Bodhichitta
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 315
- 762
UTANGULIZI
Kama tujuavyo sekta binafsi imekuwa na mchango katika ukuzaji wa uchumi wa nchi yetu, lakini mbali na hilo ni mdau mkubwa sana wa utoaji wa ajira nchini hususani kwa kipindi hiki ambacho nchi yetu imekumbwa na kadhia kubwa ya ukosefu wa ajira kwa wahitimu na vijana kwa ujumla. Hivyo basi mbali na changamoto zake sekta binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa ajira. Kwa mfano mwaka 2020 sekta binafsi imeajiajiri takribani watu 280,941 sawa na 47.22% za ajira zote zilizotelewa (chanzo: Ofisi ya waziri mkuu-kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu).
Hivyo basi kama tujuavyo kuwa rasilimali watu ndio kiungo muhimu sana katika hizi sekta katika uzalishaji na utoaji huduma kwa lengo la kutengeneza faida, hapa ndipo panapokuja suala la makubaliano/mkataba baina ya mwajiri na mwajiriwa ili kutengeneza usawa na haki baina yao.
Makala hii tutaangalia Zaidi mikataba ya ajira pamoja na changamoto zinazowakumba waajiriwa katika mikataba hiyo.
MKATABA WA AJIRA
Ni makubaliano yenye nguvu kisheria baina ya mwajiri na mwajiriwa juu ya utekelezaji wa kazi au majukumu kwa kipindi husika. Kuna aina tatu za mikataba ambazo ni; - mikataba ya kudumu, Mikataba ya muda na mikataba ya kazi maalum. Ambapo pande zinazoingia kwenye mikataba zinaweza kuchagua kulingana na muda au majukumu ya kazi.
Mkataba lazima ufuate vigezo maalum vinavyotakiwa kuzingatiwa pande zote zinazoingia mkataba ili yawe makubaliano yenye nguvu kisheria, vigezo hivyo ni kama vile utashi huru, pande zote ziwe na uwezo wa kuingia makubaliano, mbadilishano wa thamani unaokubaliwa kisheria na jambo la makubaliano liwe linakubalika kisheria.
Mikataba ya ajira ni mikataba kama mikataba mingine hivyo husimamiwa na sheria ya mikataba lakini pia sheria mahususi ambayo husimamia mikataba hii ni sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004.
CHANGAMOTO ZA MIKATABA YA AJIRA KATIKA SEKTA BINAFSI
Zipo changamoto nyingi zinazokumba sekta binafsi hasa kwa upande wa wafanyakazi kama vile ukiukwaji wa haki za wafanyakazi, malipo yasiyoridhisha, kufanyakazi nje ya masaa ya kazi bila malipo na mengine mengi ambayo haya yote hutokea kwa kutokuwa mikataba ya ajira au mikataba mibovu ya ajira.
Changamoto za mikataba inaweza kujadiliwa kwa kuangalia vipengele vifuatavyo;-
i. UPATIKANAJI/UINGIAJI WA MIKATABA YA AJIRA
Hii ni hatua ambapo mwajiri na mwajiriwa wanatakiwa kuingia mkataba inayohusu kazi waliyokubaliana, changamoto kubwa iliyopo katika kipengele hiki ni kuwa waajiri huwa hawatoi mikataba hii kwa waajiriwa wao au hutoa kwa kuchelewesha kwa sababu tofauti ikiwemo kuepuka kuwajibika na mikataba hiyo au kutengeneza mazingira ya kunyonya nguvu kazi ya mwajiriwa au kukwepa baadhi ya kodi na michango kutoka kwenye mamlaka husika kama vile TRA (PAYE&SDL) na mifuko mbalimbali ya jamii kama NSSF.
Changamoto hii hufanya wafanyakazi kupoteza haki zao lakini pia serikali kupoteza baadhi ya mapato
kutoka kwenye hizi sekta.
ii. MAUDHUI YA MIKATABA
Haya ni makubaliano au vipengele vilivyopo ndani ya mikataba, kwakuwa muandaaji wa hii mikataba ni mwajiri hivyo hii mikataba huwa haiakisi hali halisi ya mazingira ya kazi, vipengele vingi vya mikataba haviwekwi wazi au kufafanuliwa kwa muajiriwa lakini pia baadhi ya mikataba huandikwa kwa lugha ambayo mwajiriwa hana ufahamu nayo hivyo mwaajiriwa kuingia mkataba ambao hajauelewa.
Changamoto hii humfanya mwajiriwa kupoteza haki zake za msingi hasa kwenye mamlaka za usuluhisho wa migogoro kama vile mahakamani.
iii. UTEKELEZAJI WA MIKATABA
Hiki ni kipengele ambacho pande zilizoingia mkataba hutekeleza majukum na wajibu wake kulingana na makubaliano, ila kwa upande wa mwajiri anaweza kutekeleza machache anayoona yanampa manufaa kwake, kwa mfano suala la mazingira ya usalama kazini waajiri wengi huwa hawaangalii sana mazingira ya usalama kwa wafanyakazi kuhusu afya na uhai wao.
Changamoto hii huweza kuleta madhara kwa wafanyakazi kama vile kupata ulemavu wakudumu, maradhi na hata vifo vilivyosababishwa kazini.
iv. USITISHAJI/UKOMO WA MIKATABA
Katika usitishaji wa mikataba uko wa namna mbili: - usitishaji kabla ya muda na usitishaji wa baada ya muda ulioko kwenye mikataba kukamilika. Katika sekta binafsi kuna usitishaji kiholela wa mikataba kabla ya muda uliopo kwenye mikataba bila sababu ya msingi na hii hutumika kama njia ya kuziba midomo ya wafanyakazi pale tu wanapodai haki zao kutoka kwa mwajiri.
Pia mwajiri huwa hafuati utaratibu wa kisheri kwenye kusitisha mikataba hiyo kama ilivyoanishwa kwenye kifungu namba 41(1) katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004.
Hii hufanya wafanyakazi wengi kuwa kimya hata pale wanapoona haki zao zinakiukwa ili kutetea ajira zao.
V. MALIPO
Waajiri wamekuwa wakiwasumbua wafanyakazi kwenye haki zao mara baada ya kusitisha mikataba yao, malipo kama vile sehemu ya mshahara (kama mkataba umesitishwa kabla ya mwezi kukamilika), likizo, kiinua mgongo, usafiri na mengine kama yalivyoelezwa katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu na 42, 43, na 44.
MAPENDEKEZO
Nini kifanyike kwa upande wa serikali pamoja na wadau wengine ili kuondoa hizi changamoto za mikataba ili kuleta haki na usawa katika hizi ajira;-

- Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 ifanyiwe marekebisho ili kubainisha wazi muda wa majaribio kwa mwajiriwa.
- Kupitiwa upya kwa kifungu namba 41(1) cha Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004, ambacho kinamtaka mwajiri kumlipa kiinua mgongo cha walau malipo ya wiki moja katika mshahara wake wa mwezi kwa mwaka, nabadala yake mwajiri alipe kiunua mgongo cha walau mshahara wa mwezi mmoja kwa mwaka mara miaka aliyokaa kazini.
- Vyombo vinavyohusika katika utatuzi wa migogoro inayohusu mikataba ya ajira itende au isimamie haki katika pande zote mbili kwa kuanza kupitia uhalali wa mikataba yao.
- wizara na mamlaka zinazosimamia hizi sekta ni lazima zihakikishe au kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika sehemu zao za kazi ili kuangalia utekelezaji wa hizi sheria hususani sheria ya mikataba.
- Kuwepo na chombo mahususi cha serikali ambacho kitakuwa karibu na hizi sehemu za kazi ili kuangalia mienendo ya wafanyakazi mara kwa mara, kama vile katika ngazi kijiji au kata ambapo mwajiri anafanya shughuli zake.
HITIMISHO
Mbali na changamoto zake pia sekta binafsi zina mchango mkubwa kwenye ajira hususani kwenye hiki kipindi ambacho kuna changamoto kubwa za ajira nchini, serikali haina budi kuweka mazingira mazuri ya sheria pamoja na miundombinu ili kuendelea kushirikiana vyema na hizi sekta.
Upvote
2