mikataba ya bodaboda

mikataba ya bodaboda

zipeda

Member
Joined
Sep 12, 2013
Posts
30
Reaction score
5
Hello! Nataka kuanzisha biashara ya kununua pikipiki za usafiri kisha kukodisha kwa waendeshaji bodaboda hizo kwa makubaliano ya kila siku akipaki pikipiki hiyo arejeshe Tshs. 10,000 na baada ya mwaka 1 bodaboda hiyo itakuwa ya kwake, je mkataba wa biashara ya kukodisha bodaboda hiyo kwa makubaliano mazuri yenye dhamira ya kujenga uhusiano mzuri kisheria unatakiwa uweje au uwe na vitu gani, nikipata nakala nitashukuru zaidi.:A S kiss:
 
makubaliano ya kila siku akipaki pikipiki hiyo
arejeshe Tshs. 10,000 na baada ya mwaka 1 bodaboda hiyo itakuwa ya
kwake,

10000x30=300000.
300000x12=3600000.
bodaboda inauzwa 1.6 >2m!
faida zaidi ya 2m kwa mwaka,na wewe umekaa nyumbani tu na mkeo wakati dereva bodaboda anapishana na,
1.magari.
2.majambazi au vibaka
3.Polisi.
na matatizo mengne kibao!
ajiri mwanao.
 
Lakini kama baada ya Mwaka anamuachia Bodaboda ni fair business, kuna watu marejesho ni elfu 10 kwa siku na bado hakuna makubaliano ya kuachiwa bodaboda hata baada ya miaka miwili..
 
haijalishi nani ataendesha but nahitaji kujua kuhusu mkataba na nikifanikiwa kupata copy itapendeza zaidi na nitashukuru xana, haya wanajamvi tuendelee kutiririka great thoughts pia ruksa kujadili kuhusu business hii
 
Mkuu kwa ushauri kabla hujafunga hiyo mikataba kwanza tafuta polisi mmoja kwa ajili ya kazi ya kuwatishia tu jamaa,maana nawajua wabongo,
Pili wazo zuri sana hilo,sio kwamba vijana wote ni matapeli wapo wenye shida na wanajua maisha na wanatafuta maendeleo pia,ila angali kwenye kiwango ulichoweka ni juu sana punguza,ila kila kheri
 
Jamani tuwe na huruma hata kama tunataka kuwasaidia, 10,000 kila siku kwa bodaboda ni nyingi sana. Kama unabisha jaribu wewe mwenyewe uendeshe uweke mafuta, ule na upate hiyo ela kila siku.
 
Jamani tuwe na huruma hata kama tunataka kuwasaidia, 10,000 kila siku kwa bodaboda ni nyingi sana. Kama unabisha jaribu wewe mwenyewe uendeshe uweke mafuta, ule na upate hiyo ela kila siku.

Mkuu kwa mtu siriazi hiyo pesa ni kidogo sana, may be hujui wanapata sh ngapi, wanapata sana pesa na uzuri wa hii kitu ni ulaji wake wa mafuta
 
Hello! Nataka kuanzisha biashara ya kununua pikipiki za usafiri kisha kukodisha kwa waendeshaji bodaboda hizo kwa makubaliano ya kila siku akipaki pikipiki hiyo arejeshe Tshs. 10,000 na baada ya mwaka 1 bodaboda hiyo itakuwa ya kwake, je mkataba wa biashara ya kukodisha bodaboda hiyo kwa makubaliano mazuri yenye dhamira ya kujenga uhusiano mzuri kisheria unatakiwa uweje au uwe na vitu gani, nikipata nakala nitashukuru zaidi.:A S kiss:
Suala la mokataba Mkuu ni la kisheria.Unapaswa kutafuta Wanasheria wakutengenezee mikataba.Usipende vya bure. Kama uko tayari,tuwasiliane niitumikie tasnia yangu ya Sheria
 
hicho unachotaka ni cha kisheria zaidi nipigie 0713463004
 
Back
Top Bottom