Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
MKATABA WA KALE WA KIUCHUMI KATI YA ISRAEL NA LEBANON U SAWA NA MKATABA WA BANDARI KATI YA TANZANIA NA DUBAI?
Mkataba wa kwanza wa kimataifa kurekodiwa katika Biblia ni Mkataba wa kiuchumi baina ya Israeli na Lebanon uliosaniwa mwaka c. 950 BK (miaka 2973 iliyopita). Mkataba ule ulihusu Lebanon kuiuzia mbao Israeli ambayo ilizihitaji ajili ya kujengea Hekalu (1 Wafalme 5:1-18 na 2 Mambo ya Nyakati 2:-18).
Makubaliano au vipengere vya mkataba ule ni kama ifuatavyo: Lebanon iliweka masharti:
1. Lebanon ndiyo iliyokuwa ikitoa magogo ya mbao.
2. Wafanyakazi wa kukata magogo ya miti ni lazima wawe Walebanoni.
3. Kazi ya kusafirisha magogo kutoka katika mapori ya Lebanon hadi bandarini ifanywe na watu wa Lebanon.
4. Kazi ya kusafirisha magogo kutoka bandari ya Lebanon hadi Israeli ifanywe na meli za Lebanon.
5. Kazi ya kupasua magogo na kulanda mbao ndani ya ardhi ya Israeli ifanywe na Lebanon.
6. Israeli itoe chakula kwa ajili ya Ufalme wa Lebanon katika kipindi chote cha mkataba.
Kwa upande wa Israeli pamoja na kutoa ngano, mafuta, na vyakula vingine kwa Lebanon kama malipo kwa ajili ya mkataba ule, nayo iliweka mapendekezo yafuatayo ili kuivutia Lebanon:
1. Israeli itatuma wafanyakazi wake pia kuwepo kila sehemu ya kazi
2. Waisraeli kwenda kufanya kazi Lebanon ni muhimu kwa ajili ya kuangalia usalama na ubora wa bidhaa.
3. Waisraeli kwenda kufanya kazi Lebanon ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanapata ujuzi wa kazi hizo. Ujuzi huo haukuwepo Israeli.
4. Lebanon ipeleke Israeli wataalam wa kukata dhahabu, fedha, Shaba, vyuma, nk. Lebanon pia itume wataalam Israeli uchoraji, uchongaji na usanifu wa michoro.
5. Wataalam hao katika kipengere cha 4 hapo juu lazima wafanye kazi pamoja na wataalam wa Israeli ili kuwajengea uwezo wataalam wa Israeli lakini pia kuhakikisha ubora wa kazi na usalama kwa Isareli.
6. Israeli kulipa mishahara ya wafanyakazi wote wa Lebanon pamoja na ya wafanyakazi wote wa Israeli watakaokuwa Lebanon.
7. Jumla ya wafanyakazi wa Israeli waliotakiwa kwenda Lebanon walikuwa 30,000 na kwamba wafanyakazi hao walikwenda kwa awamu.
Katika mkataba huo, Isareli ilijali sana ubora wa bidhaa, usalama wa Hekalu lao na kuhakikisha watu wao wanapata ujuzi. Lebanon waliangalia sana kupata Lebanon, wao waliangalia sana malipo stahiki kwa bidhaa zao, chakula kwa watu wao na ajira kwa vijana wao.
Mkataba ule pia uliweka ukomo wa muda wa muda ambapo ulikuwa ni muda wote wa ujenzi wa hekalu hadi kukamilika.
Je, unaweza kuchunguza vipengere vyoye vya mkataba huo na kulinganisha na vipengere vya mkataba wa sasa wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai? Je, ni vipengere gani vinafanana? Je, kuna tofauti gani iliyopo?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, ambaye ni mwandishi wa makala hii, ni Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani. Pia, ni mhadhiri wa Utafiti, Historia ya Kanisa (Ecclesiologia), Literature, Theologia, Falsafa, Missiologia, Missiologia, Dini za asili za Kiafrika (African tradition religions) na Soshologia. Amefundisha masomo hayo kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu, St. John's University of Tanzania.