Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 40.

Inaendelea.............

Asubuhi kulipokucha niliendelea kutafakari na kujiandaa kisaikolojia maana tayari nilikuwa nishapokea maagizo!.Nakumbuka ilipofika mida ya saa 3 asubuhi kuna simu iliingia ilikuwa ambayo ilikuwa na namba ngeni!.

Ilikuwa sauti ya kike ikiniambia"Halloo mambo".

Nilijibu"Poa,nani?".

Akaendelea kujibu "Mimi .......(alikuwa yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu).

Nilimwambia "Ooh mambo".

Aliniuliza "kwani........(dereva)hakukupa namba yangu?".

Nikamjibu "hapana,maadamu wewe umenipigia nitaisevu mama".

Akaniambia "Ok sawa,lakini nilikuwa nina jambo nataka kukwambia,tafadhali kama hutojali".

Nilimwambia "Ondoa shaka wewe niambie mama".

Aliniuliza "Yule rafiki yangu niliyekuja naye kwako unamkumbuka?".

Nilimuuliza "Si scolastica au?".

Aliniambia "Eenh huyo huyo".

Nikamwambia "Ok namkumbuka vipi kwani kafanya nini?".

Aliendelea kuniambia "Basi mwenzio anakupenda na anashindwa kukwambia nikaona mimi nikwambe badala yake".

Moja kwa moja nikajua tayari yule mwanamke alikuwa ameshapagawa na maisha niliyokuwa nikiyaishi.

Nilimwambia "Daaah sasa itakuwaje?"

Akauliza "Kwanini?"

Nilimwambia "mimi nakupenda wewe sana na bahati nzuri umenipigia simu nimepata wasaa mzuri wa kukueleza hisia zangu".

Japo pia scolastica alikuwa mwanamke mzuri sana,lakini mimi nilikuwa ninampenda huyo mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu.

Akaendelea kuniambia "sasa itakuwaje jamani maana mwenzako nimeolewa".

Niliendelea kumshawishi ili akubali kila nililomwambia "Mimi sitaki kukuoa ila nataka tuwe tunapiga starehe tu na chochote utakacho nitakupa,kuhusu rafiki yako wewe nitumie namba yake nitajua namna ya kumwambia".

Kwenye mawazo yangu nilikuwa nataka niwacharaze bakora wote wawili pasipo kufahamu!.

Aliniambia "Basi sawa nakutumia ila usimvunje moyo na kuhusu mimi tafadhali usije ukamwambia kwamba tunatoka wote maana anaweza nichukia kwamba nilimgeuka".

Nilimwambia aondoe wasiwasi maana sita mvunja moyo bali atanielewa tu,pia nilimkubalia yote aliyonieleza kwamba uhusiano wetu uwe wa siri.Nilipanga baadae ningempigia Scolastica!,nilikaa pale sebuleni nikiangalia luninga na hatimaye usingizi ukanichukua!.Ndipo nilionyeshwa maeneo ambayo inapaswa kwenda kwa siku ambayo ingefuatia kutoa kafara.Nilionyeshwa eneo la Buhemba ambayo sasa nadhani liko Wilaya ya Butiama ila zamani ilikuwa wilaya ya Musoma vijijini,hilo ndilo eneo ambalo ilipaswa mimi na hao wenzangu ambao sikuwafahamu mpaka wakati huo ilipaswa twende hapo tukafanye tukio,nilionyeshwa kwamba tutakapofika hapo ilitupasa kukaa kati ya Buhemba na Kiabakari yaani katikati ya hayo maeneo mawili,pale ambapo tulitakiwa kwenda kufanya tukio kulikuwa na mteremko kwa kila upande wa barabara na kulikuwa kuna daraja ambalo halikuwa kubwa sana.Nilishituka na kuelekea chumbani kulala,wakati huo nilikuwaga nachoka sana na sikufahamu sababu zilizokuwa zinapelekea mimi kuchoka!.Kila kitu kilichopaswa kifanyike kwenye ile kafara nilikiona ndotoni.

Sasa siku iliyofuata kwakuwa ndiyo ilikuwa ya kwenda kwenye eneo la tukio,nilielekea kule kwenye chumba cha siri ambako zilikaa zana za maangamizi.Hili tukio nakumbuka nilienda kulifanya siku tatu za mwezi uliofuata maana zile tarehe za kawaida za kutoa kafara zilikuwa zimepita,sikuogopa chochote kwasabau Malikia alikuwa ameniambia nijiandae kwa ajili ya hili tukio tu,hivyo na mimi nilitii!.Nilipomaliza kujiandaa kama kawaida niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi na kueleza ya kwamba natakiwa niwe eneo la tukio la siku hiyo.Ghafla nilijikuta nipo lilelile eneo nililoonyeshwa ndotoni,nilipofika hapo kuna watu niliwakuta wakiwa uchi kama walivyozaliwa.Walikuwa wanawake wawili na mwanaume mmoja,huyo jamaa niliyemkuta hapo baadae nilikuja kumfahamu,kwani alikuwa tajiri maarufu pale Mwanza aliyekuwa akimiliki mijengo kadhaa katikati ya jiji.Majengo yake walikuwa wamekodi watu mbalimbali kwa ajili ya biashara,alikuwa ni tajiri mkubwa sana pale Mwanza na mpaka sasa ninapoandika bado yupo anaendelea kudunda na huo utajiri wake!,watu wengi wanamfahamu na kama nikimtaja watu hawatoamini!.Wale kina mama sikuwahi kuwaona mara baada ya lile tukio,sikufahamu wao walitoka wapi,Kama nilivyosema hapo awali kwamba tuliambiwa kwamba kila tutakachokiona ikawe ni siri ya kila mtu,hatukupaswa kusema ya mtu yeyote na mwenzako na yeye hakupaswa kusema ya kwako!.Hayo ndiyo yalikuwa masharti ya wakati huo nikimtumikia shetani.

Kwasasa nimeshamfahamu Yesu kristo na nimesha achana na mali za Ibilisi ila sitoweza kumtaja mtu maana watu wengi wanasoma humu ndani hivyo sikutotaka kutaja baadhi ya majina ya watu kwasababu kama mnavyoelewa mtu anaweza kwenda kukushitaki kwa kumuita mchawi na ukiambiwa uthibitishe mahakamni ukakosa uthibitisho hivyo ikanigharimu kwenda jela bila sababu za msingi!.Mtu atakaye itaji nimtajie nitamtajia lakini kwa masharti maalumu.Na ndiyo maana hata wale matajiri ambao wanaendelea kutesa mjini Dar es salaam kwa mali za kishirikina ambao niliwakuta Ziwa Tanganyika na nikawashuhudia kwa macho yangu sikuweza kuwataja,tena ni watu maarufu sana na kuna mmoja naona alianziaha mpaka kanisa ili kuendelea kuzuga!,huwa naangaliaga hata hao waumini wake nabaki nawasikitikia tu!.

Hivyo basi hao watu nikawakuta hapo pamoja na mimi tukawa watu 4,tofauti yao na mimi ni kwamba,mimi nilikuwa nimevaa nguo japo zilikuwa za kishirikina na wao walikuwa uchi kama walivyozaliwa.Basi nikawasogelea pale,tulikuwa hatuongeleshani kwa maneno bali tulikuwa tunapeana ishara tu!,Wenzangu wao hawakuwa na vibuyu na sikufahamu kazi yao kubwa ilikuwa ni nini,lile barabara kipindi hicho lilikuwa linajengwa maana kwa pembeni kidogo kulikuwa kuna mitambo ya ujenzi wa barabara.Basi kwa mbali nikaliona basi nililionyeshwa ndotoni likiwa linakuja,kugeuka kulia pia kuna basi jingine lilikuwa linakuja ambalo pia nilikuwa nimeonyeshwa!.Yale magari yaliposogea karibu ndipo nikagundua kwamba ni moja lilikuwa Bus la kampuni ya Mwanza Coach na jingine lilikuwa Bus la J4!.

Mwanamke mmoja akanifanyia ishara kwamba nikae tayari na nikiandae kile kibuyu kwa ajili ya damu,yule mwanamke mwingine aliyebaki alienda kusimama katikati ya barabara pale darajani,akafanya mambo yake pale na alipomaliza akatoka akasimama kando,yale magari yalipokaribiana yalijikuta spidi inaongezeka mara dufu,ndipo yaligongana uso kwa uso,sikutaka kupoteza muda nikachukua kibuyu changu kama kawaida nikaanza kuweka damu!.Sasa kitu ambacho nilikuja kugundua ni kwamba wale watu niliyowakuta pale walikuwa na nguvu za ziada maana walitumwa hapo kwa kazi hiyo tu,mimi niliyekuwa na kibuyu kazi yangu ilikuwa ni kuweka damu za kafara ndani ya kile kibuyu tu!.Kiukweli wakati ule nilikuwa sinaga huruma kabisa nikiwa eneo la tukio maana nilifahamu ningejidai nina huruma ningetolewa kafara mimi.

Yule jamaa ambaye baadae nilikuja kumfahamu kama tajiri wa hapo Mwanza yeye alikuwa na kazi ya kuwaponda vichwa na kuwamalizia wale wote waliopaswa kufa,wale kina mama wao kazi yao ilikuwa ni usalama wa lile eneo la tukio yaani haikutakiwa kiumbe yeyote wa kishirikina awepo pale tofauti na sisi!,Kìukweli watu wengi walikufa kwenye ile ajali,ile ndiyo ilikuwa ajali yangu kubwa kuifanya wakati huo wa ushirikina,ilikuwa ajali ya kikatili sana naya kutisha maana watu wengi wasiyokuwa na hatia walipoteza maisha yao hapo,kwa upande wangu nilifurahi sana maana nilijua sasa Malikia angeenda kuniruhusu kuiafanyia maendeleo ile pesa!.Baada ya kukusanya damu za kutosha na kuona imefikia kipimo kilichohitajika,wale akina mama walinifanyia ishara ya kuondoka hapo eneo la tukio haraka!,sikutaka kabisa kupoteza,niliushika mkono uliyokuwa irizi na kutamka ya kwamba inapaswa niwe mle chumbani.Niliweka kile kibuyu palepale kilipokuwa kinakaa nikarudi zangu chumbani.

Niliporudi nilimkuta yule binti sebuleni akaniuliza "Kaka nilikuwa nakutafuta sijakuona kumbe ulikuwa chumbani huko,maana nimegonga sana chumbani kwako sikukuona,chakula kipo tayari?"

Nilimwambia "Nilikuwa nafanya ibada ndiyo maana ulikuwa unaona kimya,mara nyingi nikiwa kwenye ibada huwa sitaki usumbufu".

Nilimwambia "Basi niandalie hicho chakula nile".

Niliamua kumdanganya maana sikutaka kabisa yule binti aelewe kitu chochote kilichokuwa kinaendelea.Sasa ilipofika usiku wa saa 6 nilisikia sauti ya Malikia kama kawaida ikiniita kule kwenye chumba cha siri,nilipotoka ili niendee kule chumbani nilimkuta yule binti dinning room akijisomea maana mitihani ya kumaliza form 4 ilikuwa karibu!.

Nilimwambia "mimi naenda kufanya ibada hivyo tafadhali kama unashida utanisubiri nimalize!".

Nilimuaminisha tangia awali kwamba kile chumba nilikuwa naingia kufanya ibada,kwakuwa hata maongezi ambayo tungeenda kuongea na Malikia sikuwa na wasiwasi maana alikuwa hana uwezo wa kusikia chochote.

Niliufungua ule mlango wa kile chumba cha siri na kuingia ndani!.

Itaendelea.................
 
Hivyohivyo tutasoma mkuu [emoji847]
Kwanza mwanae yupo humu humu jf hivyo itaniletea shida mkuu ila kitu nilichojifunza ktk haya maisha usione watu wanatanua na mandinga ya maana ukazani ni Mungu aliwabariki hapana.

Kama si za kishirikina hizo basi tambua huyo naye ni fisadi anaiba serikalini ambayo nayo inatoa kafara kimtindo, halafu kitu ambacho nawashangaa watu wanao miliki pesa ambazo si za harali huwa wanajisahau sana.

Pia sisi pale walikua wanachukua damu kwa njia kichawi yaani ukiwa umelala
 
Mkuu bwana sasa huyo mwanae anakujua kama wewe ndio unatumia hii I'd
 
Kwanza mwanae yupo humu humu jf hivyo itaniletea shida mkuu ila kitu nilichojifunza ktk haya maisha usione watu wanatanua na mandinga ya maana ukazani ni Mungu aliwabariki hapana.

Kama si za kishirikina hizo basi tambua huyo naye ni fisadi anaiba serikalini ambayo nayo inatoa kafara kimtindo, halafu kitu ambacho nawashangaa watu wanao miliki pesa ambazo si za harali huwa wanajisahau sana.

Pia sisi pale walikua wanachukua damu kwa njia kichawi yaani ukiwa umelala

Usitaje majina
Wewe tupe mkasa tu
 
tulio poteza ndugu zetu kwenye ii ajari tuta kutaftaView attachment 1717119
Ndugu zangu naona nimeanza kuwachefua watu,kama nilivyosema hapo mwanzo ya kwamba hayo yalikuwa ni maisha ya zamani ambapo nilikuwa nikimtumikia Ibilisi kuliko sababishwa na kupenda mali za bure.Hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye niliyatambua makosa yangu nikatubu kwa Mungu wa Mbinguni,hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye ninamuabudu Mungu na wala si shetani.

Naombeni mnisamehe kwa wote ambao niliwagusa moja kwa moja.

Ili nisiendelee kuleta taharuki kwa watu ni vema nikaishia hapa ndugu zangu maana huko mbele nisije fanya watu wakakosa amani kabisa.
 
Sema nin boss yaani ni katika harakati za life huwez mfurahisha kila mtu ko samehe tu ndugu yangu ndo Mana jamaa anajaribu kuonyesha kwamba saivi kabadilika ujue kuweka wazi vitu ka hiz lazma uwe umejikana na kukubali liwalo na liwe yaan
 
Ndugu zangu naona nimeanza kuwachefua watu,kama nilivyosema hapo mwanzo ya kwamba hayo yalikuwa ni maisha ya zamani ambapo nilikuwa nikimtumikia Ibilisi kuliko sababishwa na kupenda mali za bure.Hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye niliyatambua makosa yangu nikatubu kwa Mungu wa Mbinguni,hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye ninamuabudu Mungu na wala si shetani.

Naombeni mnisamehe kwa wote ambao niliwagusa moja kwa moja.

Ili nisiendelee kuleta taharuki kwa watu ni vema nikaishia hapa ndugu zangu maana huko mbele nisije fanya watu wakakosa amani kabisa.
Lwanda eeh wee endelea ndugu ujue tunapata funzo huyo Mr. Shetan achana nae asikutishe Wala nini
 
Ndugu zangu naona nimeanza kuwachefua watu,kama nilivyosema hapo mwanzo ya kwamba hayo yalikuwa ni maisha ya zamani ambapo nilikuwa nikimtumikia Ibilisi kuliko sababishwa na kupenda mali za bure.Hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye niliyatambua makosa yangu nikatubu kwa Mungu wa Mbinguni,hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye ninamuabudu Mungu na wala si shetani.

Naombeni mnisamehe kwa wote ambao niliwagusa moja kwa moja.

Ili nisiendelee kuleta taharuki kwa watu ni vema nikaishia hapa ndugu zangu maana huko mbele nisije fanya watu wakakosa amani kabisa.

Huyo ana kuzingua wewe ulishafanya toba kwa Mungu hio inatosha
Hebu tuendelee mkuu mbona kutesana hivi story za jf jamani [emoji51][emoji51][emoji51]
Shusha vitu tunaendelea kufatilia
 
Ndugu zangu naona nimeanza kuwachefua watu,kama nilivyosema hapo mwanzo ya kwamba hayo yalikuwa ni maisha ya zamani ambapo nilikuwa nikimtumikia Ibilisi kuliko sababishwa na kupenda mali za bure.Hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye niliyatambua makosa yangu nikatubu kwa Mungu wa Mbinguni,hivi sasa mimi ni mtu mpya ambaye ninamuabudu Mungu na wala si shetani.

Naombeni mnisamehe kwa wote ambao niliwagusa moja kwa moja.

Ili nisiendelee kuleta taharuki kwa watu ni vema nikaishia hapa ndugu zangu maana huko mbele nisije fanya watu wakakosa amani kabisa.
Endelea lwanda wameshakusamehe
 
Back
Top Bottom