Rweyemamu Cleophace
New Member
- Jun 4, 2024
- 3
- 1
Utangulizi; Muda mrefu mfumo wa ufanyakazi kwa serikali umekuwa wa kuajiliwa jumla, jambo ambalo limekuwa likifanya watumishi wengi wafanye kazi kwa mazoea,wakose uadilifu nk. Yote ayo ni kutokana na wafanyakazi awa kuwa na uhakika wa kazi kwamba hata afanye kosa gani anajua ataendelea kuwepo kazini tu.
UHALISIA: Ni vigumu kuukwepa ukweli kwamba huu ni mfumo uliopitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya Dunia tuliyopo iliyojaa ushindani, zama za watumishi kufanya kazi kwa miaka 55 hadi 60 angali kuna wahitimu wanaomaliza elimu kila siku na kuambiwa awana uzoefu izo zama zimepitwa na wakati, Unawaambiaje vijana awana uzoefu wakati wenye uzoefu wapo makazini.
SULUHISHO: Tanzania tuitakayo ni Tanzania itakayotoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi; Wafanyakazi wapewe mikataba ya kazi kwa miaka kadhaa kuanzia 10 hadi 20 na watumishi waboreshewe maslahi yao naamini pesa na posho ambazo ungemlipa mtumishi kwa miaka 55 ukimlipa kwa miaka 10 na kuweka sheria kwa mifuko ya hifadhi itasaidia sana kuondoa changamoto ya ajira.
FAIDA: Faida ya mfumo huu wa kufanya kazi kwa mikataba inaanzia kwa watumishi wenyewe, mtumishi atakuwa na uwezo wa kumaliza kazi akiwa bado na nguvu kimwili na kifikra ivyo atatumia kiinua mgongo chake kujiwekeza na kiinua mgongo chake kikiw kizuri ataweza kutoa ajira pia kwa watu wengine.
2: Faida nyingine ni kwa serikali kutoa fursa ya ajira kwa vijana wanaokuwa wamemaliza masomo yao.
MWISHO: Ni matamanio yangu kuona Tanzania ijayo inakuwa bora na imara,naamini wazo langu likichukuliwa na kuboreshwa linaweza kuwa tiba kwa tatizo la ajira na ugonjwa huu unaoitwa uzoefu kwa watafuta ajira lengo letu ni kulijenga Taifa letu.
Ahsanteni Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.

Upvote
2