Kuna jambo nimeandika hapo juu, ila sidhani kama nimefafanua vizuri kwa kueleweka.
Nimeongelea tabia ya Wasanii kutothamini weledi na kupenda kusimama wao kama wao a.k.a umimi.
Weledi ninaozungumzia ni kwa Wasanii kutambua taaluma nyingine, watambue ya kwamba kwenye tasnia ya filamu wao ni sehemu tu ya timu kuubwa inayofanikisha kazi zao, na miongoni mwao ni kama ulivyotaja hapo enterntainment lawyers n.k.
Ukosefu wa weledi umewapelekea kutoshirikiana/wakaribisha wadau wengine muhimu, na ile michezo waliyokuwa wanafanya ya mtu mmoja kuwa Mwandishi, Cameraman, director n.k.
Wasipobadili matazamo na kuruhusu weledi watapiga marktime miaka nenda rudi....bila kusahau umoja, nguvu yao ndio itawapa maslahi na kuzuia wababaishaji kuwanyonya hao wenye vipaji vyao kama kina Mzee Majuto na wengine.
Sio rahisi kila Msanii kuwa na lawyer, ila kama chama/kikundi wanaweza kuwa na lawyers atakayesaidia kwenye mikataba n.k.
Ulichokisema nimekielewa sana. Ni kweli, suala la utumiaji wana-Sheria ni dogo sana and I doubt kama wapo wanaotumia.
Lakini vilevile tatizo linakuwa kubwa zaidi kwa sababu SYSTEM yenyewe haitoi STAHIKI zote anazostahili Msanii!
Hii maana yake ni kwamba; Producer/Film Company inaweza kukupa mkataba wa kisheria. Lakini kwavile System haitoi Stahiki zote anazo-deserve Msanii; basi utakuta mkataba husika tayari hauna baadhi ya Stahiki muhimu kwa sababu mfumo wenyewe hautoi hizo Stahiki.
Which means, hata kama una Mwanasheria basi atatakiwa kufanya kazi ya ziada kutaka hiki na kile ambacho kwenye mkataba hakipo na hakipo kwa sababu the system doesn't offer such benefits!
Na hata kama Producer aka-amend mkataba na kuingiza yale uliyo demand bado unaweza kushindwa kuyapata kwa sababu mfumo haupo rafiki kukuwezesha kupata ukweli wa hizo Stahiki!
Tuchukulie suala la Bonus kwa mfano! Bonus ni moja ya Stahiki ambazo msanii anatakiwa kupata!
Wenzetu Bonus inakuwa offered baada ya ku-hit kiwango fulani cha mauzo! Hivi Bongo Movies unaweza kupata revenue halisi?!
Binafsi nimeshawahi ku-submit takribani mara 3 (bila mafanikio) kazi zangu kwenye advanced film industry...
Huko nako ukipeleka kazi unakutana na mkataba upo tayari and so, you either take it or pass unless kama wewe ni pro.
Lakini kwavile mfumo wenyewe tayari upo advanced; mkataba nao unakuta umeweka karibu Stahiki zote za msingi. Hata kama una-hire Entertainment Lawyer; kazi yake itakuwa ndogo tu... sana sana kuhakikisha ikiwa vipengele vyote vya mkataba ni rafiki. Kazi itakuwa ndogo kwa sababu stahiki zote muhimu zitakuwepo na kama kuna ku-negotiate labda ku-negotiate structure ya hizo stahiki!
Screenwriter kwa mfano! Kwa Hollywood kuna structure kuu mbili za compensation structure... ya kwanza ni percentage production cost na ya pili ni fixed price. So, kutokana na experience ya Entertainment Lawyer wako, anaweza kukushauri compensation structure tofauti na ile uliyopewa kwenye mkataba.