Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 14

Inaendelea.............

Tuliendelea na safari kwa muda mrefu na kwakuwa ilikuwa mchana niliendelea kulishangaa ziwa Tanganyika namna lilivyokubwa na kwa upande wa Kongo kiukweli kulikuwa na misitu mikubwa sana!
Ile nchi ya Kongo ilibarikiwa sana kuwa na uoto wa Asili na kijani kibichi!

Kwenye lile boti kulikuwa na vijana 5 lakini mmoja wao ambaye ndiye niliyemlipa kile kiasi cha fedha ilionekana kama ndiye Bosi wa ile Boti,Ile boti ilikuwa ni boti fulani tu la mbao lakini lilikuwa limepachikwa injini lakini ilikuwa kubwa!,Nilimuuliza jamaa itatuchukua muda gani mpaka kalemii,Jamaa akanambia kama masaa 3!
Basi kweli,baada ya Masaa 3 tulikuwa tumefika kalemii!,Kiukweli ule mji wa kalemii ulikuwa mkubwa sana kama vile kigoma tu!,

Kwakuwa mimi safari yangu haikuishia pale nilimuuliza jamaa aniambie namna ya kufika kwenye kijiji cha Kirungu!,Jamaa alishangaa sana "Kirungu unaenda kufanya nini"?
Nilimwambia kuna shughuli inanipeleka kule!
Jamaa alinambia Kijiji cha kirungu kiko mbali kutoka hapo kalemii na endapo nikitumia Usafiri wa pkpk itanighraimu pesa nyingi,pia kupita maporini huko kuna uwezekano kukutana na waasi wakanifanya kitu mbaya !

Yale maeneo tuliyokuwa tumetia nanga yalikuwa nje kidogo ya Bandari ya kalemii kwasababu inaonekana wale jamaa walikuwa wanafanya Biashara za magumashi hivyo walikwepa mkono wa serikali!
Jamaa aliniambia hiyo kirungu ipo kusini mwa Kalemii hivyo ningepaswa kutumia njia ya maji ili iwe rahisi mimi kufika huko!,Jamaa aliendelea kunipatia maelekezo pale kwamba Kabla ya kufika Kirungu kuna Bandari bubu inaitwa Moba,sasa nikishafika hapo Moba nitatafuta bodaboda za kunipeleka Kirungu maana ukitoka hapo Moba kwenda Kirungu si mbali!

Aliniambia sasa hapo Kalemii itabidi nikutafutie bodaboda akupeleke ng'ambo ya pili kuukwepa mji halafu kuna njia ya kurudi tena ziwani kwa ng'ambo ya kusini!,Utakapofika huko lazima utazikuta boti za kwenda Moba,na ukifika Moba ni kama umefika Kirungu!

Basi nilishuka pale nikatafuta Boda maeneo yale na nilimpo mpata nilimwambia jamaa amwelekeze namna nilivyo mwambia!,Yule jamaa alimwambia "Mpeleke huyu jamaa kwenye Boti za kwenda Moba",Yule Boda aliniambia nimpe faranga 3000!
Tuliondoka zetu kupita mitaani ambako alikuelewa yeye,Ule mji ulikuwa umechangamka sana nami kawa kawaida niliendelea kushangaa mitaa hiyo ya kalemii,Baada ya muda si mrefu jamaa alifika maeneo ya ziwani kwa upande wa kusini!,alielekeza kulikuwa kuna maboti ya mbao kibao yamepaki pembeni mwa ziwa!

Niliachana na yule jamaa wa Boda boda pale mi nkaelekea kutafuta usafiri wa boti unaoelekea huko Moba!
Kuna jamaa mmoja nilimkuta pale anafuma nyavu za samaki na nikamsalimia!,Jamaa alionekana kama kiswahili anakijua vyema na nilimuomba anielekeze wapi ambapo ningepata usafiri wa kwenda Moba!
Jamaa aliniambia mara nyingi usafiri wa kwenda Moba unategemeana na mizigo ya kwenda huko ila kama hakuna mizigo inakuwa ngumu sana kwenda huko labda nipite barabarani!

Nilianza kuishiwa nguvu pale maana sikutaka kupita barabarani kwa maana sikuwa na pasipoti na ukizingatia ile nchi ya Kongo kulikuwa na mambo ya Waasi,hivyo nilijua inaweza kuniingiza matatani!
Jamaa aliniambia kwanini nisikodi mtumbwi unipeleke Moba?,Nilimuuliza gharama za kukodi mtumbwi mpaka Moba ni kiasi gani?,Jamaa aliniambia ni namna nitakavyoelewana na mwenye mtumbwi!

Basi nilimwambia yule jamaa aniulizie kukodi mtumbwi mpaka Moba ni kiasi gani kwa wale wavuvi wenzie!
Kuna jamaa alikuja pale tukaanza kuelewana nae na alikubali kunipeleka ila nimlipe faranga 40000/=,nilimlipa ile hela nami nikabaki mfukoni kama na faranga 38000/=,Hizi faranga nilizobaki nazo ni zile nilizochenji Kule kigoma na nilikuwa na pesa za kitanzania kama 202000/=

Kabla ya kuondoka maeneo hayo nilimuomba jamaa anielekeze maeneo ya kupata chakula maana nilikuwa nina njaa sana!
Muda huo ilikuwa kama saa 8 mchana!,Jamaa alinichukua mpaka kwenye banda moja lililokuwa jirani nikakuta wanauza vyakula kadhaa wa kadhaa,Mimi niliagiza wali samaki,Nilipomaliza kupata msosi nilishusia na maji na nikamlipa yule mama pale kama faranga 2000/= nikaondoka zangu!

Jamaa alimchukua rafiki yake mwingine hivyo kwenye ule mtumbwi tukawa watu 3,mimi nilikaa katikati na kibegi changu halafu wale jamaa mmoja alikaa nyuma na mwingi mbele wakaanza kupia makasia!
Tuliyakata maji kwa umbali mrefu sana na mida ya saa kumi na moja tukawa tumefika pale Moba,Nakumbuka Jamaa alinielekeza kwamba nikifika hapo moba nitafute usafiri wa kunipeleka Kirungu maana si mbali!
Nilitafuta usafiri pale Moba nikafanikiwa kupata na safari ya kuelekea kirungu ilianza!
Wakati tukiwa njiani nilijaribu kumuuliza yule jamaa wa boda boda kama anamfahamu mganga maarufu maeneo hayo ya Kirungu anafahamika kama Nchibaronda!
Jamaa aliniambia alikuwa akimfahamu na atanipeleka mpaka kwake maana alikuwa anakaa nje ya mji wa Kirungu huko milimani maporini!

Baada ya mwendo mrefu tuliingia hapo mjini kirungu,Kiukweli mimi Kongo nilipapenda kwasababu kila mji ulikuwa mkubwa na ulikuwa na huduma zote mpaka usafiri wa Anga,yaani unakuta mji ni mdogo tu lakini mpaka una kiwanja cha ndege tofati kabisa na Tanzania ambapo viwanja vya ndege ni kwenye miji mikubwa ambayo ni makao makuu ya mikoa lakini kongo ilikuwa tofauti kidogo!
Tuliikamata barabara ya kuelekea huko milimani kwa Nchibaronda na haikuchukuwa muda mrefu tukawa tumefika pale!

Nilimlipa jamaa pesa tuliyokuwa tumekubaliana na akanielekeza kwa Mzee Nchibaronda!,Nilitembea kidogo maana haikuwa mbali na pale Boda aliponiacha!
Nilipofika hapo kwa huyo mzee nilipokelewa na mama mmoja na nilikaribishwa kwa lugha ya kilingala "boyei bulamu"
Boyei bulamu alimaanisha "Karibu",sasa kwakuwa mimi nilikuwa sielewi kilingala na kifaransa nilimwitikia kwa kiswahili "Ahsante"
Nilipokuwa huko kuna maneno baadhi ya lugha ya kilingala nilikuwa nimeshayaelewa hivyo sikupata taabu sana!

Baada ya kuwa nimekaribishwa niliambiwa nikae hapo nje maana mtaalamu (Mganga)kuna watu kaenda nao polini kuwaagua!
Hiyo ilikuwa mida ya saa 12 jioni mpaka nafika pale!
Kiukweli nilikuta kuna watu wengi kidogo na kuna jamaa kama wawili walikuwa wametoka Tanzania,nilipowaona nilijua tu hizi njema ni kutoka Bongoland maana mbongo anafahamika tu hata mkikutana nae nchi za watu!
Niliwasalimia na kwa bahati nzuri walinionyeshea ushirikiano,mmoja alikuwa mnene alionyesha alikuwa na maisha mazuri,basi hatukupiga sana stori maana niliona kama wana nikwepa ile kiaina!

Kwenye hilo eneo la Mganga Nchibaronda kulikuwa na vijumba vingi vya nyasi vilivyokuwa vidogo vidogo!,kama kawaida ya pale pia ulipofika usiku walikoka moto tukawa tunaota pale nje!
Ilipofika mida kama ya saa 2 Usiku yule Mzee Nchibaronda alifika na Alisema wageni waitwe waingie mmoja mmoja,sasa kwakuwa mimi kuna watu niliwakuta pale ilibidi waanze wao!,Zamu yangu ilifika ilikuwa kama mida ya saa 4 za usiku!,Nilipofika ndani nilimsalimia yule Mzee na kabla ya kuongea nae chochote nilitoa kile kingozi kilichokuwa kimekazwa kama kijiti ambacho nilipewa kule Kasulu na yule Mama akiambia ile ni rufaa ya mimi kwenda pale!

Mzee Nchibaronda alikipokea na akaniambia alifahamu ninakuja na alikuwa akiniona kila hatua niliyopiga,Yule Mzee aliniambia hata kabla sijamweleza chochote mimi pale nimefata utajiri na nitaupata!
Aliniuliza "JE UTAWEZA"?,kwakuwa nilikuwa nimedhamiria nilimwambia "Nitaweza"
Mzee Nchibaronda aliniambia hakuna aliyefata hapo kwake utajiri na akashindwa kufanikiwa kwani wote wanafanikiwa,Aliendelea kuniambia kwamba hata hao watanzania niliowakuta hapo nje wamekuja kumlipa shukurani baada ya kufanikiwa kwenye shughuli zao!

Baada ya mazungumzo mle ndani aliniambia kwakuwa kazi yangu ilikuwa ngumu kidogo alinitaka nikae pale wiki nzima maana kuna safari ya kwenda ziwa Tanganyika ambako huko ndiko nitapatiwa utajiri,na akaendelea kusisitiza kwamba yupo atakayenipa Utajiri ila siyo yeye!,Yeye kazi ambayo angeifanya ni kuniandaa ili safari ya kwenda Ziwani itakapofika nisije kupata madhara!


Itaendelea................
Alooooo mkuu ume hustle sio mchezo
 
Mrume ndago kwa hisani ya ghost members naomba ni koment uko byeee


Mrume ndago shusha vitu
 
Jamaa ananifanya najiona msahaulifu sana.

Anakumbuka details ndogondogo sana kama majina ya watu, majina ya sehemu alizopita mpaka muda wa matukio.

Mimi mpaka muda huu sikumbuki hata ulisema faranga moja ni sawa na sh ngapi ya TZ.
Kichwa chako kibovu.
 
Jamaa ananifanya najiona msahaulifu sana.

Anakumbuka details ndogondogo sana kama majina ya watu, majina ya sehemu alizopita mpaka muda wa matukio.

Mimi mpaka muda huu sikumbuki hata ulisema faranga moja ni sawa na sh ngapi ya TZ.
Mkuu IQ Yako ndogo [emoji22][emoji846][emoji846][emoji2]

Ukiona haukumbuki hata jana ulifanya nn jua wewe unaishi leo tu
 
Kichwa chako kibovu.

Mkuu IQ Yako ndogo [emoji22][emoji846][emoji846][emoji2]

Ukiona haukumbuki hata jana ulifanya nn jua wewe unaishi leo tu

IMG_6326.png
 
Jamaa ananifanya najiona msahaulifu sana.

Anakumbuka details ndogondogo sana kama majina ya watu, majina ya sehemu alizopita mpaka muda wa matukio.

Mimi mpaka muda huu sikumbuki hata ulisema faranga moja ni sawa na sh ngapi ya TZ.
Ukisema nisimulie maisha yangu vya nyuma vitaenda mbele vya mbele vitakaa nyuma na vya katikati vitapachikwa juu kwa juu
 
Jamaa ananifanya najiona msahaulifu sana.

Anakumbuka details ndogondogo sana kama majina ya watu, majina ya sehemu alizopita mpaka muda wa matukio.

Mimi mpaka muda huu sikumbuki hata ulisema faranga moja ni sawa na sh ngapi ya TZ.
hata mm mwanangu inaniumizaga kukosa kumbukumbu kwenye vitu vidogo vidogo
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 15.

Inaendelea.............


Asubuhi kulipokucha mzee Nchabironda aliniambia inapaswa sasa twende porini ambako ingenibidi kukaa kwa wiki nzima nikifundishwa kuchanganya madawa mbalimbali kwakutumia miti pori.Kusudi la kufundishwa namna ya kuchanganya dawa ni namna nitakavyokuwa ninahusika na kafara na namna ya kuishi na utajiri nitakaoupata.Basi mzee Nchibaronda aliniambia inapaswa niache kila kitu hapo nyumbani kwake na huko ninako elekea inapaswa nibebe Kisu tu!.

Mzee aliniuliza "Uko tayari?".

Nilimjibu "nipo tayari mzee".

Mzee aliniambia kwakuwa ninautaka utajiri inapaswa chochote nitakachokiona huko msituni inapaswa nishinde na nisiogope kwani hayana budi kutokea ili kunikomaza,mzee aliniambia akiangalia nyota yangu anaona kabisa mimi ni jasiri kama dume la Simba hivyo akasema sipaswi kushindwa!.Kwakuwa nilikuwa nimedhamiria kuwa tajiri kiukweli sikuona jambo lolote la kunizuia,nilikuwa nikikumbuka kauli za dharau na nyodo za yule shemeji wa Mwanza nilikuwa napata kama uchizi! Nilikuwa nikijisemea kwamba "siwezi kusafiri umbali mrefu,nimevuka mabonde na milima halafu nishindwe".

Mzee Nchibaronda aliendelea kusisitiza kwamba mara baada ya kunipeleka porini yeye atarudi na ataniacha huko mpaka siku saba zitimie yeye ndiyo angekuja kunichukua!.Nilimuuliza huko porini nitakula nini?.

Akasema "kuna mzee mtakuwa naye huko atakueleza kila kitu cha kufanya!".

Tuliondoka hapo nyumbani kwake kuelekea porini,msitu ule ulikuwa umefunga sana na katikati ya ule msitu kulikuwa na mto mkubwa!,wakati tunaenda mzee aliniambia nitakapokuwa kule porini nisije kuwa na mawazo ya mwanamke wala tamaa!.Baada ya kufika kwenye lile pori mara ghafla mzee siku muona na nilisikia tu sauti ikisema "Nitarudi".Kiukweli niliogopa sana lakini sikuwa na namna maana nilisema kwakuwa niliutaka utajiri sikuwa na budi kuvumilia,mpaka wakati huo sikuwa na kitu chochote zaidi ya kisu na nguo nilizokuwa nimevaa tu!,lilikuwa ni pori zito lililofunga,sikuona nyumba wala mtu yeyote zaidi ya mto mkubwa!.

Nilipiga hatua kadhaa mbele nikasikia sauti ikisema "Kombo na yo?",ilikuwa ikimaanisha "Unaitwa nani?".

Nilimwambia naitwa...........

Kiukweli ndugu zangu mpaka leo huwa sijui ni nini kilitokea kule msituni maana kwa wiki hiyo yote nilikuwa naweza kuongea na kuelewa lingala vizuri bila shida yeyote ila nilivyotoka tu msituni ikawa tia maji tia maji!,japo niliendelea kuelewa maneno baadhi!.

Ile sauti iliendelea kuniuliza "Mpo na nini ozali awa?",ilikuwa ikimaanisha "Kwanini uko hapa?".

Niliijibu "Ninataka kuwa tajiri".

Baada ya muda kidogo nilihisi kama kuna mtu alikuwa nyuma yangu,ile nageuka nikakutana na mzee mmoja ambaye alikuwa uchi kama alivyozaliwa!,nilishituka sana ndipo mzee aliniambia "Kobanga te!",yaani "Usiogope".

Yule mzee alinichukua mpaka mahali fulani porini kwa ndani zaidi,baada ya kufika huko aliniambia nivue nguo nibaki uchi kama yeye alivyokuwa!.Kiuweli kulikuwa na baridi kali lakini hukukuwa na namna!,basi mzee alianza kunionyesha miti mbalimbali na namna ya kuichanganya mpaka inakuwa dawa!,Kuna mti fulani alinionyesha na namna ya kuuchanganya na miti mingine hatimaye ukawaka moto!.

Mzee aliniuliza "Omoni alingaki ete tokolya?" ,yaani "Je unataka kula?".

Nilimjibu "Boye",nilimaanisha "Ndiyo".

Basi yule mzee alianza kunifundisha namna ya kuchanganya dawa ambayo ningeweza kumkamata mnyama yeyote hapo porini pasipo shida yeyote!,aliendelea kunifundisha dawa za aina mbalimbali ikiwemo ya kusimama mahala popote pasipo kuonekana na mtu yeyote na nikafanya chochote nitakacho.Siku zilisonga nikiwa humo msituni nikifundishwa na huyo mzee,ndani ya siku zote hizo saba sikuwahi kupata usingizi wa aina yeyote na nilipokuwa nikihisi njaa nilitengeneza dawa ambayo ilinielekeza mnyama yeyote alipo,nilipofika hapo nilimkamata na kuchinja kisha nilitengeneza dawa ya kuwasha moto na kuanza kupiga kitoweo kama kawaida,niliwala sana digidigi pamoja kware kwa kipindi hicho cha wiki nzima niliyokuwa huko porini!.Siku moja kabla kumaliza zile siku saba nikiwa mle porini,yule mzee kwa wakati ule hakuwepo maana yeye alikuwa akija na kutoweka!,wakati huo nilikuwa uchi kama nilivyozaliwa.Niliteremka kwenda mtoni ili nikamate kambale ambao nije nichome nile,mara ghafla nikakuta mwanamke mzuri ambaye sijawahi kumuona toka nizaliwe akiwa anaoga pembeni ya mto akiwa kama alivyo zaliwa!.

Nilipokaribia wale kambale ambao tayar nilishawafanyia dawa wakiwa wananisubiri niwatoe mtoni,yule mwanamke aliniita kwa jina langu,aliniambia nisogee nikamsugue mgongoni!.Kiukweli namna alivyokuwa mzuri nilishindwa kuelewa katokea wapi na ukizingatia mle ndani ya pori hakukuwa na makazi ya watu au viumbe wa kawaida!.Nilipomsogelea yule mwanamke nilijikuta uume umesimama ghafla,nilikumbuka ile kauli ya mzee Nchibaronda kwamba nisiwe na tamaa ya mwanamke yeyote nitakaye muona au kukutana naye!.Nilisikia sauti moja ilikuwa ikiniambia nishiriki naye ngono yule mwanamke na nyingine ilikuwa ikinisihi sana niache tamaa maana ningefanya hilo tendo kila kitu kilikuwa kinaharibika!,Kiukweli nilikuwa katika jaribu kali sana na hakuna mwanaume yeyote ambaye alikuwa mwenye uwezo kamili angemwacha yule mwanamke,ukizingatia nilikuwa nina muda mrefu sijakutana na mwanamke!.Niliwaza sana namna nilivyosota kufika hapo na kile kilichonipeleka huko,ghafla nilighairi mawazo mabaya na uume wangu ulianza kulala na ndipo ghafla yule mwanamke alipotea machoni pangu!.Nilichukua zangu kambale na kwenda kuchoma tayari kwa kuliwa,nikiwa porini pia nilifundishwa namna ya kukinga damu kwenye kibuyu na namna ya kutoa kafara kwa njia ya ajali.

Basi baada ya zile siku saba yule mzee Nchibaronda alinifata na alifurahi sana akawa anasema kama nimeweza kukaa kwenye pori na kuvumilia misuko suko yote ikiwemo baridi kali kusingekuwa na cha kunishinda!.Nilipofika hapo nyumbani kwake nilikaa siku mbili na siku ya tatu walikuja jamaa wawili ambao walikuwa watanzania,wao walikuwa wenyeji wa Sumbawanga.Hawa jamaa baadae nilikuja kufahamu kwamba wao walifuata uchaw.Hao jamaa siku ambayo nilikwenda ziwa Tanganyika niliongozana nao.Siku ya tano baada ya kutoka msituni mzee Nchibaronda alisema umewadia sasa wakati wa sisi kwenda Ziwa Tanganyika,na hatukupaswa kuvaa nguo za kawaida bali kila mtu alifungwa ngozi ya mnyama kufunika nyeti zake,sikuweza kuelewa ile ngozi ilikuwa ya mnyama wa aina gani!.

Wale jamaa mmoja alipewa shilingi iliyokuwa na tundu katikati,mzee Nchibaronda akatuambia hiyo ni nauli,yule mwingine alipewa irizi ikiwa imefungwa kwa ustadi wa hali ya juu na mzee akasema hiyo ni pasipoti ya tunapokwenda!,Pia mzee alinipatia unga fulani hivi ambao baadae nilikuja kugundua ulikiwa unga wa mifupa ya albino uliyokuwa umesagwa sana!.Mzee alitupatia maelekezo kila mtu kutokana na kitu alichopewa,mimi niliambiwa tutakapofika hapo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika niumwage ule unga ziwani(Kwenye maji),maana ni chakula cha majini na ndiyo shukurani yetu kwa wakati huo,wale wenzangu pia walipewa maelekezo kila mtu kulingana nanalichopewa.Basi baada ya kukamilisha lile zoezi ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua tukajikuta tupo kando ya Ziwa Tanganyika,tulikuta watu wanafanya shughuli mbalimbali kando ya lile ziwa lakini wao walikuwa hawatuoni lakini sisi tuliwaona wao!.



Itaendelea....................
 
Back
Top Bottom