Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Vile nasubiria episode inayofuata!
20200525.JPG
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 12

Inaendelea.............

Tuliondoka Mwanza majira ya saa 12 Asubuhi,Ile njia mimi mwisho wangu ulikuwa katoro,Geita lakini kuelekea huko mbele sikuwahi kufika na hiyo ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza!,Mimi nilibeba kibegi kidogo nkaweka nguo za kubadilisha maana niliwaza yasije kunikuta yaliyonikuta hapo nyuma!
Jamaa yangu yule yeye alienda akiwa amevaa nguo alizokuwa nazo na uenda nikasema safari kama hizi yeye ni mzoefu!

Ile safari ilikuwa ndefu sana,Jamaa alinambia tukifika Kasulu sisi tutashuka maana baada ya kufika hapo Kasulu ingetubidi tuelekee kuna kijiji kimoja kinaitwa Munyegera!.
Ilituchukua masaa kama 9 hv au kumi mpaka kufika Kasulu mjini na kwakuwa bado ilikuwa mapema Jamaa aliniambia tutafute kwanza sehemu wanayouza chakula hapo Kasulu tule!

Baada ya kumaliza kupata chakula jamaa alinambia tutafute usafiri wa kuelekea huko kijijini Munyegera,Kwa kuwa mimi ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika hapo kasulu nilikuwa nikishangaa shangaa tu!

Hii nchi ni kubwà sana ndugu zangu sikuwahi kudhani kama ipo siku ningefika kigoma - kasulu!,Basi jamaa akaniambia inabidi tuchukue pale boda boda mpaka huko kijiji cha Munyegera!,Kwakuwa jamaa alikuwa mwenyeji mimi sikuwa na shaka yeyote!,
Tuliita boda mmoja akaja na jamaa alipoongea nae akakubali angetupeleka kwa 15000/=kwa wote wawili.
Tulianza safari sasa ya kuelekea huko Munyegera na ilituchukua kama saa moja na nusu hivi mpaka kufika hapo Munyegera!,Baada ya kufika tulimpa hela yake jamaa akaondoka zake na sisi kuianza safari ya kuelekea maporini!
Yule jamaa alinambia kutoka hapo Munyegera mpaka kwa huyo Mama(Mganga)si mbali hivyo tutembee!

Ilikuwa tayari ishaingia giza na sisi tuliendelea kuchanja mbuga!,Mfukoni mpaka kwa wakati huo mimi nilikuwa nina laki tatu,Jumla nilibeba kama laki tatu na 70000/=hivyo ukijumlisha nauli pamoja na mambo mengine humo njiani nilibaki kama na laki tatu!Sikutaka kupata shida kama niliyoipata hapo nyuma,Japo jamaa tukiwa Mwanza alinambia nitafute laki mbili lakini mimi nilijiongeza!

Basi baada ya kutembea kwa muda mrefu hatimaye tulifika hapo nyumbani kwa huyo Mama mganga na tulipokelewa na mabinti wawili waliokuwa pale!,Kuna watu tuliwakuta pale ilibidi nimuulize jamaa mwenyeji wangu akaniambia hao pia walikuwa pale wamefata tiba!,Akili yangu mara zote ninapokuwa ugenini ni mahali pa kulala!

Kwakuwa ilikuwa ishafika usiku tulikuta umekokwa moto na kuna raia wengine walikuwa wakiota moto pale huku wakiendelea kupiga story za hapa na pale kwa kiswahili chenye lafudhi ya Kiha!

Jamaa alinambia ngoja anaenda kumuona mama mganga kama yupo halafu anarudi,baada ya dakika kadhaa alirudi na kuniambia msaidizi wa yule mama kamwambia Hayupo na anarudi asubuhi hivyo hata hao watu tuliowakuta walikuwa wakimsubiri yeye!,Kwakuwa baridi ishaanza kuwa kali ilibidi mimi na jamaa tusogee kwenye moto pale na tulikaa hapo chini ya mkeka mpaka mimi usingizi ukanipitia!,Nimekuja kushituka bado ni usiku lakini bado jamaa wako macho wakipiga story,Usingizi ulikuwa ukichukua na kushituka,niliendelea na hiyo hali mpaka kulipo pambazuka!,Kuna jamaa pale yeye kazi yake ilikuwa ni kuongeza magogo tu kwenye ule moto kila ulipoonyesha hali ya kufifia!

Asubuhi kila mtu pale alikuwa na ishu zake na niliona kila mtu alikuwa kakaa na mtu ambaye walikuwa wakifahamiana naye!,Yule Mama mganga tuliambiwa karudi na nilijiuliza alirudi vp wakati usiku huo wote hakukuwa na mtu mwingine aliyeingia hapo nkakosa majibu!
Watu tuliowakuta hapo kila mtu alienda humo ndani kwenye nyumba ya mganga na kuelezwa walicho elezwa!,Kuna wengine walikuwa wakitoka wanaondoka jumla na kuna wengine walikuwa wakitoka wanarudi tena nje kukaa nadhani waliambiwa wasubiri!

Tulikaa kwa muda mrefu kidogo na zamu yetu ilipofika tuliitwa na Msaidizi wa yule mama!,Tuliambiwa tunaingia mmoja mmoja ndipo mimi nikamwambia yule jamaa aanze yeye!
Jamaa alikaa humo ndani kama nusu saa hivi halafu akatoka akanambia niende ndani!

Nilipofika ndani nilimsalimia Yule mama ambaye hakuwa Mzee sana kama nilivyofikiria na kabla sijaanza kuongea aliniambia ninyamaze maana maisha yangu yote toka tukiwa Tarime mpaka nimefika hapo kwake anayafahamu hivyo akaniambia nimwambie ninataka nini!,Kiukweli aliponiambia anayafahamu maisha yangu Tangu nikiwa Tarime nilishangaa kidogo!,

Hivyo ilibidi nimueleze kwamba ninataka kuwa tajiri,Aliniangalia akawa anatikisa kichwa tu ,kisha akaniambia "Mbona mwanangu umeharibiwa sana"!,Hauwezi kuwa tajiri mpaka usafishwe kisawa sawa!,akawa ananiambia kwamba nyota ya marehemu Baba ninayo mimi ila kuna kitu kipo hapo katikati kinachozuia ile nyota kung'aa ili niweze kuwa tajiri!

Akaniambia yeye atanisafisha na kunipa dawa ya kinga ili chochote kibaya kitakachonisogelea basi kiende na maji!, akaniambia baada ya kunisafisha itanipaswa niende mpaka kigoma nivuke ng'ambo ya pili upande wa kongo sehemu inaitwa Kalemii,huko kuna mtu ambaye angeniondolea huo mpaka hapo katikati hatimaye nyota ya Baba yangu niipate mimi,maana ilionekana kung'aa sana ila kuna mshenzi mmoja kaizuia na ndo maana ninateseka!

Kiukweli nilivuta pumzi sana maana nilijua nimemaliza kumbe ndo kwanza kazi haijaanza!,Aliniambia itanibidi nikae pale kwa siku tatu ili akimaliza kuwashughulikia wale wagonjwa wengine ndipo nianze dozi!

Nilipomaliza kuongea na yule mama ilibidi nitoke nje kuongea na yule jamaa aliyenipeka na akashangaa sana!,Jamaa akaniambia "Mwanangu jipe moyo,kwakuwa umeamua pasipo kulazimishwa we kuwa na uvumilivu"
Yule mama alitoka ndani na alikuwa akiongea na wateja wake pale nje na alipofika kwetu alimwambia jamaa huyu Mwenzio bado nina kazi naye!,We kama utamsubiri we msubiri maana bado anasafari nyingine!,Jamaa tuliongea nae na hakuwa na namna aliniambia ilibidi aondoke akawahi kazi zake lakini akaniambia mimi ni mwanaume nijipe moyo!,

Nilimwambia jamaa endapo sitorudi nyumbani kwa chochote ambacho kingenipata basi anichukulie vile vyombo vyangu anipelekee nyumbani kwetu,jamaa alikubali!,Aliniaga pale na akaniongezea laki moja tena ila nilimwambia nikirudi ningemrudishia!
Kwahiyo ukijumlisha kiasi jamaa alichonipa na nilichokuwa nacho nilikuwa kama na laki nne!,Wakati jamaa anaondoka nilijikuta nalia kama mtoto maana sasa nilijiona bado nina safari ndefu ukizingatia nilikuwa mgeni!

Nilijipa moyo sana maana niliona ningekata tamaa hakuna ambacho ningefanikisha!

Itaendelea..............
Wahenga wanasema MAJI UKIYAVULIA NGUO HUNA BUDI KUYAOGA
Lakini mm nasema ukiona ya baridi Sana vaa nguo zako ondoka aisee

Mwenzako anakuacha hivi hv

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: T11
Habarini za jioni ndugu zangu,bila shaka mko vizuri!,Kwa wale wa kazi wa Dar es salaam poleni sana kwa joto,Kwa wale wa mikoa mingine sifahamu hali ya Hewa ya mikoa yenu kwa sasa ila tu niwatie shime tuendele kupambana maana maisha ni kutafuta na wala si kutafutana!

Kama nilivyoahidi kwamba nina visa viwili ambavyo nilivipitia mimi mwenyewe kwenye maisha yangu tangu nikiwa na Umri mdogo na nilipokuwa mtu mzima,Kisa cha kwanza kilieleza namna maisha yangu ya utoto yalivyokuwa na mikasa niliyopitia japo kuna visa vingi tu ndani yake sikuvisimulia kwa maana Wakuu walitaka nifupishe stori!

Hivyo ninaona ni wakati sahihi kabisa wa kuelezea kisa cha pili ambacho nimekutana nacho katika maisha ningali mtu mzima!

Tuanze...........

Kwanza kabisa niseme mimi kwa kabila ni Msukuma,Kabila ambalo nimerithi upande wa Marehemu Baba,Baada ya elimu yangu ya Msingi nilifanikiwa kujiunga na Masomo ya sekondari Shule ya Pamba iliyoko Mwanza na baada ya Masomo ya O level nilibahatika kuchaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari ya Minaki kwa ajili ya elimu ya A level,Nilichukua HGE na namshukuru Mungu japo nilikuwa mkorofi lakini kichwani zilikuwemo kidogo!

Baada ya kuwa nimemaliza shule nilirudi Nyumbani Mwanza,Kumbuka baada Bi mkubwa kuwa ameuza nyumba ile Tarime ilibidi Mwanza ajenge nyumba nyingine japo haikuwa kubwa kama ile ya Tarime lakini kwa kiasi fulani ilikuwa nzuri naya wastani!,Nilirudi nyumbani na nkawa napiga deiwaka za hapa na pale kama tuisheni ili angalau niweze kupata hata hela za kununua boxa na mahitaji madogomadogo,Sikuweza tena kumuomba Bi mkubwa pesa maana tayari nshakuwa jitu zima! Basi bana kuna siku katika pitapita zangu mtaani kwa mbali kidogo nkamuona jamaa mmoja tuliyekuwa tumesoma wote Primary kule Tarime!,Kiukweli sikuweza kufahamu kama ndiye au nilimfananisha,Jamaa alikuwa pembeni anaongea na simu,hivyo nilijaribu kusogea karibu nione kama ndiye!

Kweli!,Baada ya kusogea karibu nikamwita jina lake(Naomba nisilitaje maana humu wanasoma watu mbalimbali isije niletea shida),Jamaa aliitika na aliponiona alinifanyia ishara kwamba nisubiri kwanza amalize kuongea na simu!,Basi jamaa alipomaliza kuongea na simu alifurahi sana kukutana na mimi,mimi pia nilifurahi sana maana jamaa alikuwa kabadilika sana na kanenepa ile kishenzi,watoto wa mjini wanasema "Shavu dodo",kiukweli jamaa alikuwa kanawili na nilivyomuona tu inaelekea alikuwa na pesa!
Jamaa aliniuliza "Aisee za miaka mingi? ,mi nkamjibu "Nzuri"

Jamaa akanambia "Hebu nikumbushe we ni nani na nilikuona wapi vile!",Duuuh kimoyo moyo nilijisemea "Ina maana jamaa mara hii kanisahau au ndo umjini mjini"?,Basi ilibidi nimkumbushie jina langu na tulisoma wote Tarime!
Daaah jamaa alicheka sana na tukaanza kukumbushiana matukio,vimbwanga na vitimbi vya shule!,Tulipiga sana pale michapo na nkamueleza mi niliendelea na shule na nkamwambia Tarime tulihama muda sana!
Basi bana alinichukua tukasogea mbele kidogo kumbe jamaa alikuwa kapaki gari!
Tulipanda kwenye gari kuelekea maeneo ya Igoma ambako alikuwa kachukua Hotel huko.

Jamaa kipindi tuko kwenye gari alikuwa ananiambia kwamba yeye baada ya kumaliza shule ya Msingi kwasababu matokeo yake hayakuwa mazuri ilibidi aende kutafuta maisha na sasa yupo huko Mkoani Geita sehemu moja inaitwa Katoro ndo kajenga huko na maisha yake yapo huko,ila siku hiyo alikuwa kaja hapo Mwanza kwa ajili ya ishu zake nyingine!

Labda tu hapa niseme,Huyu jamaa kipindi Tunasoma alikiwa KILAZA darasani na kiukweli ningeshangaa sana kusikia aliendelea na Shule!

Basi baada ya kufika hapo hotelini alipofikia mi nilikaa nje yeye akaingia huko ndani,Muhudumu alikuja pale kuniuliza natumia nini lakini nilisita kumwambia maana sikuwa na kitu na mtu ambaye ndiye mwenye pesa kaingia ndani!,Hivyo nisingeweza kuagiza bila ruhusa ya mtoa pesa!,Baada ya dakika kadhaa jamaa kaja kwa mbwe mbwe kama zote!,"Mwanangu agiza chochote uletewe ule"
Kabla sijamwita muhudumu jamaa alipaza sauti "We muhudumu njoo umsikilize jamaa hapa",Mrume ndago niliagiza Wali Samaki pamoja na Soda!

Jamaa aliniuliza "Vipi mwanangu upigi mambo yetu"?,Nkamwambia "Hapana kaka",Jamaa akanambia "inaonekana kijana ushakuwa mlokole,yaani na ukorofi na utundu wote ule wa shule ya Msingi hupigi huang'unywa?,Neno HUANG'UNYWA hapa alimaanisha pombe,maana ndizo lugha tulizokuwa tunazitumia kipindi hiko tukiwa wadogo!
Nkamwambia "Sipigi kaka"!

Basi stori za hapa na pale ziliendelea tukiendelea kukumbushana jamaa na marafiki tuliosoma nao,Baada ya kumaliza kula mi ilibidi nimuulize jamaa siku hizi anapiga ishu gani!,maana alikuwa kanawili na ukiangalia mimi nilikuwa nimechoka!

Basi jamaa alinambia yeye anajihusisha na mambo ya madini ila akasema isingekuwa vyema tuongee leo pale ila alinambia nijitahidi niende geita ndani ya siku chache nkamwone wife wake pamoja na mtoto wao pia nipate experience ya maisha ya kule yakoje!.
Basi baada ya hapo jamaa akanipa kama elfu 30000/= ,mi nkamuaga ila nilimwambia sina hata simu,alinambia nisiwaze nijatahidi nitafute siku niende huko geita kwani angesababisha hayo yote!,Basi baada ya maongezi nilimuaga jamaa lakini ilibidi anipakie kwenye gari yake na kanipa escoti mpaka mabatini then mi nkachukua daladala za kuelekea Nyegezi nyumbani!

Kiukweli ile elfu 30000/=niliona kama kanipa milioni ukizingatia nilikuwa nimepigika kinoma!,Pia nilikuwa nawaza sana,Inawezekanaje mtu niliyemzidi kila kitu kuanzia Akili,elimu mpaka maisha enzi hizo leo Anizidi maisha?,Niliumia sana lakini sikuwa nala kufanya!,Sasa pale nyumbani kuna vi-hela nilikuwa nimesevu,hivyo nkachukua na hii jamaa ambayo alinipa nkajumlisha ikawa ya kutosha japo si haba!
Basi kesho yake ilibidi niingie kwenye mitumba kusaka pamba za kuzugia kitaa!

Nilipata kama suruali mbili nkanunua na makobazi pamoja na sweta!

Baada ya kama wiki nilianza kuwaza namna ya kwenda geita ili nkaonane na jamaa maana niliona kama nimechelewa sana!,Jamaa kipindi tupo hotelini kule alinipa direction nkifika pale Katoro na kuna jina alinitajia ambalo ni maarufu nkifika pale hata watoto wangenipeleka kwake!,lile jina lake la shule ya Msingi alinambia kule hakuna anayelifahamu bali limebaki kwenye vyeti tu!

Itaendelea................
@Moderator Fang Invisible

Mods kwanini hamuweki links za story kwenye post ya awali? Yani msomaji anatakiwa asumbuke kutafuta mwendelezo mpaka aupate kweli? Be serious mods!!
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 3

Inaendelea.............

Nilisikia honi ya gari ikipiga kwa nje ya nyumba hivyo nilifahamu atakuwa ndo jamaa karudi!,Kweli alikuwa ni jamaa ndo kafika na kiukweli alionekana kunichangamkia sana na bila kupoteza muda alinitambulisha kwamba yule ndo Mke wake na yule Binti alikuwa ni mdogo wa huyo mkewe!
Alinambia pia wanao watoto wawili mabinti na kwa wakati ule mimi sikuwaona pale kumbe baada ya kutoka shule vilikuwa vimelala!

Basi mazungumzo ya hapa na pale yaliendelea na jamaa akawa ananielezea namna yeye baada ya maisha kule Tarime kuwa magumu aliamua kutokomea Huko Geita ambako aliitwa na rafiki yake!,Kwahiyo baada ya mapambano ndo kama ninavyomuona alivyo!
Mkewe baada ya kumwambia mimi ni msukuma alinambia "Kumbe wewe ni wakwetu kabisa",Kumbuka jamaa yeye alikuwa mkurya!

Baada ya kupiga msosi wa usiku niliona kama ile nyumba imechangamka tofauti na Mwanzo maana jamaa kama kawaida yake akaanza kupiga HUANG'UNYWA na mimi kama kawa nkakamata soda!,Basi yule wife wake akawa ananishangaa mimi kunywa soda wakati wao wakipombeka!,Nilimwambia sikuwahi kunywa Bia ila katika maisha yangu yote na alishangaa sana!,Baada ya kuburudika sana usiku ule na stori za hapa na pale jamaa alimwambia mkewe aende akaniandalie chumba,ndipo mkewe alimwita yule mdogo wake akamwambia nenda kaandae chumba cha mgeni!,Yule dogo alisema "Kipo tayari dada".
Baada ya muda nilimwambia Jamaa basi mi nadhani nkapumzike,ndipo jamaa alinambia kesho asubuhi tutaondoka wote kuelekea geita akanionyeshe kazi zake kule nami nilimkubalia ukizingatia nilienda kule ili kama ingepatikana kazi yeyote niruke nayo!maana maisha ya jamaa tayari yalishanichanganya akili!

Basi niliingia chumba cha wageni ambacho kilikuwa ni self contained na kabla ya kulala nkaona kwanza nkapige maji!,Kiukweli sikuwa na nguo za ziada maana nilienda tu kama nilivyo vaa tena nguo zenyewe ni zile nilizonunua mtumbani nikiwa Mwanza!,

Asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa jamaa alinichukua na safari ya Geita ikaanza,Jamaa alikuwa akimiliki enzi hizo harrier old model na hiyo ilikuwa miaka ya 2010,Kiukweli jamaa niliona kama kayapatia sana maisha!,Tukiwa ndani ya gari mastori ya hapa na pale yaliendelea na akisimulia namna alivyompata huyo Mkewe mpaka wakaoana!
Tulivyofika pale Geita jamaa alipaki gari mahala fulani hivi na akanambia "nisubiri kidogo nakuja",Alikuwa akiingia kuna duka moja la vifaa vya ujenzi na ilimchukua kama dakika 10 akawa amerejea!,Jamaa akawa ananiambia lile duka nila kwake na mara nyingi huwa anashinda hapo kama akiwahi kutoka huko kazini kwake tulipokuwa tukielekea!
Tulikuwa tukielekea nje ya mji wa Geita na njia tulitumia ilikuwa kama tunarudi Mwanza,baada ya kusonga kwa umbali mrefu hatimaye tuliikamata barabara ya vumbi kuelekea kwa ndani ndani huko!,Baada ya muda wa kama dakika 45 tulifika hapo kazini kwake!

Kiukweli lile eneo lilikuwa kubwa kiasi na kulikuwa na watu wengi kiasi na palikuwa pamechangamka!,Jamaa akanambia hapa ni ndipo mahali pangu pa kazi na akaanza kunitembeza na kunionyesha namna watu wanavyofanya kazi!

Baadaye nilikuja kuelewa ya kwamba jamaa anafanya ishu za uchenjuaji wa udongo wa dhahabu,wao kule walikuwa wanaita "MARUDIO",Haya marudio ni ule udongo ambao migodi mbali huwa wameshauondoa dhahabu,sasa yeye kumbe alikuwa akiununua na anafanya kazi ya kuuozesha kwenye mashimo then anaufanyia process unatoa dhahabu!,na pale tulipofika kumbe ndo ilikuwa kambi ya huo udongo maana ulikuwa umerundikwa mwingi umetengeneza kama mlima!,Kiukweli jamaa alikuwa vizuri maana hapo kambini alikuwa kajenga nyumba fulani hivi za mabati ambazo hao wafanyakazi wake walikuwa wakiishi hapo!

Basi baada ya jamaa kuwa amenizungusha hapo nilimwambia aniajiri hapo nami nianze kupiga kazi maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha!,Jamaa aliniambia kama naweza kweli kufanya kazi twende kwanza nyumbani halafu kesho tutarudi wote!,Basi nilimwambia jamaa kwamba sikuwa na nguo akanambia wala nisijali!
Tulirudi pale geita nakumbuka tuliingia dukani jamaa akaninunulia jinsi mbili na mashati mawili!,akaninunulia na wanchoma(four angle) moja matata!,Kiukweli nilijiona kama mtu niliyeyapatia maisha kwa wakati huo kumbe nilikuwa msindikizaji!,Tuliingia duka moja walikuwa wakiuza visimu fulani hivi vilikuwa vya promosheni vya zain (Airtel),na mbele ya kioo kwa juu vilikuwa vimendikwa Zain,Basi jamaa alininunulia na nkasajili na laini ya Zain maana kasimu kalikuwa kanatumia laini ya zain tu!,kiukweli nilimshukuru sana Jamaa !

Kweli kesho yake ilibidi nimuage pale shemeji nkamwambia mi ngoja nkapambane na siku si nyingi tungeonana!

Tulielekea huko porini kama kawaida na baada ya kufika jamaa alinambia kwa kuwa sina uzoefu ataniweka niwe kama kibarua ili niendelee kujifunza!,Ndani ya hiyo kambi kulikuwa na watu walioajiriwa rasmi kama 4,Hao walikuwa wakiendesha mitambo ya jamaa hapo na shughuli zilizohitaji uzoefu lakini vibarua wengine ikiwemo mimi kazi yetu ilikuwa ni kupiga chepe kwenye udongo na kupangiwa shifti ya kuzungukia kwenye maduara ya kuozeshea udongo ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa!,Wale jamaa 4 walikuwa wakilipwa mishahara rasmi na sisi vibarua ilitegemea kama dhahabu ingepatikana tulikuwa tunalipwa posho tu!

Basi bhana baada ya jamaa kuwa ameondoka alinikabidhi kwa jamaa mmoja tulikuwa tukimuita Bonge ambaye alikuwa mmoja wa wale jamaa 4,Tulikuwa tukipiga stori za hapa na pale na yule Bonge!
Ilipofika mchana jamaa Alisema twende tukale maana ugali wa pale ni kama wa gerezani,ukiukosa muda huo wa Jioni ndo mpaka kesho yake!
Japo nilienda kutafuta maisha lakini kiukweli hali ya pale ilianza kunitisha!,Maana ugali wenyewe ulokuwa umepikwa ni hatari,Siunajua tena ugali wa masela unavyoga kuwa!,Walipiga na dagaa bila kuungwa nyanya na mchuzi ndo kama woote yani!,Yaani kiukweli nilikula tu ili isije ikaonekana nina dharau!

Basi ilibidi nizoee ile hali maana sikuwa na namna,nakumbuka kila baada ya siku 7 walikuwa wanafanya kazi ya uchenjuaji kwa baadhi ya mashimo na dhahabu ilikuwa inapatikana na kwa wakati huo aliyekuwa akitulipa ni yule bonge,Pesa yangu ya kwanza kupata kwa kipindi kile ilikuwa kama laki moja na themanini(180000/=),Nilifurahi sana maana ndo ilikuwa hela kubwa kuanza kuikamata hiyo miaka ya 2010,Basi baada ya siku kadhaa nilipokuwa mzoefu wa ile kazi na kupata marafiki pale!

Siku moja nakumbuka kuna jamaa miongoni mwa wale vibarua tuliokuwa pale na tulikuwa tushazoena alikuwa akipiga story na mimi akawa anaieleza kwamba Jamaa ile kambi si ya kwake bali kuna mtu anakuwa anamwangalizia tu!,Ilibidi nimuulize tena jamaa mara mbilimbili!Jamaa akawa anasisitiza kwamba yule jamaa ile kambi si yake,yeye pale anakuwa anazuga tu!,,Jamaa akanambia yule jamaa hakuna hapo asiyemfahamu kwani ni Jambazi mkubwa!
Kiukweli mimi mara ya Kwanza nilikataa sana na sikukubali ila jamaa akanisihi nisimwambie mtu maana watu wengi pale hawafahamu ila anayefahamu ni yule Jamaa Bonge,wengine wote hawafahamu chochote!,Jamaa akawa ananiambia mwenye Mgodi yupo Mwanza na huwa anakuja mara moja moja kwa maana sehemu kama hizo anazo za kutosha hapo Geita!

Pia nilirejesha mawazo nyuma maana kuna maswali kadhaa jamaa niliwahi kumuuliza akawa anaishia nisiwe na wasiwasi!,Nikajiuliza pia yawezekana pia hata lile duka la vifaa vya ujenzi alilosema nila kwake yawezekana si lake!

Basi kweli kwakuwa nilikuwa nimezoeana na yule Bonge siku moja tukiwa maeneo ya jirani mi nkipata soda na Bonge akipiga Pombe ndo aliponieleza ukweli kwamba yule jamaa ni Jambazi na mara nyingi ishu zake yeye na wenzie wanaenda kupigia huko Mutukura kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania ila akasema kwa kuwa yeye alinambia toka mwanzo kwamba wewe ni ndugu yake nikajua utakuwa unaelewa!

Jamaa akanambia kwamba watu wote pale wanafahamu wewe ni ndugu yake!,Duuuu kiukweli kusikia vile niliishiwa nguvu maana sasa nkaona linaweza kutokea suala lolote lile nkajumlishwa na mimi wakati ndo hata sielewi chochote!

Siku hiyo ilibidi niweke vocha kwenye kile ki simu changu alichoninunulia jamaa nkawapigia nyumbani,kuna nyumba ya jirani huwa nawapigia halafu wanaenda kumwita Bi mkubwa naongea nae!,Basi walipomwita Bi mkubwa niliongea nae na nkamweleza kazi namna zilivyo na akanambia kuna mtoto wa Mama yetu mdogo kwao ni wilaya ya Bunda alikuwa amekuja kuniulizia pale nyumbani na alitaka kuna kazi imepatikana ya kutafuta kitu fulani hivi tukikipata tunapata mamilioni!
Ile taarifa ya Bi mkubwa ni kama ilinichanganya na nkamwambia ngoja niweke mambo sawa kesho naanza safari ya kurudi Mwanza!

Kesho asubuhi nilichukua mkoba wangu nkaweka nguo na nkamuaga Bonge na yule aliyekuwa msela wangu nkaondoka zangu kupanda gari nielekee Mwanza!,Kumbuka hapo siku zote yulee Jamaa yangu niliyeambiwa ni Jambazi sikuwahi kumuona tena toka aliponipeleka hapo kambini!

Nilipofika town nilikata zangu tiketi na safari ya kurejea Mwanza ikawa imeiva!

Itaendelea..................
Duuuh!!
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 12

Inaendelea.............

Tuliondoka Mwanza majira ya saa 12 Asubuhi,Ile njia mimi mwisho wangu ulikuwa katoro,Geita lakini kuelekea huko mbele sikuwahi kufika na hiyo ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza!,Mimi nilibeba kibegi kidogo nkaweka nguo za kubadilisha maana niliwaza yasije kunikuta yaliyonikuta hapo nyuma!
Jamaa yangu yule yeye alienda akiwa amevaa nguo alizokuwa nazo na uenda nikasema safari kama hizi yeye ni mzoefu!

Ile safari ilikuwa ndefu sana,Jamaa alinambia tukifika Kasulu sisi tutashuka maana baada ya kufika hapo Kasulu ingetubidi tuelekee kuna kijiji kimoja kinaitwa Munyegera!.
Ilituchukua masaa kama 9 hv au kumi mpaka kufika Kasulu mjini na kwakuwa bado ilikuwa mapema Jamaa aliniambia tutafute kwanza sehemu wanayouza chakula hapo Kasulu tule!

Baada ya kumaliza kupata chakula jamaa alinambia tutafute usafiri wa kuelekea huko kijijini Munyegera,Kwa kuwa mimi ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika hapo kasulu nilikuwa nikishangaa shangaa tu!

Hii nchi ni kubwà sana ndugu zangu sikuwahi kudhani kama ipo siku ningefika kigoma - kasulu!,Basi jamaa akaniambia inabidi tuchukue pale boda boda mpaka huko kijiji cha Munyegera!,Kwakuwa jamaa alikuwa mwenyeji mimi sikuwa na shaka yeyote!,
Tuliita boda mmoja akaja na jamaa alipoongea nae akakubali angetupeleka kwa 15000/=kwa wote wawili.
Tulianza safari sasa ya kuelekea huko Munyegera na ilituchukua kama saa moja na nusu hivi mpaka kufika hapo Munyegera!,Baada ya kufika tulimpa hela yake jamaa akaondoka zake na sisi kuianza safari ya kuelekea maporini!
Yule jamaa alinambia kutoka hapo Munyegera mpaka kwa huyo Mama(Mganga)si mbali hivyo tutembee!

Ilikuwa tayari ishaingia giza na sisi tuliendelea kuchanja mbuga!,Mfukoni mpaka kwa wakati huo mimi nilikuwa nina laki tatu,Jumla nilibeba kama laki tatu na 70000/=hivyo ukijumlisha nauli pamoja na mambo mengine humo njiani nilibaki kama na laki tatu!Sikutaka kupata shida kama niliyoipata hapo nyuma,Japo jamaa tukiwa Mwanza alinambia nitafute laki mbili lakini mimi nilijiongeza!

Basi baada ya kutembea kwa muda mrefu hatimaye tulifika hapo nyumbani kwa huyo Mama mganga na tulipokelewa na mabinti wawili waliokuwa pale!,Kuna watu tuliwakuta pale ilibidi nimuulize jamaa mwenyeji wangu akaniambia hao pia walikuwa pale wamefata tiba!,Akili yangu mara zote ninapokuwa ugenini ni mahali pa kulala!

Kwakuwa ilikuwa ishafika usiku tulikuta umekokwa moto na kuna raia wengine walikuwa wakiota moto pale huku wakiendelea kupiga story za hapa na pale kwa kiswahili chenye lafudhi ya Kiha!

Jamaa alinambia ngoja anaenda kumuona mama mganga kama yupo halafu anarudi,baada ya dakika kadhaa alirudi na kuniambia msaidizi wa yule mama kamwambia Hayupo na anarudi asubuhi hivyo hata hao watu tuliowakuta walikuwa wakimsubiri yeye!,Kwakuwa baridi ishaanza kuwa kali ilibidi mimi na jamaa tusogee kwenye moto pale na tulikaa hapo chini ya mkeka mpaka mimi usingizi ukanipitia!,Nimekuja kushituka bado ni usiku lakini bado jamaa wako macho wakipiga story,Usingizi ulikuwa ukichukua na kushituka,niliendelea na hiyo hali mpaka kulipo pambazuka!,Kuna jamaa pale yeye kazi yake ilikuwa ni kuongeza magogo tu kwenye ule moto kila ulipoonyesha hali ya kufifia!

Asubuhi kila mtu pale alikuwa na ishu zake na niliona kila mtu alikuwa kakaa na mtu ambaye walikuwa wakifahamiana naye!,Yule Mama mganga tuliambiwa karudi na nilijiuliza alirudi vp wakati usiku huo wote hakukuwa na mtu mwingine aliyeingia hapo nkakosa majibu!
Watu tuliowakuta hapo kila mtu alienda humo ndani kwenye nyumba ya mganga na kuelezwa walicho elezwa!,Kuna wengine walikuwa wakitoka wanaondoka jumla na kuna wengine walikuwa wakitoka wanarudi tena nje kukaa nadhani waliambiwa wasubiri!

Tulikaa kwa muda mrefu kidogo na zamu yetu ilipofika tuliitwa na Msaidizi wa yule mama!,Tuliambiwa tunaingia mmoja mmoja ndipo mimi nikamwambia yule jamaa aanze yeye!
Jamaa alikaa humo ndani kama nusu saa hivi halafu akatoka akanambia niende ndani!

Nilipofika ndani nilimsalimia Yule mama ambaye hakuwa Mzee sana kama nilivyofikiria na kabla sijaanza kuongea aliniambia ninyamaze maana maisha yangu yote toka tukiwa Tarime mpaka nimefika hapo kwake anayafahamu hivyo akaniambia nimwambie ninataka nini!,Kiukweli aliponiambia anayafahamu maisha yangu Tangu nikiwa Tarime nilishangaa kidogo!,

Hivyo ilibidi nimueleze kwamba ninataka kuwa tajiri,Aliniangalia akawa anatikisa kichwa tu ,kisha akaniambia "Mbona mwanangu umeharibiwa sana"!,Hauwezi kuwa tajiri mpaka usafishwe kisawa sawa!,akawa ananiambia kwamba nyota ya marehemu Baba ninayo mimi ila kuna kitu kipo hapo katikati kinachozuia ile nyota kung'aa ili niweze kuwa tajiri!

Akaniambia yeye atanisafisha na kunipa dawa ya kinga ili chochote kibaya kitakachonisogelea basi kiende na maji!, akaniambia baada ya kunisafisha itanipaswa niende mpaka kigoma nivuke ng'ambo ya pili upande wa kongo sehemu inaitwa Kalemii,huko kuna mtu ambaye angeniondolea huo mpaka hapo katikati hatimaye nyota ya Baba yangu niipate mimi,maana ilionekana kung'aa sana ila kuna mshenzi mmoja kaizuia na ndo maana ninateseka!

Kiukweli nilivuta pumzi sana maana nilijua nimemaliza kumbe ndo kwanza kazi haijaanza!,Aliniambia itanibidi nikae pale kwa siku tatu ili akimaliza kuwashughulikia wale wagonjwa wengine ndipo nianze dozi!

Nilipomaliza kuongea na yule mama ilibidi nitoke nje kuongea na yule jamaa aliyenipeka na akashangaa sana!,Jamaa akaniambia "Mwanangu jipe moyo,kwakuwa umeamua pasipo kulazimishwa we kuwa na uvumilivu"
Yule mama alitoka ndani na alikuwa akiongea na wateja wake pale nje na alipofika kwetu alimwambia jamaa huyu Mwenzio bado nina kazi naye!,We kama utamsubiri we msubiri maana bado anasafari nyingine!,Jamaa tuliongea nae na hakuwa na namna aliniambia ilibidi aondoke akawahi kazi zake lakini akaniambia mimi ni mwanaume nijipe moyo!,

Nilimwambia jamaa endapo sitorudi nyumbani kwa chochote ambacho kingenipata basi anichukulie vile vyombo vyangu anipelekee nyumbani kwetu,jamaa alikubali!,Aliniaga pale na akaniongezea laki moja tena ila nilimwambia nikirudi ningemrudishia!
Kwahiyo ukijumlisha kiasi jamaa alichonipa na nilichokuwa nacho nilikuwa kama na laki nne!,Wakati jamaa anaondoka nilijikuta nalia kama mtoto maana sasa nilijiona bado nina safari ndefu ukizingatia nilikuwa mgeni!

Nilijipa moyo sana maana niliona ningekata tamaa hakuna ambacho ningefanikisha!

Itaendelea..............
🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Back
Top Bottom