Kwanza kabisa nianze kuwashukuru wale wote waliyofanikisha hadi mimi kuwa hapa pamoja na changamoto nilizopitia kama mwanadamu,pia niwaombe radhi watu wote ambao huu mkasa wangu wa maisha ya kitajiri yaliyohusisha nguvu za giza yalivyo ondoa roho za wapendwa wao.
Pia ndugu zangu huu mkasa naendelea kuusimulia pale RADIO FREE AFRICA kwenye kipindi chao cha SITOSAHAU ambacho huruka hewani kila siku ya Jumapili kuanzia saa 4 -5 asubuhi.
Vilevile pia kama nilivyowajulisha ya kwamba,kile kitabu changu kilichosheheni hiki kisa cha kweli cha maisha yangu kipo tayari na kinajulikana kama UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA YANGU,kipo sehemu 1 & sehemu ya 2,Kwakuwa mambo yote niliyoyafanya yaliyokuwa yanatisha,sitoweza kuyaweka hapa ila kwenye kitabu nimeyaandika pasipo kificho chochote.
Mods pia niwaombe msamaha kwa yale yaliyojitokeza hapo mwanzo mpaka kufikia kunipiga Ban,sitorudia tena na nimejifunza,pia niwaombe muwe mnanielekeza ambapo mnaona navuka mipaka ya kitaaluma,anuani yangu ni hii -
lwandamagere2012@gmail.com
KARIBUNI.
MKASA WA PILI - Sehemu ya 24
Inaendelea.............
Nilihamia pale nyumbani kwangu rasmi na nilitenga chumba maalumu ambacho hakuruhusiwa kuingia mtu mwingine yeyote ila mimi tu!
Kile chumba kabla ya kuhamia pale nilimwambia yule Mwanamke niliyempa kazi ya ku-decorate nyumba asikiguse maana nilimdanganya kuna mafundi wanakuja kukikarabati!
Na kweli!yule mwanamke hakukigusa kile chumba!.
Baada ya kufika hapo nyumbani mboni ya jicho langu na roho yangu ilikuwa kwenye hicho chumba!,basi niliingia kwenye kile chumba nikakisafisha kikawa cheupe peee!,kuna mazulia makubwa mekundu nilinunua nikatandika chumba kizima!
Nilichukua kile kibuyu nikakiweka katikati ya kile chumba na lile begi la kuhifadhi pesa nikaliweka kando ya kile kibuyu.Baada ya kuwa nimemaliza na kuhakikisha mle ndani pako sawa nilitoka zangu!,
Kumbuka kule ziwani Tanganyika niliambiwa nikishakuwa na chumba na kukitenga ingenipasa kuingia mara mbili tu!
Mara ya kwanza ni kila tarehe 15 ya kila mwezi kuingia kuchukua pesa na kila mwisho wa mwezi kuhakikisha nakiingiza kibuyu kikiwa na damu ambazo ilipaswa kila mwezi niwe natoa kafara!
Sasa kule geto sikuweza kuyafanya hayo yote maana nilikuwa kwenye chumba kimoja na bahati nzuri nilikuwa nikisikia sauti ikinipa maelekezo hivyo ingekuwa jambo baya nisingemaliza hata dakika moja ningekaushwa!.Huku kwangu niliko hamia jamaa hawakutaka kabisa masikhara.
Nilipanga kwenda kumwambia mama yangu kwamba nimenunua nyumba maana hapo awali nilikua nimemdanganya ya kwamba nimechukua mkopo!
Basi nilimpigia simu nikamwambia dereva awachukue yeye pamoja na ndugu baadhi waliokuwa nyumbani Nyegezi awalete mpaka Igoma.Baada ya mama kufika pale kwenye mjengo wangu alihamaki sana na kiukweli aliniuliza pesa za kununua ule mjengo nimetoa wapi?,Niliendelea kumdanganya kwamba nimechukua mkopo na hii nyumba nimeilipia nusu, najitahidi kuendelea kutafuta pesa ili niweze kumalizia pesa za watu!
Miongoni mwa watoto ambao mama yangu alikuwa akiwaamini, basi ni mimi,hakuwa na shaka kabisa!
Kiukweli heshima ilikuwepo kwa wajinga wote waliyokuwa wakitudharau, habari zilianza kumfikia yule shemeji ambaye alikuwa na nyodo na niliapa kumfunza adabu kwa kumfanya mke wangu!.
Ndugu zangu yule shemeji asingekuwa kajaaliwa na mwenyezi Mungu ningeachana naye,lakini kilichomponza ni namna alivyokuwa kuwa kanona na kiuweli alikuwa kajaaliwa shepu na uzuri,niliapa nitamshughulikia kisawasawa.Mpaka wakati huo nilikuwa nimeagiza gari Dar es salaam aina ya VX V8 Amazon,Lile gari la Vx v8 amazon kuna jamaa mmoja hapo mjini Mwanza alikuwa na maduka ya spea za magari alikuwa anatembelea ,hivyo kwakuwa nililipenda niliamua kuagiza Dar es salaam na nilikuwa nimelipia pesa nusu!.
Baada ya muda mama na ndugu aliyokuwa amekuja nao waliondoka,nilimwambia baadae nitaenda kupata chakula hivyo waniandalie.Sasa kwenye akili yangu nilikuwa ninamuwaza Zainati pamoja na Yusta na niliapa hakika usiku huo lazima wakione cha mtema kuni!.Kwakuwa yale maduka yaliyokuwa yakiuza vito yalikuwa yakiwahi kufungwa,niliingia ndani nikaandaa dawa ambayo hakuna mwanamke yeyote chini ya jua ambaye nilikuwa nikimuhitaji angekataa, nikaiweka kwenye mfuko wa suruali,uzuri wa ile dawa hata kama ungeichukua kama kitone cha mbegu ya mchicha huyo mwanamke uliyemkusudia alikuwa anaisoma namba!
Niliondoka zangu kuelekea hapo dukani kwao Zainati, ilikuwa kama mida ya saa 9 alasiri,Kwa bahati nzuri nilimkuta yeye akiwa dukani!,Lile duka lilikuwa kubwa na kuna jamaa mwingine aliyekuwa bize na mambo yake wakati naingia.
Japo nilikuwa nina dawa lakini sikutaka kuonekana mnyonge kwenye suala la kupendeza,nilikuwa navaa ki-gentlemen na nguo zilikaa sana hasa ukizingatia nilikuwa nina ka-kitambi ka kuzugia hivyo yeyote ambaye aliniona hakuwa na shaka kwamba nina hela!.
Nilimsabahi Zainati na alinichangamkia sana!.
Nilimuuliza "Vp mrembo mbona umekaa kiunyonge unaumwa?".
Alinijibu "Hapana ni uchovu tu".
Sikutaka kupoteza muda,nilimwambia "leo nataka nikutoe out"
Alinijibu"Niwewe tu na roho yako!"
Nilijua tayari magome ya mzee nchibaronda yameshafanya kazi!.
Nilimwambia "Nipe namba yako ya simu nitakucheki baadae".
Alinitajia namba yake pasipokuwa na shaka yoyote na safari hii hakuwa na ubavu wa kukataa kutoa namba!.
Aliniambia nihakikishe saa 1 jioni naenda kumchukua na atanielekeza maeneo nimfuate!.Basi nilimuaga nikaondoka zangu.Zainati alikuwa mzuri sana mtoto wa kiarabu na niliapa ningemshughulikia usiku huo mpaka maji aite mmah!.Niliondoka hapo dukani kwao kuelekea kupanda taxi ili niende Nyegezi na akili yangu ilihamia kwa Yusta, nilisema kabla ya kwenda kwa mama, nitaanzia kwao Yusta ili nimalize kila kitu.
Nilipofika kwao niligonga kengele na baada ya muda kidogo alikuja kufungua geti dogo mmoja wa kiume!.
Nilimuuliza "dogo baba yako yupo?".
Dogo akasema "Hayupo".
Nikamuuliza "Mama je?".
Pia akasema "hayupo,wameenda kazini".
Nilimuuliza "Nani yupo?"
Aliniambia "yupo dada Yusta na dada emy".
Nikamwambia "Niitie dada Yusta,mwambie kuna mgeni wake".
Kati ya wanawake wote niliyokutana nao katika kipindi hicho cha utajiri wa nguvu za giza niliyekuwa nikimwona natetemeka,alikuwa Yusta,sijajua mpaka leo kwanini ilikuwa hivyo,nadhani uenda kwasababu alikuwa mzuri sana!.
Alipokuja aliniambia "Ooh Braza J karibu".
Nikamwambia "Kwahiyo mara hii Yusta nishakuwa braza wako?"
Alicheka sana akaniambia "jamani!,kwani kukuita braza kuna ubaya,haya niambie handsome wa mama.......".(alitaja jina ambalo mama alikuwa akiitwa kutokana na dada yetu kuwa wa kwanza).
Nilimwambia "Kwanini Yusta unaendelea kunitesa mama,shida yako kubwa ni nini?".
Kwa mara ya kwanza akaniambia "basi wewe niambie leo chochote nitafanya ili nikuridhishe".Baada ya hiyo kauli nilisema kimoyo moyo "leo utanitambua mimi ni nani"
Nilimwambia "Nataka leo nikutoe out na ikiwezekana tukalale kwangu".
Aliniangaliaa akakosa jibu kwa muda kisha akaniambia "so nitawaaga wazazi wangu naenda wapi?".
Hapo hapo akili ikanituma nikwambia "Utamwambia mama unaenda kwa rafiki yako amekuita".
Akaniambia "unadhani itakuwa rahisi kihivyo?".
Sasa kwakuwa nilikuwa nimedhamilia nilimwambia "wewe ukimwambia hivyo tu mama atakubali na hatokuwa na maswali"
Aliniambia "Sawa kwahiyo unakuja kunichukua saa ngapi?".
Nilimwambia mimi naelekea nyumbani kwa mama kula,hivyo wewe jiandae na msubiri mama yako na baba yako uwaage ili iwe vyepesi mimi kukufuata baadae!,basi akaniambia mida ya saa 1 niende nikamchukue!.Nilipoondoka hayo maeneo nilivuta mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na ile irizi ya maajabu na kuanza kuongea ya kwamba "Chochote atakachosema mbele ya wazazi wake,wakubali na wasiwe na maswali".
Itaendelea.................