mzuri,kiukweli alikuwa ana maringo sana,alikuwaga ananifahamu kwasababu tulikuwa majirani,ila kwakuwa sikuwaga na uwezo wakati huo,yaani hata nilikuwa nikimsimamisha asimami,kiukweli niliteseka sana wakati huo.

Sasa nilipomuona sikuamini kwasababu alikuwa amejaa sana tofauti na mwanzo,pia uzuri wake ulikuwa umeongezeka mara dufu!.Kwakuwa alikuwa hajaniona,ilibidi nimuite,nilimuita bahati nzuri akanisikia akasimama.

Nilimwambia "Mambo Yusta".

Aliniambia "Poa,za siku?".

Tuliendelea kupiga stori na kwakuwa nilikuwa nina mpenda sana sikuchoka kumtazama.

Nilimuuliza "uko wapi siku hizi mama?".

Aliniambia "Nipo Dar nasoma IFM mwaka wa pili".

Aliniambia "Nina haraka mwenzio tutaongea siku nyingine".

Nilimwambia "Naomba namba yako ya simu nitakupigia Yusta".

Akaniambia "Sina simu J".

Sasa wakati namuomba namba yake ya simu,mkononi alikuwa ameshikilia simu.

Nilimuuliza "Hiyo uliyoshika mkononi niya nani?".

Aliniambia "J hii si yangu,ingekuwa yangu ningekupa namba".

Nikamwambia "basi sawa".

Aliondoka zake na mimi nikaendelea na safari,lakini moyo wangu haukuridhika kabisa kumuachia yule mtoto mzuri anipite hivi hivi.Sasa wakati anasoma St mary's kulikuwa na stori kwamba alikuwa akitembea na mtoto wa kigogo mmoja hapo Mwanza ila mimi sikuwahi kulithibitisha hilo!.Kiukweli nilijisemea "Huyu mtoto lazima na yeye nimkomoe maana anajifanya yuko matawi ya juu,lazima anitambue mimi ni nani!".

Ndugu zangu labda tu niseme ya kwamba iwapo kutakuwa na muhusika yeyote ambaye alihusika kwenye harakati zangu hizo za maisha ya dhambi niliyoyaishi zamani na akafanikiwa kusoma huu uzi,tafadhali sana naomba anisamehe maana bado nilikuwa kwenye giza la Ibilisi na sikuwa na akili nilizo nazo leo,tafadhali sana naomba mnisamehe sana,nipo tayari kubeba adhabu yeyote maana tayari nishampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu hivyo sitaona shaka yoyote kufa nikiwa ndani ya Yesu!,nisameheni sana ndugu zangu wa Mwanza niliowakwaza na wa maeneo mbalimbali ya nchi yetu hii ya Tanzania.

Basi niliporudi geto nilikuwa namuwaza mtoto mzuri Yusta pamoja na Zainati na hawa wote niliapa ya kwamba nitalala nao kitanda kimoja niwapige bakora za kim-kakati mpaka wanyooke!.Nilitaka kuitest ile dawa niliyopewa na mzee Nchibaronda siku chache zilizopita na tageti yangu ilikuwa kwa hao warembo wawili!.

Wakati huo japo nilitembea na wanawake wachache lakini walikuwa na viwango vya kimataifa,kama ni bidhaa basi hao wanawake ningediliki kusema walikuwa wamethibitishwa na shirika la viwango la kimataifa,yaani ISO.

Baada ya ile wiki moja kuisha nilimpigia yule mama niliyempa kazi ya kupamba ile nyumba yangu na aliniambia nyumba iko tayari ila kuna vitu vidogo walikuwa wanamalizia.Basi nilimwambia mimi nahamia hivyo hivyo kwa maana nishachoka kukaa geto,nilipaona kule geto nilikoanzia maisha ya kujitegemea hapakuwa na hadhi yangu tena kwa wakati huo;kiukweli wakati huo nilikuwaga ninapendeza sana,nilikuwaga nikivaa nguo zinanikaa kwenye mwili kama vile nilishonewa mimi.Nilienda kuikagua ile nyumba na kiukweli mpaka niliogopa,kwa muonekano ule nilihofia uenda serikali ingenishitaki kwa kuwa na nyumba nzuri kama ile wakati kipato changu kilikuwa kidogo,hata hivyo nilikuwa nimefanya namna ya kimazingara ambayo mtu yoyote ambaye angeleta fyokofyoko basi alikuwa anaenda na maji.Kwa wakati huo pia niliplani kufanya biashara ya ujenzi,yaani nilitaka niwe na kampuni ya ujenzi wa nyumba halafu zikiisha napangisha!.

Sasa ulifika muda wa mimi kuondoka geto na kuhamia rasmi kwenye nyumba yangu kile Igoma.Vile vitu nilivyokuwa nikikaa navyo geto kuna jamaa yangu yule aliyekuwa akifanya kazi kiwandani nilimwachia vyote,mle ndani mimi nilitoa na kile kibuyu na yale mabegi dogo na kubwa yaliyokuwa yakizihifadhi pesa zangu,pamoja na dawa zangu zote.Nilihamia kwenye nyumba yangu rasmi na kuna chumba cha siri ambacho nilikitenga na kilikuwa safi kupita maelezo.




Itaendelea...........................
 
Back
Top Bottom