Majula Jm
Member
- Sep 12, 2020
- 14
- 11
nitag basiNitag huo uzi mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nitag basiNitag huo uzi mkuu
Hapo ndio unafaidi story sio Mambo ya nusu nusuHaya mambo ys nitaendelea ningejua ningefanya kama ile hadithi ya msitu wa nairoto. Niliacha uzi utiririke week kadhaa. Nilipokuja kusoma nikasoma yote.
Lipua mzeeTulipueeeeee????
MKASA WA PILI - Sehemu ya 21
Inaendelea.............
Nikiwa geto nilisikia sauti kama kawaida ikiniambia niende mbeya na nikifika hapo mbeya nitapewa ishara ya nini cha kufanya!
Kwakuwa tayari nishazoea ile hali hivyo nilikuwa siogopi wala kuwa na wasiwasi!
Kwa wakati ule sikuwa kabisa na akili nyingine zaidi ya kuona ninayafaidi maisha kwa maana kila nilichokitaka nilikipata kwa wakati!
Basi nilijiandaa na niliushika mkono wangu wa kushoto na kutamka "Ninataka niwe mbeya muda huu",ilikuwa ni kitendo cha kufumbua nikajikuta nipo uyole mbeya!
Kiukweli ile irizi ambayo iliwekwa mkononi mwangu na yule malikia kule chini ya ziwa Tanganyika ilikuwa na nguvu za ajabu na ilinipatia kiburi sana mpaka nikawa nawaoana binadamu wenzangu kama TAKA TAKA!
Namshukuru sana Mungu kwa kunitoa huko!Mungu ni mwema sana na uwezo,rehema na fadhili zake hazina kikomo!
Basi nilipofika yale maeneo kuna gari nililiona lilikuwa costa na kwa muonekano nililifahamu kwamba ndilo gari ambalo inapaswa nikalipige mzinga,Lilipofika yale maeneo nilipokuwa lilisimama na konda akawa anasema "Kyela hiyooooooo,twenzetu tukuyu mpaka kyela hiyoooooo!",Nilipanda ndani ya ile costa na kama kawaida sikulipa nauli na yule konda hata hakuniuliza kuhusu nauli!
Lile gari lilifika kwenye mji mmoja nadhani ulikuwa unaitwa Kimo kama sijakosea(Kama kuna wenyeji wa huko wanaosoma huu uzi watanikumbushia,maana ni muda kidogo),Huo Mji wa kimo ulikuwa kabla ya kufika Tukuyu!,Ile sauti iliniambia nishuke na niendee mbele ya Tukuyu kuelekea kyela kulikuwa kuna mtelemko mkali sana pale nikaisubiri pale!
Nilifanya kama ile sauti ilivyonitaka nifanye na nilipotea ghafla yale maeneo na nikafika eneo la tukio!
Kiukweli kilikuwa na mtelemko mkali sana yale maeneo na sikumbuki palikuwa wapi maana kulikuwa na miti mingi sana ile ya mbao!,Nadhani ni hapo hapo tukuyu kwa ndani ndani,Wenyeji wa huko watatusaidia!
Basi niliweka tego kama kawaida nikiwa nimeshika kibuyu cha kazi,Baada ya kusubili kwa muda niliiona ile costa ikiwa inakuja kwa mwendo wa kasi!,Ilipofika yale maeneo ilikula mzinga wa maana sana!
Niliisogelea ile costa na kwenda kuanza kuchukua kilichonipeleka!,Lakini ghafla ndani ya ile costa niliwaona akina mama wawili wakiwa wananiangalia wakisema "We mtoto unafanya nini"?
Wale kina mama walikuwa washirikina na watu wengine walipokuwa wamelaliwa na viti wao walikiwa wamekaa wakinikodolea macho!
Waliniita mimi mtoto si kwamba umri wangu nilikuwa mtoto bali walionyesha dharau kwamba mimi si lolote wala chochote!
Niliwaambia kwakuwa wameniita mimi mtoto ninataka niwaonyeshe mimi si mtoto kwenye ile kazi kama wao walivyodhani!,Kama nilivyosema hapo awali kwamba nilikuwa nina uwezo wa ajabu na kiburi kilikuwa kimenijaa sana!
Niliwasogelea na kuanza kushindana nao pale kichawi lakini nilipotamka ya kwamba "Naomba mkauke muwe kama samaki",haikuchukua muda walikuwa wamekauka kauuu!
Wao ndo walikuwa wa kwanza kuchukua damu yao na baada ya hapo nilianza kukusanya damu za abiria wengine!,Nilipomaliza kufanya lile zoezi nilipotea yale maeneo! Na nikatokezea pale nilipokuwa mwanzo Uyole!
Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa kuna mgahawa mmoja ambao ulikuwa mkubwa tu kama hotel kwa ajili ya kupata chakula!,Nilipofika hapo kwa kuwa bado nilikuwa nimevaa uhusika wa kishirikina maana sikutaka bugudha!,Ile nimeingia ndani ya huo mgahawa niliona kina mama ambao walikuwa wakitoa huduma hapo hotelini walikuwa uchi wa mnyama!,Alikuwa mwanamke mmoja mnene na Binti yake ambaye pia alikuwa uchi!
Huyo binti yake yeye alikuwa akivuja damu kutoka kwenye uke wake na alikuwa akizichukua zile damu na kuziweka pakaza kwenye vile vyakula vya wateja walivyokuwa wamemwagiza!
Sasa kwa bahati mbaya sana hakuna mteja ambaye alikuwa akiona yale matukio yote isipokuwa mimi niliyekuwa na uwezo huo!Hicho ki-mgahawa kilikuwa kimechangamka sana maana hadi madereva wa magari makubwa niliona walikuwa wakiingia kula pale!,ukimuondoa yule mama na yule Binti niliyewakuta uchi pale pia kulikuwa na wahudumu wengine wawili,Mmoja alikuwa mpishi na mwingine pia alikuwa akihudumia lakini hawa wao walikuwa wamevaa nguo zao tu za kawaida!
Sikupata shida kuelewa kwamba yule mama ndiye alikuwa mmiliki wa ule mgahawa na yule aliyekuwa akivuja damu ukeni alikuwa binti yake wa kumzaa!
Yule mama aliponiona tu alinifanyia ishara ya kidole kwamba nikae kimya!Yule binti alikuwa akinitolea macho na nilimuona anakuwa na wasiwasi!
Basi nilimwita yule mwanamke nikamwambia aniletee chakula ila kiwe kisafi tofauti na hapo ningemuumbua!
Alimwita yule binti aliyekuwa kavaa nguo akamwambia "Mpe yule kaka chakula"
Zilikuja ndizi zimejaa sahani na nyama na kwakuwa nilikuwa nina uwezo wa kukiangalia kama ni kisafi ama la!,baada ya kujiridhisha kilikuwa kisafi kwa maana kwamba hawakuweka mambo yao ya kishirikina nilianza kula!
Wakati nakula watu wengi walikuwa wakiingia kupata msosi wakiamini ni msosi mtamu kumbe yule binti alikuwa akichanganya na damu zake zilizokuwa zinatoka ukeni!
Wakati nikiwa bado naendelea kupata msosi waliingia jamaa mmoja akiwa na mwanamke na bila shaka walikuwa mke na mume,Walipotengewa chakula kabla ya kula walifanya pale ishara ya msalaba kwa maana nadhani walikuwa wakiomba na hii ishara ya msalaba haikusaidia kitu kwani walilishwa uchafu kama wenzao!
Kiukweli ule mgahawa ulikuwa na wateja sana na yule mama kama ni pesa basi alikuwa akiingiza ki-kwelikweli!
Labda niseme kitu hapa kidogo!,Ndugu zangu ukiamua kuwa mfuasi wa kristo basi achana na mabo mengine ya duniani vinginevyo unaweza ukadhani Yesu anakulinda kumbe tu kwakuwa unashika mambo mawili mawili ukawa huna tofauti na watu wasiyosali!Wale jamaa waliongia na mkewe kwenye ule mgahawa inaonekana walikuwa wakimpenda sana Yesu kwa maneno ila matendo hakuna!,Kiukweli wangekuwa watu wa maombi wasingelishwa ule uchafu,lakini kwasababu wengi wetu dini tumezifanya kama fasheni ilikuwa haijawasaidia kitu!
Mimi mwenyewe kuna wakati nilishindwa kufanya tukio lolote la ushirikina kwasababu kuna watu niliokutana nao wakiwa na nguvu ya Yesu na nilishindwa pamoja na ujanja wangu wote!
Baada ya kuwa nimemaliza kula niliondoka zangu bila kulipa na yule mama aliniita kabla ya kuondoaka na akaanza kuniuliza "Vp mwenzetu wewe niwa nchi gani"?
Nilimwambia mimi natokea Kigoma na hapo nilipo nilikuwa safarini kurudi kigoma
Alikuwa akinishangaa sana kwa namna nilivyokuwa jasiri,na wakati huo naongea nae alikuwa uchi kama alivyozaliwa ila watu wengine walikuwa wakimuona kavaa nguo!
Nipomaliza kuzungumza nae nilimwambia mi naondoka zangu!
Basi nilitamka tu kwamba "Nahitaji hivi sasa kuwa Mwanza"
Ndani ya sekunde nilijikuta nipo Geto na kama kawaida nilikiweka kile kibuyu chini ya uvungu na mimi nilijipumzisha kidogo kisha baada ya kuamka nilielekea nyumbani kwa Bi mkubwa!
Itaendelea......................
Piga namba hii kwa ajili ya maswali na maulizo yoyote 0757453320
Kabisa mkuu huenda mzee alikua na maagano na huyo dada.Mshua wenu kwa namna moja ama nyingine anahusika na Huyo Bi ashura ni ngumu sana nguvu za Giza zikusumbue bila sababu iwe ni wewe au mtu yoyote wa damu yako aliingia mkataba na hizo nguvu ndo maana walikuwa huru kuwamiliki
ila kuna viashiria vingi kuwa hii ni zile hadithi za hekaya za Abunuwasi iliyoimarishwa ...iwe hekaya iwe kweli soma pita hivi kwanza hulazimishw kusoma .
Ukija apa unatuuliza hivi halafu unakimbia huwa una maana gani?Tulipueeeeee????
Stori ishaanza kukosa Radha Haina hata uzuri wowte yaani ,kisa huko chini itaendelea nachokushauri usilete huo mwendelezo badala ya kusema itaendelea andika hata siku mbili au tano kabisa ikisha kamilika ndo uilete hapo hakuna hata Cha kukielewa ,smart people always doing smart thingu
Unamlipa nnStori ishaanza kukosa Radha Haina hata uzuri wowte yaani ,kisa huko chini itaendelea nachokushauri usilete huo mwendelezo badala ya kusema itaendelea andika hata siku mbili au tano kabisa ikisha kamilika ndo uilete hapo hakuna hata Cha kukielewa ,smart people always doing smart thing
Hata kama wana kamati watachukia lakini lazima tukubali maelezo yamekuwa mengi yasiyo na maana yoyote[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]hebu tuondolee uchuro hapa...andika ya kwako isiyo ms maeleze
Habari za masiku Mkuu, naweza pataje hii story Mkuu wangu j.pili nakua kanisani hyo mida? Kama iko Instagram ni unge Mkuu.Kesho kama kawaida kisa hiki ķinaendelea kusikika redioni kwenye kipindi cha sitosahahu?nawakaribisha nyooooooooote.
Kaa kwa kutulia mkuu itaendelea hapa muda si mrefuHabari za masiku Mkuu, naweza pataje hii story Mkuu wangu j.pili nakua kanisani hyo mida? Kama iko Instagram ni unge Mkuu.
Alafu kesho umuambie Magasha apangilie vizuri mfuatano wa visa youtube, sio haya mambo ya sehemu ya 4 ni LwandaMagere, ya 5 ni Zabloni. Ili ambao hatupati ule muda wa redioni tuende sambamba na awamu ya tano.Kaa kwa kutulia mkuu itaendelea hapa muda si mrefu
Fanya hivyo mkuu sehemu ya 24Kaa kwa kutulia mkuu itaendelea hapa muda si mrefu