Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 13.


Inaendelea.............


Nilikaa pale kwa yule mama mganga kwa siku tano,maana siku mbili zilikuwa za kuwatibu wale wateja wake wengine tuliowakuta na ndipo zile siku tatu alizokuwa ameniahidi zilitimia!.Kiukweli nilioga sana dawa pamoja na kunywa nyingine,pia alinipiga chale sehemu mbalimbali za mwili wangu!.

Zile siku zilipotimia aliniambia niko vizuri kwa maana amenipiga kinga ambayo yeyote atakaye jipendekeza ni lazima aende na maji!.Akaniambia inapaswa niende Kongo sehemu moja inaitwa Kalemii na nikifika hapo Kalemii inapaswa nitafute tena usafiri unipeleke mpaka Mji/Kijiji kimoja kinaitwa Kirungu,nitakapofika hapo Kirungu nimuulizie mzee mmoja anaitwa Nchibaronda ambaye ni mganga maarufu na hakuna ambaye alikuwa amfahamu hapo kijini!,aliendelea kuniambia kwamba huyo mzee Nchibaronda yeye ndiye atakayenipa utajiri maana hakuna ambacho kingemshinda!,Kwakuwa nilikuwa bado mgeni na sikuyaelewa maeneo vizuri nilimuomba karatasi na kalamu ili niandike hiyo miji ya Kongo na lile jina la huyo mganga ili iwe rahisi mimi kukumbuka!.Kabla ya kuondoka nilijaribu kuwasiliana na yule jamaa tuliyeenda naye hapo Kasulu kwani nilitaka kufahamu yeye kule nyumbani Mwanza alikuwa anaendeleaje,bahati mbaya sikuweza kumpata maana mtandao ulikuwa wa shida huko maporini.

Yule mama kuna kitu alinipatia kilichokuwa kimefungwa kwa ustadi na ngozi kikiwa kimebanwa sana kama kijiti kidogo,akaniambia nikifika kwa huyo mganga mzee Nchibaronda nimpatie kwani hiyo ndiyo ilikuwa rufaa yangu ya kutoka hapo Kasulu kwenda huko kijijini Kirungu!.Nilimwambia yule mama ile njia tuliyokuja nayo nilikuwa siikumbuki,ndipo akanipa binti wa makamo tuliyemkuta pale,akamwambia anisindikize mpaka barabarani na ahakikishe nikipata usafiri ndipo arudi.Tuliondoka na yule binti akinisindikiza kuelekea barabarani,tulipofika hapo barabarani nilisubiri pikipiki ili nipande nielekee Kasulu mjini kuchukua gari za kwenda Kigoma.Baada ya muda bodaboda ilifika na tulikubaliana na yule jamaa nimpatie elfu 10 mpaka Kasulu mjini,yule binti nilimpatia elfu 5 kama shukurani ,wakati huo mfukoni nilikuwa nimebaki na laki tatu na elfu hamsini na tano(355000).Yule mama mganga alisema nimpatie elfu 30 tu ya dawa maana asingeniomba hela nyingi kwakuwa bado ndiyo nilikuwa naianza safari ya utafutaji.

Yule dereva bodaboda alijaribu kukimbia sana na kiukweli tuliwahi kufika Kasulu,ile njia niliiona ilikuwa fupi tofauti na siku ya kwanza!,niliingia Kasulu mida ya saa 7 mchana,moja kwa moja nilimwambia jamaa anipeleke stendi kuu ya kupandia magari ya kuelekea kigoma.Nilipofika hapo stendi kuna jamaa aliniwahi fasta alifahamu fika mimi nilikuwa msafiri,alianza kunitajia miji na vijiji ambavyo magari aliyokuwa akiyapigia debe yalikuwa yakielekea!.Mimi nilimwambia naelekea kigoma mjini,akaniambia nisubiri kidogo kuna gari itafika hapo muda si mrefu!,jamaa alikuwa shapu sana maana wakati nashangaa alikuwa tayari kachomoa kitabu cha tikiti mfukoni na kuanza kuandika pale!.Muda si mrefu gari ilifika na jamaa akasema tuongozane naye,nilipofika nilipewa siti nikakaa na safari ikaanza.Tulitumia kama saa 1:30 mpaka Kigoma na hiyo ilikuwa mida ya saa 10 alasiri.

Baada ya kuwa nimefika Kigoma nilitafuta mahala pa kula maana nilikuwa nikihisi njaa sana!.Baadae nilianza kuzunguka hapo mjini kuna jamaa nilikutana naye nikamwambia nahitaji kuelekea Kongo na anielekeze namna ya kufika,jamaa aliniuliza "Mshua unaelekea Kongo mahala gani?".

Nilimwambia "naelekea Kalemii".

Jamaa akaniuliza "Je,una pasipoti?".

Nilimjibu "hapana sina pasipoti".

Basi jamaa akaanza kuniambia kwamba kwenda Kongo hapo Kalemii kuna njia tatu,Ya kwanza ni kupitia Burundi kwa njia ya Bus na inapaswa niwe na pasipoti,njia ya pili ni kupitia angani kwa njia ya ndege na njia ya tatu ni kupitia majini,lakini pia lazima niwe na pasipoti.

Jamaa akaniuliza "Wewe upo tayari kupitia njia gani?"

Yule jamaa ilionekana Kongo alikuwa akipaelewa sana maana alikuwa mjanja mjanja sana!

Mimi nilimwambia "Nataka wewe ndiyo uwe mwenyeji wangu,nahitaji msaada wako".

Jamaa aliniambia "Usijali mshua hapa umefika".

Basi jamaa akaniambia "twende zetu!".

Jamaa alinichukua pale tukawa tunaelekea maeneo ya Ziwa Tanganyika,tulipofika hayo maeneo ya ziwani ilikuwa mbali na bandarini akaniambia ngoja kuna jamaa hawa huwa wanaelekea Kongo kwa njia za panya ziwani nikuitie uongee naye!.Alimuita jamaa mmoja aliyekuwa pale na akamueleza namna hali ilivyokuwa.

Yule jamaa akaniuliza "Mkuu una shilingi ngapi?".

Kwa wakati huo mimi sikufahamu nauli ni kiasi gani!,Nilimwambia wewe niambie unataka shilingi ngapi?,jamaa akasema nitampatia elfu 15,ila akaniambia wao wanaelekea sehemu moja inaitwa Kabanga,akaniambia kutoka hapo Kabanga mpaka Kalemii haikuwa mbali,kuna maboti yapo ya kutosha yangenipeleka!.Nilikuwa sina namna ilibidi iwe hivyo maana nilishaamua,jamaa akaniambia tutaondoka hapo kigoma usiku wa saa 2 kuelekea huko Kabanga,hivyo nijiandae niwe maeneo ya jirani,nilitoa elfu 15 nikampatia jamaa nikamwambia tutarudi muda si mrefu!.Yule mwamba niliyekutana naye hapo Kigoma akaniambia kama nina hela niende nikabadilishe ili nipate faranga za Kongo ili iwe vyepesi kuitumia nitakavyo kuwa huko,jamaa alinipeleka mahala fulani nikawakuta jamaa fulani walikuwa wanapesa nyingi sana ambazo walikuwa wanabadilisha,nilitoa laki moja ya Tanzania nikabadilishiwa nikapata faranga ya Kongo elfu 85.

Nilimwambia jamaa tuelekee maeneo ya mjini nitafute angalau mashuka mazito ya kimasai ili linisaidie kwenye safari!.Kuna mahali jamaa alinipeleka nikanunua kitenge kimoja kilichokuwa kizito mithili ya shuka na nikalipa kama elfu 15,yule jamaa ikabidi nimpe na yeye elfu 15 kama shukurani kwasababu alinisaidia sana,hivyo kwa wakati ule nilibaki na laki mbili na elfu mbili (202000) bila kusahau ile ya faranga 85000 pia nilikuwa nayo.Nilimwambia jamaa tutafute maeneo tukae tupumzike kidogo ili masaa yakikaribia anirudishe kule ziwani halafu yeye aendelee na mitikasi yake.Tulipiga sana stori na yule mwamba na nilipata sana uzoefu,nilijua uenda labda nilikuwa nimeshahangaika kwenye haya maisha lakini baada ya mwamba kunisimulia uzoefu wa maisha yake nikajiona bado cha mtoto,uzoefu wa maisha yake aliyonisimulia ulinipa morali ya kufanya zaidi.Ilipofika saa 12 jioni nilimwambia jamaa anirudishe Ziwani kwa wale jamaa maana muda haukuwa mbali sana,basi nilipofika hapo ziwani niliagana na yule mwamba,nilikaa jirani na lile boti,ingawa halikuwa boti,lilikuwa kama jahazi au Mashua fulani hivi,ilikuwa ngumu mimi kulitofautisha kwasababu sikuwahi kufahamu huo usafiri wa majini na aina zake.Nilijaribu kumtafuta kwenye simu yule jamaa wa Mwanza na nilifanikiwa kumpata,tuliongea mambo mengi sana,jamaa alinipa moyo akaniambia nikomae sana!,Kwa muda wote huo sikutaka kabisa kumpigia mama yangu simu na mara nyingi nilikuwa nazima simu ili hata akinitafuta nisipatikane kirahisi.

Muda wa kuondoka ulipofika jamaa aliniambia nipande kwenye lile jahazi kwa ajili ya safari!,mle ndani ya Jahazi walikuwa wamebeba madumu mengi yaliyokuwa yakinuka harufu ya petroli hivyo sikuwa na shaka kwamba ile ilikuwa ni petroli iliyokuwa ikisafirishwa,pia kulikuwa na magunia na viroba vya unga na mchele!,Kiukweli lile Jahazi lilikuwa limesheheni mzigo.Ngoma ikang'oa nanga na ikaanza kupepea kuelekea ziwani!,Kiukweli sikuwahi kusafiri kwa umbali mrefu sana ziwani na ile ndiyo ilikuwa mara ya kwanza,nilikuwa nikiogopa sana hasa ukizingatia hapo zamani tulikuwa tukisimuliwa kuhusu Ziwa Tanganyika na Kigoma kwa ujumla mambo ambayo yalikuwa mabaya naya kutisha tu!.Kwasababu mimi ndiye nilikuwa nimeamua sikulazimishwa na mtu yeyote,ilibidi nijikaze kisabuni.Chombo iliendelea kupepea na baridi ilianza kuwa kali sana,nikatoa zangu kitenge nilichokuwa nimekinunua masaa machache yaliyopita nikajifunika.Tulitembea ziwani kwa umbali mrefu na nilimuuliza jamaa ingetuchukua siku ngapi hadi kufika hapo Kibanga,jamaa aliniambia kwamba usiku huo huo walipaswa kufika Kabanga maana asubuhi walitakiwa kurudi Kigoma!.

Baada ya muda mrefu tukaingia hapo Kabanga mida ya saa 7 usiku!.Jamaa akanishtua maana nilikuwa nimepitiwa na usingizi,niliwasha simu kuangalia muda ilikuwa saa 7 usiku.

Nikamwambia jamaa "mimi hapa ni mgeni usiku huu nitaenda wapi?".

Yule jamaa aliniambia "Usiwe na shaka wewe jiegeshe humu ndani maana wanapakua mizigo na watamaliza asubuhi saa 12 kutakuwa kushakucha".

Jamaa akaendelea kuniambia "Kukisha kucha nitakuonyesha boti zinazoenda Kalemii".

Niliuchapa usingizi mle ndani mpaka asubuhi,nilipoangalia saa ilikuwa saa 1 asubuhi,nilimfata jamaa nikamwambia anionyeshe boti zinazoelekea Kalemii.Jamaa alinichukua akanisogeza mbele kidogo kuna jamaa alimkuta pale akamwambia "Aisee abiria huyu hapa anaelekea Kalemii".

Jamaa akaniambia "boti za kalemii ni hizi hapa hivyo wewe kaa hapa maana nimeshamwambia huyo jamaa mtaelewana!"

Yule jamaa wa boti za Kalemii alinisogelea akaniuliza "Kaka unaelekea Kalemii?".

Nilimjibu "Ndiyo".

Jamaa alikuwa akiongea kiswahili fulani hivi chenye rafudhi ya lingala,jamaa akaniambia ya kuelekea Kalemii ni faranga elfu 4 ambazo kwa pesa ya Tanzania ilikuwa kama elfu 5,Kuna mizigo walikuwa wakipakia pale na jamaa alisema wakimaliza kupakia hiyo mizigo wanaondoka.Basi nilisogea kidogo hapo ziwani nikawa nina nawa uso na kushangaa ziwa Tanganyika namna lilivyokuwa kubwa!.

Baadae walipomaliza kupakia mizigo tuliondoka kuelekea Kalemii na hiyo ilikuwa saa 4 asubuhi.


Itaendelea.................
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 13


Inaendelea.............


Nilikaa pale kwa yule mama mganga kwa siku kama tano,maana siku mbili zilikuwa za kuwatibu wale wateja wake wengine tuliowakuta na ndipo zile siku tatu alizokuwa ameniahidi zilitimia!
Kiukweli nilioga sana dawa pamoja na kunywa nyingine,pia alinipiga chale sehemu mbalimbali za mwili wangu!

Zile siku zilipotimia aliniambia sasa niko vizuri kwa maana amenipiga kinga ambayo yeyote anatakaye jipendekeza ni lazima aende na maji!
Basi akaniambia inapaswa niende kongo Sehemu moja inaitwa KALEMII na nkifika hapo Kalemii inapaswa nitafute tena usafiri unipeleke mpaka Mji/Kijiji kimoja kinaitwa KIRUNGU na ntakapofika hapo basi nimuulizie mtu mmoja hapo anaitwa NCHABIRONDA kwani ni mganga maarafu na ntapelekwa mpaka kwake!,Alinambia huyu yeye ndo atakayenipa utajiri maana hakuna kitakacho mshinda!,Kwakuwa nilikuwa bado mgeni na sikuyaelewa maeneo vizuri nilimuomba karatasi na kalamu niandike hiyo miji ya Kongo na Jina la huyo mganga ili iwe rahisi mimi kukumbuka!
Kabla ya kuondoka nilijaribu kuwasiliana na yule jamaa tuliyeenda nae hapo kasulu kwani nilitaka kufahamu yeye kule nyumbanj Mwanza anaendeleaje,Bahati mbaya sikuweza kumpata maana mtandao ulikuwa wa shida!

Yule mama kuna kitu kama ki-Ngozi kikiwa kimebanwa sana kama kijiti kidogo hivi,Akanambia nikifika kwa huyo Mganga nimpatie kwani hiyo ndo kama rufaa yangu ya kutoka hapo kasulu kwenda Huko kijijini Kirungu!
Nilimwambia yule mama ile njia tuliokuja nayo kiukweli siikumbuki na akanipa Binti wa makamo mmoja aliyekuwa pale akamwambia anisindikize mpaka barabarani ntakapo pata pikipiki!

Tuliondoka na yule binti pale huku tukipiga story za hapa na pale na tulipofika hapo barabarani nilisubiri pikipiki pale ili nipande nielekee kasulu kuchukua gari za kwenda kigoma!
Baada ya muda bodaboda ilifika na tulikubaliana na yule jamaa nimpatie 10000 mpaka kasulu mijini,yule Binti nilimpatia 5000 ,Mpaka wakati huo mfukoni nilikuwa nimebaki na 355000/=Yule mama mganga alisema nimpatie 30000 tu ya dawa maana asingeniomba hela nyingi kwakuwa bado ndo naaza safari ya utafutaji!

Boda alijaribu kutembea sana na kiukweli tuliwahi kufika kasulu,Ile njia niliiona imekuwa fupi tofauti na siku ya kwanza!,Niliingia kasulu mida ya saa saba mchana na moja kwa moja nilimwambia jamaa anipeleke stendi!
Nilipofika hapo stendi kuna jamaa aliniwahi fasta alifahamu fika mimi ni msafiri,Alianza kunitajia pale miji na vijiji ambavyo magari aliyokuwa akiyapigia debe yanaelekea!
Mi nilimwambia naelekea kigoma mjini,Basi akanambia nisubiri kidogo kuna gari itafika hapo muda si mrefu!,Jamaa alikuwa shapu sana maana ile nashangaa pale alikuwa tayari kachomoa kitabu cha tiketi mfukoni na kuanza kuandika pale!,Nilimpa kama 8000/=

Muda si mrefu gari lilifika na jamaa akasema tuongozane nae na nilipofika nilipewa siti nkaa na safari ikaanza!
Tulitumia kama saa 1 na nusu mpaka tunaingia kigoma na hiyo ilikuwa mida ya saa 10 Alasiri!
Baada ya kuwa nimefika kigoma nilitafuta mahala pa kula maana nilikuwa nikihisi njaa sana!

Baadae nilianza kuzunguka hapo mijini na kuna jamaa nilikutana nae nkamuuliza nahitaji kuelekea Kongo na anielekeze namna ya kufika!,Jamaa aliniuliza "Mshua unaelekea Kongo mahala gani"?,Nilimwambia naelekea "Kalemii"
Jamaa akaniuliza "Je,unapasipoti"?
Nilimjibu "hapana sina pasipoti"

Basi jamaa akaanza kuniambia Kwenda Kongo hapo Kalemie kuna njia tatu,Ya kwanza ni kupitia Burundi kwa njia ya Basi na inapaswa niwe na pasipoti,Njia ya pili ni kupitia angani kwa njia ya ndege na njia ya tatu ni kupitia majini pale Bandarini lakini pia lazima niwe na pasipoti,Jamaa akaniambia "Wewe upo tayari kupitia njia gani"?
Yule jamaa inaonekana hata Kongo alikuwa akipaelewa sana maana alikuwa mjanja mjanja sana!,Mi nilimwambia "Nataka weww ndo uwe mwenyeji wangu na nahitaji msaada wako"
Jamaa aliniambia "Usijali Mshua hapa umefika"

Basi jamaa akaniambia twende zetu!,Jamaa alinichukua pale tukawa tunaelekea maeneo ya Ziwa Tanganyika na tulipofika hayo maeneo ya ziwani ilikuwa mbali na bandarini akaniambia ngoja kuna jamaa hawa huwa wanaelekea Kongo kwa njia za panya ziwani nikuitie uongee nae!
Alimwita jamaa mmoja aliyekuwa pale na akamweleza namna hali ilivyo,yule jamaa akaniuliza "Mkuu una shilingi ngapi"?,Kwa wakati huo mimi sikufahamu nauli ni kiasi gani!,Nilimuuliza weww niambie unataka sh ngapi?,Jamaa akasema ntampa 15000/= Ila akaniambia wao wanaelekea sehemu moja inaitwa "KABANGA" na akaniambia kutoka hapo Kabanga mpaka kalemie siyo mbali kuna Maboti yapo ya kutosha yatanipeleka!
Nilikuwa sina namna,Jamaa akaniambia tutaondoka hapo kigoma Usiku wa saa 2 kuelekea Huko Kabanga hivyo nijiandae na niwe maeneo ya jirani!,nilitoa 15000/= nikampa jamaa nikamwambia tutarudi muda si mrefu!

Mwamba niliyekutana nae hapo Kigoma akaniambia kama nina hela niende nikabadilishe ili nipate faranga za kongo ili iwe vyepesi ntakavyo kuwa huko!,Mpaka hapo mfukoni nilibakiwa na 332000/=,Jamaa alinipeleka mahala fulani nkawakuta jamaa wanapesa nyingi wakawa wanabadilisha pale,nilitoa laki moja ya Tanzania nikabadilishiwa nikapata kama 85000/=Faranga ya Kongo!,Hivyo nikabakiwa kama na 232000 ya kitanzania na 85000 faranga!

Nilimwambia jamaa tuelekee maeneo ya Mjini nitafute angalau yale Mashuka mazito ya kimasai ili linisaidie kwenye safari!
Kuna mahali jamaa alinipeleka nikanunua kitenge kimoja kilichokuwa kizito mithili ya shuka na nkalipa kama 15000/= na jamaa ikabidi nimpe 15000 maana alinisaidia sana!,Hivyo kwa wakati ule nilibaki kama na 202000 jumlisha ile ya faranga 85000!.
Nilimwambia jamaa tutafute maeneo tukae tupumzike kidogo ili masaa yakikaribia anirudishe kule ziwani halafu yeye aendele na mitikasi yake,Tulipiga sana story na yule Mwamba na nilipata sana uzoefu maana nilijua kwamba nimeshahangaika kwenye haya maisha lakini baada ya mwamba kunisimulia experience ya maisha yake nkajiona bado cha mtoto,hivyo kama ilinipa morali ya kufanya zaidi!

Ilipofika saa 12 jioni nilimwambia jamaa twende Ziwani kwa wale jamaa maana muda hauko mbali sana!,Basi nilipofika hapo ziwani niliagana na yule Mwamba na nikaa jirani na lile Boti,halikuwa Boti bali kama jahazi fulani hivi!
Nilimpigia simu yule jamaa wa Mwanza na nilimpata na tuliongea mambo mengi sana,Jamaa alinipa moyo akaniambia nikomae sana!,Kwa muda wote huo sikutaka kabisa kumpigia Bi mkubwa na mara nyingi nilikuwa nazima simu ili hata akinitafuta nisipatikane kirahisi!
Muda wa kuondoka ulipofika jamaa aliniambia nipande kwenye jahazi kwa ajili ya safari!,Mle ndani ya Jahazi walikuwa wamebeba madumu mengi na yalinuka halufu ya petroli hivyo sikuwa na shaka kwamba ile ilikuwa ni petrol ilikuwa ikisafirishwa,pia kulikuwa na magunia na viroba vya unga na mchele!,Kiukweli lile jahazi lilikuwa limesheheni mzigo!
Ngoma ikang"oa nanga na ikaanza kupepea kuelekea ziwani!,Kiukweli sikuwahi kusafiri kwa umbali mrefu sana ziwani na ile ndo ilikuwa mara ya kwanza!,Nilikuwa nikiogopa sana hasa ukizingatia hapo zamani tulikuwa tukisimuliwa kuhusu ziwa Tanganyika na Kigoma kwa ujumla wake mambo ambayo yalikuwa mabaya tu!

Nilikuwa nikijisemea kwamba "NILIZALIWA SIKU MOJA NA NTAKUFA SIKU MOJA"

Chombo iliendelea kupepea na baridi ilianza kuwa kali kidogo nikatoa zangu kitenge nilichokuwa nimekinunua masaa machache yaliyopita nkajifunika!
Tulitembea sana ziwani kwa umbali mrefu na nilimuuliza jamaa itatuchukua siku ngapi kufika hapo Kibanga,Jamaa aliniambia kwamba usiku huo huo wanaingia kabanga maana asububi wanapaswa kugeuza Kigoma!

Basi tuliyakata maji na tuliingia hapo kabanga mida ya saa 7 usiku!
Jamaa akanishtua maana nilikuwa nimepitiwa na usingizi kidogo,"Mwanangu tushafika",Niliwasha simu kuangalia muda ilikuwa saa 7 usiku,Nakamwambia mimi hapa ni Mgeni usiku huu ntaenda wapi?
Yule jamaa aliniambia "Usiwe na shaka wewe jiegeshe humu ndani maana wanapakua mizigo na watamaliza Asubuhi 12 kutakuwa kushakucha",Jamaa akaendelea kuniambia "Kukisha kucha nitakuonyesha Boti zinazoenda kalemii ",nkamwambia "Poa"

Niliuchapa usingizi mle ndani mpaka asubuhi nilipoangalia saa ilikuwa kama 1 asubuhi,nilimfata jamaa nikamwambia anionyeshe Boti zinazoelekea kalemii!

Jamaa alinichukua akanisogeza mbele kidogo na kuna jamaa alimkuta pale akamwambia "Aisee abiria huyu hapa anaenda kalemie",Jamaa akaniambia boti za kalemii ni hizi hapa hivyo we kaa hapa maana nimeshamwambia huyo jamaa mtaelewana!

Yule jamaa wa boti za kalemii alinisogelea pale na akaniuliza "Kaka unaelekea kalemii",Nilimjibu "Ndiyo",Jamaa alikuwa akiongea kiswahili fulani hivi chenye radha ya kikongo ndani yake!,Jamaa akanimbia nauli ni Faranga 4000 ambazo kwa pesa ya Tanzania ilikuwa kama 5000 hv,Hivyo mfukoni nilibaki kama na Faranga 81000/=
Kuna mizigo walikuwa wakipakia pale na jamaa alisema wakimaliza kupakia hiyo mizigo wanaondoka!

Basi nilisogea kidogo hapo ziwani nikawa nina nawa uso na kushangaa ziwa Tanganyika namna lilivyokuwa kubwa!

Baadae walipomaliza kupakia mizigo tuliondoka sasa kuelekea kalemii na hiyo ilikuwa kama saa 4 asubuhi!


Itaendelea.................
Duh mwamba bado unausaka tu utajiri kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom