Mikasa ya wachungaji uchwara.

Ulirchdov

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2019
Posts
356
Reaction score
258
Salaam kwenu wakuu!!

Kuna kitu nimekuwa nikijiuliza lakini sipati jibu, ila nikaona ni vyema kuwashirikisha ili tuweze kujadili kwa pamoja.

Jambo ambalo limekuwa likinitatiza ni kuhusa hawa wachungaji wanaoibuka na kuanzisha makanisa lengo likiwa ni kuleta wokovu na kueneza injili ila nyuma ya pazia wachungaji hawa wamekuwa chanzo cha mikasa na matukio mbalimbali yenye kuleta wasiwasi katika jamii. Mfano, hivi juzi tu Kuna taarifa zilienea kuhusu mchungaji mmoja aliyewanyesha jiki waumini wa kanisa lake kitu kilichopelekea vifo vya baadhi ya watumishi waliotendewa jambo hilo. Kisa kingine ni kuhusu mchungaji aliyetumia mafuta ya taa kuondoa mapepo kwa mtu aliyeonekana kuhitaji msaada wa kiroho ili kuyashinda mapepo yaliyokuwa yakimsibu, kilichotokea mtu yule aliambulia majeraha.

Kuna wachungaji wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwafufua wafu wakiamini kuwa wana nguvu na imani ya kutosha kuwarejesha wafu katika ulimwengu huu waliokuwa wakiuishi kabla ya kupatwa na umauti.

Swali 1: Je, hawa wachungaji wanapingana na Mwenyezi Mungu ambae ndiye aliyetuumba na pia anao uwezo wa kututwaa kwa kutuletea umauti? kama tunavyoamini sisi wakristo na madhehebu mengine kwamba kila nafsi itaonja mauti kama ilivyoandikwa katika biblia takatifu ambayo mara nyingi wachungaji hawa wanaitumia.

Swali 2: Je, kama wamepewa uwezo wa kufufua mtu aliyekwisha kufa kutoka mavumbini kumrejesha katika dunia wanashindwa nini kuzuia kifo ili watu wasipatwe na umauti?
 
Hizi taarifa ni za uongo kabisa zenye lengo Si tu la kumchafua na Kumshushia heshima Gwajima Bali linachafua kanisa la Mungu kwa ujumla, hata kama Gwajima humpendi au sio mchungaji wako lakini kufurahia aibu na video hzi kwa Gwajima ikiwa ni Kuutukanisha Ukristo wako pia na kumtukana Mungu

Hivyo, Ikiwa kweli wewe ni mkristo wa kweli lazima utaukemea ushetani huu unaosambazwa na maajenti ya ibilisi kuuchafua ukristo kwa ujumla.Hivyo kushiriki kufurahia au kusambaza taarifa hizi chafu kwa kufurahia aibu hii kwa Gwajima ujue unashiriki kazi za shetani, na wewe ni mchafu wa namna hiyo hiyo.
 
Huu uzi niliuanzisha hata kabla huyo mchungaji hajafanya hayo uliyoyanena hapa kwahiyo weka mbali hisia zako mkuu hakuna mahali nimemtolea mfano gwajima wala hakuna sehemu niliyomtaja
 
Kwa maswali yako tu natilia mkazo kuwa utakuja kuwa mpagani one day, karibu ulimwengu wa ma-atheist mkuru!!
Nina wasiwasi na kazi wanayofanya wachungaji wanaoibuka kila siku ila sio kwamba maswali hayo niliyouliza yatanifanya niwe mpagani hapana na haitowezekana.
 
mzee mbona povu jingi sana,,mbona hakuna alipitajwa gwajima
 
Huu uzi niliuanzisha hata kabla huyo mchungaji hajafanya hayo uliyoyanena hapa kwahiyo weka mbali hisia zako mkuu hakuna mahali nimemtolea mfano gwajima wala hakuna sehemu niliyomtaja

Usione hofu kumtaja huyu nae ni wale wale.....me nimefika kwake pale ana makanisa zaidi ya 400 kwa mujibu wake ila kanisa mama lipo kama banda la kuku kwann asiuze chopa ajenge kanisa zuri
 
Nina wasiwasi na kazi wanayofanya wachungaji wanaoibuka kila siku ila sio kwamba maswali hayo niliyouliza yatanifanya niwe mpagani hapana na haitowezekana.
Kwan walio wapagani na nyie walokole mna tofauti gani? tena nafuu na atheist wao wanaishi pasipo kusukumwa kama mawe mlimani...!!
 
ni mazingaombwe tu hayo. ni yesu ndiye atakayekuja kuwafufua wafu!!
 
Soma biblia utaelewa unayotaka kuelewa
Mbali na hapo utapata majibu ya kilevi sababu nawe umeuliza huku umelewa
 
Kwan walio wapagani na nyie walokole mna tofauti gani? tena nafuu na atheist wao wanaishi pasipo kusukumwa kama mawe mlimani...!!
Usibashiri imani na dhehebu langu mkuu
 
Sijawai kuwa na imani na hizi ministry na makanisa ya kilokole pia.
 
Hakuna Wachungaji Uchwara Hao wanafuata Injili kama walivyo magaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…