Ulirchdov
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 356
- 258
Salaam kwenu wakuu!!
Kuna kitu nimekuwa nikijiuliza lakini sipati jibu, ila nikaona ni vyema kuwashirikisha ili tuweze kujadili kwa pamoja.
Jambo ambalo limekuwa likinitatiza ni kuhusa hawa wachungaji wanaoibuka na kuanzisha makanisa lengo likiwa ni kuleta wokovu na kueneza injili ila nyuma ya pazia wachungaji hawa wamekuwa chanzo cha mikasa na matukio mbalimbali yenye kuleta wasiwasi katika jamii. Mfano, hivi juzi tu Kuna taarifa zilienea kuhusu mchungaji mmoja aliyewanyesha jiki waumini wa kanisa lake kitu kilichopelekea vifo vya baadhi ya watumishi waliotendewa jambo hilo. Kisa kingine ni kuhusu mchungaji aliyetumia mafuta ya taa kuondoa mapepo kwa mtu aliyeonekana kuhitaji msaada wa kiroho ili kuyashinda mapepo yaliyokuwa yakimsibu, kilichotokea mtu yule aliambulia majeraha.
Kuna wachungaji wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwafufua wafu wakiamini kuwa wana nguvu na imani ya kutosha kuwarejesha wafu katika ulimwengu huu waliokuwa wakiuishi kabla ya kupatwa na umauti.
Swali 1: Je, hawa wachungaji wanapingana na Mwenyezi Mungu ambae ndiye aliyetuumba na pia anao uwezo wa kututwaa kwa kutuletea umauti? kama tunavyoamini sisi wakristo na madhehebu mengine kwamba kila nafsi itaonja mauti kama ilivyoandikwa katika biblia takatifu ambayo mara nyingi wachungaji hawa wanaitumia.
Swali 2: Je, kama wamepewa uwezo wa kufufua mtu aliyekwisha kufa kutoka mavumbini kumrejesha katika dunia wanashindwa nini kuzuia kifo ili watu wasipatwe na umauti?