Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
- Thread starter
- #21
Asante sana brother š.Hongera mkuu
Mimi mke wangu pia yupo mwaka wa mwisho.
Hongera kwako na kwake pia kiongozi, jitahidi tu awahi na Law School.
Vipi hapa kwetu katika mahakama za juu?
Kwakweli, mahakama yetu umepiga hatua kubwa sana katika hili, tuna tovuti mbalimbali zinazotuwezesha kupata mambo mbalimbali ya kisheria kwa sasa , hapa nitataja chache kutokana na umuhimu wake.
- Tunayo Tanzlii, hii imekua chanzo cha thamani kwa kupata hukumu za kesi zilizotolewa na Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Hata hivyo, kuna mwito wa kutaka maamuzi yaliyofanywa na mahakama za ngazi za chini kuanzia Mahakama ya Mwanzo, Wilaya, na zile za Hakimu Mkazi, kupatikana kwa urahisi mtandaoni ili kuongeza uwazi na ufikiaji.
- Ipo pia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Tovuti maalumu ya Sheria ya Bunge hizi zinatusaidia kupata Katiba na sheria zote za nchi. Japo changamoto inayojitokeza ni kwamba, sheria nyingi bado zinapatikana kwa lugha ya Kiingereza, jambo linaloleta ugumu kwa watumiaji wasio wanasheria. Hii inaashiria haja ya kutafsiri sheria hizi muhimu katika lugha ya Kiswahili ili kuhakikisha kila mwananchi anaweza kuzielewa na kuzitumia ipasavyo.
- Nyingine ni e-Wakili inayojulikana pia kama āmjue wakiliā, inatoa mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama na uhakiki wa taaluma ya uwakili. Inawezesha mtu kuthibitisha iwapo mtu anayedai kuwa wakili ni sahihi au la, hivyo kuzuia udanganyifu na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za kisheria kutoka kwa wataalamu waliothibitishwa na si matapeli/ vishoka.