LwandaMagere
JF-Expert Member
- Mar 15, 2020
- 264
- 2,484
- Thread starter
- #1,881
MKASA WA PILI- Sehemu ya 28
Inaendelea.............
Nilipofungua kile chumba na kuingia ndani sikuamini macho yangu nilikutana uso kwa uso na yule Malikia aliyenipa yale masharti chini ya maji.
Baada ya kumsujudia aliniuliza "Inaelekea wewe unaufahamu sana kuliko sisi,si ndiyo?".
Nilimjibu "Hapana Malikia"
Akaendelea kuniuliza "wewe ulitumwa nini na ulichoenda kufanya ni nini?"
Kiukweli wakati huo nilikuwa naogopa na kutetemeka sana maana sikutegemea kumuona yule Malikia humo ndani,alikuja akiwa ndani ya vazi refu jeusi na nywele zake zilishuka mpaka chini ya lile zulia jekundu na kutokana na rangi yake kuwa nyeupe sana,yale mavazi yalimpendeza sana lakini alikuwa na hali ambayo nilipomuona tu nilianza kutetemeka kama nimewekwa kwenye baridi kali.Aliniambia itabidi nilipe gharama ya nilichokifanya na akasema hiyo gharama isichukue muda mrefu,aliniambia mtu ambaye inapaswa awe mbadala wa kile nilichokifanya ni yule mwalimu ambaye alikuwa mpenzi wangu.
Ndugu zangu kama mnakumbuka nilipoenda kutoa kafara kule Bungu niliwaambia kuna mama alikuwa kabeba mtoto,yule mama yeye nilimkausha na yule mtoto nilimwacha maana iliniingia huruma.Sasa kumbe lile lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo lingepelekea mimi kupoteza uhai,nilipaswa yule mtoto mchanga nimuue na nilikuwa nikifahamu kabisa lakini sasa kutokana na huruma kuniingia nilijikuta namwacha.Hivyo nilipaswa kulipa gharama ya kumuacha yule mtoto kuwa hai,hivyo kwa nilichokuwa nimefanya,yule Malikia aliniambia yule mwalimu niliyekuwa natembea naye inabidi nimtoe kafara mara moja.
Kiukweli niliumia sana na nilikuwa nina mawazo sana maana yule mwanamke tayari alishaanza kuniingia akilini,Sikuwa na namna ilibidi nitii yale maagizo ya Malikia.Baada ya dakika chache yule Malikia alipotea mle ndani na sikuweza kumuona tena.Mwaka huo ilikuwa mwanzoni mwa mwaka wa 2014 ambapo mambo haya yanatokea.Niliwaza sana namna itakavyokuwa bila yule mwalimu maana nilishaanza kumzoea,nilijipa moyo maana sikuwa na namna.
Asubuhi ya siku iliyofuata nilienda kule shuleni kama kawaida kuendelea na kazi yangu,baada ya vipindi tulionana na yule mwalimu.
Nilimwambia "Hivi unafahamu kwamba nimehamia kwenye ile nyumba yangu mpya?".
Alinijibu"Nitajulia wapi mimi wakati wapo unao wapenda ndiyo unaowambia!".
Kiukweli lile jibu liliniumiza sana hasa ukizingatia namna nilivyokuwa nampenda.
Nilimwambia "kesho jitahidi uje Igoma mpenzi wangu,uje uone mpenzi wako ninapokaa"
Yule mtoto wa watu hakuwa na hiyana alikubali bila kufahamu ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake hapa duniani.Kwakuwa siku hiyo nilikuwa nimechefukwa na mawazo yangu kichwani yakutosha,ndipo nilichukua simu nikaanza kutafuta namba ya yule shemeji,nilipoipata nilianza kumpigia maana tangu dada yangu aliponipatia sikuwahi kumpigia.
"Hallooo nani mwenzangu" Yule shemeji alikuwa akiniuliza.
Nilimwambia "Mimi ni........"
Aliendelea "Ooh,Shem za siku?"
Nilimjibu "Nzuri,mbona upo kimya sana shem".
Aliniambia "nakwambia shem nimebanana sana,siunajua tena kazi zetu hizi"
Aliniuliza "Shem nasikia umeshusha bonge la mjengo,yaani shem mpaka unajenga hatuambiani!,nimewakosea nini jamani,Wikiendi hii nakuja kwako na watoto shemu,hivyo andaa wine na msosi wa kutosha".
Sikutaka kumuonyeshea dharau maana pamoja na yote aliyoyafanya mpaka kusababisha mimi kuingia kwenye utajiri wa ushirikina,lakini niliamua kuwa mtulivu.Nilimwambia kwamba hapo nyumbani nakaa peke yangu labda nitamwambia dada yangu mkubwa aje awaandalie chakula kwa ajili ya ugeni wao.Nilikuwa natengeneza mazingira ili iwe rahisi kumtia kwenye himaya yangu na niliapa atakapo kuja hiyo wikiendi basi nitafanya niwezalo aingie kwenye kumi na nane.
Siku iliyofuata,kweli yule mwalimu alikuja pale nyumbani na alikuwa akishangaa sana namna ile nyumba ilivyokuwa nzuri.
Aliniuliza "Mwenzetu kumbe uko vizuri eenh!"
Yeye hakuwa akishangaa sana maana toka mwanzo niliwahi kumdanganya kwamba kazi ya pale shuleni mimi naifanya tu kama kuzugia ila nina biashara zangu nyingine,siku hiyo sikuwa na hamu kabisa ya kumkung'uta bakora kwasababu niliona muda si mrefu angepoteza uhai.
Nilimshika mkono kama geresha na nikamwambia "Nilikuwa nimekumiss sana mama".
Nilimwambia "nisubiri nakuja!".
Niliingia kwenye kile chumba cha siri nikaanza kutengeneza dawa na nilihakikisha namnyonya damu yote,kiukweli nilikuwa namuonea huruma sana lakini sikuwa na namna kwa maana asingekufa yeye ningekufa mimi na mimi wakati huo naogopa kufa!.Kuua wenzangu nilikuwa napenda ila mimi kufa nilikuwa sitaki kabisa kusikia.Nilipomaliza lile zoezi nilitoka mle chumbani na nilimwambia nataka kwenda kwa mama kule Nyegezi, hivyo twende tuondoke wote.Wakati tukiwa ndani ya taxi alianza kuvuja damu puani na nilielewa fika hatochukua muda atakuwa kapoteza uhai.
Nilitoa kitambaa nikaanza kumfuta zile damu na nikawa namuuliza "Unaumwa mama?".
Aliniambia "Nahisi kichwa kinauma".
Nilimuuliza "nikupeleke hospitali?".
Akaniambia "hapana,naelekea nyumbani kupumzika naamini kitapona"
Tulipofika maeneo ya Sahara,mimi nilishuka, nilimwambia dereva ampeleke mpaka nyumbani kwake na kisha atakuja kunichukua hapo aliponiacha anipeleke Nyegezi,niliamini hatomaliza siku akiwa hai maana nilikuwa tayari nishanyonya damu yake na kuitia kwenye kibuyu.
Nilipofika kwa mama kiukweli sikuwa na raha.Basi jioni nilimwambia mama kwamba shemeji kasema atakuja na familia yake kunitembelea jumamosi hivyo amwambie dada yangu mkubwa aje Igoma awaandalie chakula.Mama alishangaa sana lakini nilimwambia dawa ya yule shemeji ni kuja aangalie mafanikio yetu ili akawasimulie ndugu zake!.Kumbe mimi wakati huo nilikuwa nina langu moyoni,sikutaka kabisa ndugu zangu waelewe ni nini nilichokuwa nimekipanga kwa wakati huo.Baada ya usiku kuingia na kupata chakula niliondoka kurudi kwangu.Asubuhi ya siku iliyofuatia nilipigiwa simu na jamaa mmoja ambaye naye alikuwa mwalimu kwenye ile shule niliyokuwa nikifundisha, akawa ananiambia habari za msiba wa yule mwalimu ambaye alikuwa mpenzi wangu,sikushangaa sana maana nilifahamu tukio zima tangia mwanzo.Tulikubaliana na jamaa tuelekee msibani siku hiyo.
Baada ya siku mbili kumalizika toka tumzike yule mwalimu,kabla ya jumamosi alinipigia simu Zainati na alitaka nikaonane naye kule dukani kwao.Niliondoka mpaka dukani kwao na nilipofika nilimkuta,nilimuuliza kulikuwa kuna shida gani?.
Aliniambia "Nilitaka tu kukuona maana nimekumiss mpenzi".
Aliendelea kuniambia kwamba usiku wa siku hiyo angekuja nyumbani kulala maana kamiss bakora.Basi baada ya maongezi na kutaniana kwingi,mimi niliondoka zangu kuelekea nyumbani maana nilikuwa nimechoka sana.Mida ya jioni nilisikia gari ikipiga honi getini,mlinzi alifungua geti na safari hii Zainati alikuwa kaja na gari aina ya Prado.Baadae nilimuuliza lile gari lilikuwa la nani akaniambia lilikuwa la mama yake ambaye kwa wakati huo hakuwepo.
Nilikuwa najisemea ya kwamba "Shida ya huyu huwa ni king'ang'anizi,naweza kumcharaza bakora kesho asiondoke".
Lengo langu sikutaka kabisa yule shemeji atakapokuja amkute pale mwanamke mwingine.
Ila nilijisemea "kwakuwa nina uwezo wote nitajua la kufanya"
Itaendelea...............