Mike Gerald "Iron" Tyson

Mike Gerald "Iron" Tyson

mbotoki

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
268
Reaction score
115
Jambo kwenu wote.
Leo wazee wa "natuma kama nilivyopokea" wamesambaza sana habari kuwa mtajwa hapo juu katutoka.
Nimejaribu kutafuta uhakika toka vyanzo vya kuaminika kuhusu hilo suala, sijaona kwa kweli.
Huyu jamaa kutokana na simulizi ninazozisikia kuhusu yeye, ni kuwa alikuwa hapigiki aisee. Na aliwahi kuwa maarufu sana na mburudishaji wa dunia.
Ninaomba hapa kama kuna mtu anajua zaidi na zaidi kuhusu huyu mjamaa,
Ubondia wake,
na kwa nini haswa jina lake lilitawala ulimwengu. Hebu teremka hapa tulinganishe na hawa waburudishaji wa leo.
Itanisaidia sana pia kwa nn kama kweli hajafa, azushiwe kifo.
 
Ni uongo...uvumi huu uliwahi kuletwa hapa siku zilizopita
 
Alikua mahiri kwenye ngumi, alichukua ubingwa wa dunia akiwa na umri mdogo, alifungwa kwa kubaka alipotoka alikua hashikiki ulingoni. Alitumia sekunde kadhaa kumtwanga peter mcneely kabla ya kumuadhibu vibaya bondia asiyekua na mashabiki frank bruno. Alidundwa vibaya sana na busta douglas huko canada!..akaja kudundwa na bondia asiye na mvuto evander na kutusononesha wengi. Funga kazi ilikua kipigo cha mbwa mwizi alichopewa na lenox lewis. Alipigwa kama mtoto tyson na kusononesha wapenzi wa ngumi.alikua dhaifu sana kwa madem, akili zake zilikua sawasawa ulingoni lkn nje ya ulingo hakuwa na akili... wengine wataongeza!!
 
Umejibu kiufasaha ndugu.
Enzi zake, watu walikuwa wanaamka saa kumi usiku kuangalia pambano kwenye kumbi za maonyesho na kumbi zinajaa.

Jamaa amebatiza majina watoto kibao tu hapa bongo.
 
Ametoa kitabu kuelezea maisha yake hata mwaka bado. Kitafute hamna njia ya mkato.
 
Hapo kwenye pambano lake na Douglas usahihi ni kwamba pambano hilo lilifanyika nchini japan mwezi February 1990

sawa sawa! ni Japan nafikiri Busta ndio alikua mcanada kama sikosei. hakuna aliyetegema kama King Tyson angepigwa vile! maana alikua anazitafuta vile vikinga mdomo halafu alikua havioni sababu macho yalikua yamevimba sana!..inasemekana Tyson baada ya kuvuna pesa akahama team ya trainers wake na kuchukua masela wake ambao walikua hawamshauri vizuri na muda mwingi akawa anautumia kwenye starehe...na siku ile busta alikua kwenye kiwango kweli kweli mzee akaadhiriwa
 
Back
Top Bottom