SoC03 Mikataba ya kazi iwekwe kwenye lugha mbili

SoC03 Mikataba ya kazi iwekwe kwenye lugha mbili

Stories of Change - 2023 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
Katiba ya nchi yetu inatambua lugha ya kiswahili kama lugha rasmi ya taifa la Tanzania, bado inashangaza sana kuona mikataba ya kazi inaandikwa kwa lugha ya kingereza tu, kwa kutumia jicho la kiupembunzi kupitia visa mafunzo kulingana na masuala ya mikataba suala la kuandaa mikataba liwe na ulazima wa kutumia kwa lugha ya kiswahili kama sio kwa lugha zote mbili, yaani mkataba mmjoa huwe kwa lugha ya kingereza na mwingine kwa lugha ya kiswahili kulingana na matakwa ya mwajiriwa/mteja.

“kusema mwingine sina maana mikataba hiwe ni mikataba miwili tofauti bali mkataba mmoja huwe katika tafsiri mbili”.

“Mtu mwenye anayetia saini bila kulazimishwa, kushurutishwa, kufichwa wala kushawishiwa hawe na maamuzi ya kuchagua lugha gani anaipa kipaumbele kabla ya kuanza kusaini mkataba wa kazi” kulingana na uelewa wake.

Hii ya kuwa na mikataba miwili kwa lugha mbili zenye maana sawa kuanzia neno kwa neno hadi maana ya jumla litamlinda hata mtu anayetoka nje ya nchi na hasiyejua lugha ya kiswahili pia na yule anayejua lugha kiswahili kutoka ndani ya nchi kuliko hile lugha ya kingereza.

Vitabu vya dini na vile vinginevyo vimetafsiriwa vizuri kutoka kwenye lugha za kigeni, kupitia hatua hizi sioni ushindikano unaofanya tusipate tafsiri sahii ya maneno ya kiswahili kutoka kwenye vifungu vya sheria hususani zile zinazohusu masuala ya mikataba hasa zilizoandikwa kwa lugha ya kingereza.

Hapa nchini vimesikika vilio vingi vya wachezaji wa mpira, wasanii na baadhi ya watengenezaji wa kazi za kibunifu wakilalamikia mikataba yao kuwa inawafunga na pengine kuwanyima haki zao za msingi ya wao kutia saini kwa pupa kulingana na shida walizonazo na kushindwa kusoma na kutafsiri vizuri baadhi ya vifungu vyake kwa sababu ya kuandikwa kwa lugha ya kingereza huku mwajiri akitumia fimbo hii katika kumkandamiza na kumyonya.

Wizara ya sheria na katiba kwa kushirikiana na baraza la kiswahili Tanzania wawajibike kwa pamoja katika kutafsiri mikataba ya kazi ya watumishi iliyopo na hile mipya kabla ya kutiwa saini na sio tu mikataba ya watumishi bali na mikataba ya mauziano pamoja na manunuzi au kandarasi.

Pia kwenye taasisi binafsi nako paguswe na takwa la hili la mikataba kuwa katika lugha mbili kwa madhumuni ya kumlinda mteja.

Ili kulinda takwa hili, sheria iweke kipengele cha kusisitiza utiwaji wa saini katika mikataba ufanyike baada ya mkataba kutafsiriwa katika lugha mbili moja iwe ya kiswahili na lugha ya pili iwe ya kingereza ili kulinda maslahi ya pande mbili na hata wanaotoka nje ya nchi.

Mapungufu mengi ya kutia saini kwenye mikataba mibovu linachagizwa na lugha hivyo watu wamekuwa na utaratibu wa kutosoma wala kuelewa kilichoandikwa.

Vile katika hili waajiri wamekuwa kama warubuni wa kuwafanya watu wasaini mikataba bila ya kuisoma kwani ni jambo la utata kutia saini ndani ya muda mfupi ambopo suala hili linahita muda mrefu wa kupitia kila kipengele na kwa utulivu. Katika kuliepusha hili jambo inabidi kuwepo na kipengele cha kumpa kipaumbele mwajiriwa kwa kumpatia muda wa masaa 24 ya kupitia na kupembea vivuli vya mkataba kabla ya kutia saini.

Mfano 1; Machifu wetu waliosaini mikataba na wakoloni, elimu ya kusoma waliipata wapi hadi kufikia maamuzi ya kutia saini na kama walikuwa nayo iliendana na lugha za kimkataba?

Mfano 2; Nilisikiliza na kufuatilia mgogoro wa mcheza maarufu hapa nchini Feisal “fei toto” yeye alipokuwa anahojiwa na kituo kimojawapo alikiri wazi kuwa lugha ilimpa kikwazo na kujikuta anatia saini mbali na matatizo mengine.

Mifano hii midogo pengine inatokea kwa makusudi ili kutufumbua macho watanzania katika kuelekea kwenye mikataba yenye maslahi ya kitaifa.

Pia tafsiri sisi ya mtu mmojammoja kutoka kwenye mikataba ya kingereza imekuwa ikipotosha na kupotoshwa hata pengine kuwa kivuli cha kuwakandamiza watu wanahoji masuala ya msingi kwani kila mmoja anatafsiri kulingana na uelewa wake na kuleta mkanganyiko wa maana iliyokusudiwa “tusirudie makosa ya mababu zetu” . Na pengine kumshinikiza anayehoji aonyesho neno lenye maana iliyotafsiriwa bali tafsiri iwe ni moja.

Mbali na mapungufu ya kimkataba yanayosababishwa na lugha nigependekeza mikataba hata inayogusa nchi au mtu binafsi iwe na kipengele cha kumtaka mwajiri/ mtoa mkataba kuwajibika kimkataba pale mkataba utakapoonekana una viashiria vya “Unyonyaji”, hiwe kwa kuuvunja au kwa kutumia njia nyingine ya kupata suruhu.

Endapo suala hili litapewa kipaumbele litatoa mwanya kwa wananchi kujadili na kupembembua kiyakinifu mikataba inayogusa nchi tofauti naya mtu binafsi kwani watakuwa na uwezo wa kujenga hoja na kuitetea kwa maslahi mapana ya nchi baada ya kuwekwa adharani.

Hivyo basi ili kuondoa mkanganyiko huu ni suala la mkata kuandikwa kwa lugha mbili zenye maana sawa kuanzia neno kwa neno hadi kwenye maana ya jumla litaleta tija kubwa sana hapa nchini.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom