Mike Tyson amrushia ngumi abiria mwenzake katika ndege baada ya kurushiwa chupa

Mike Tyson amrushia ngumi abiria mwenzake katika ndege baada ya kurushiwa chupa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363






Bondia wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson amempiga ngumi abiria mwenzake katika ndege baada ya mtu huyo "kumrushia chupa ya maji," msemaji wa Tyson amesema.

Video iliyochukuliwa kwenye ndege hiyo inamuonesha Tyson akiwa ameegemea kiti chake huku akimpiga ngumi za mara kwa mara mtu ambaye hakuonekana.

Msemaji wa Jumba la ndondi la Hall of Famer alithibitisha kwamba Tyson alimpiga abiria mwenzake ambaye alimchokoza bila sababu.

Polisi waliwaweka kizuizini watu wawili kwa muda.

Mtu mmoja alitibiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco kwa kuwa alipata majeraha kidogo.

"Hawakutoa ushirikiano kwa polisi kufanya uchunguzi zaidi," msemaji wa Idara ya Polisi ya San Francisco alisema katika taarifa.

Wote wawili waliachiliwa huru "kusubiri uchunguzi zaidi". Idara ya polisi haikubainisha jina la mhusika yeyote.
Shambulio hilo lilitokea kwenye ndege ya JetBlue Jumatano usiku, kabla ya kuondoka San Francisco hadi Florida.

Video - iliyochapishwa na TMZ - haioneshi ugomvi wote na chupa ya maji kurushwa haioneshi.

Kwa mujibu wa TMZ, Tyson alikuwa amekubali kupiga picha na abiria mwanzoni mwa safari hiyo. Lakini mwanaume huyo aliendelea kumsumbua Tyson, licha ya Tyson kumuomba atulie.
 
Tyson anapenda kupanic

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
1646064790908.png

Hii picha polisi wakimzunguka Tyson kutaka kumkamata baada ya kumng'ata sikio evander.

Cheki polisi walivokua makini na walivokua timamu na kutumia njia ya busara zaidi kumtia nguvuni.
 
View attachment 2198040
Hii picha polisi wakimzunguka Tyson kutaka kumkamata baada ya kumng'ata sikio evander.

Cheki polisi walivokua makini na walivokua timamu na kutumia njia ya busara zaidi kumtia nguvuni.
Tyson kateketeza zaidi ya dollar milion 300 na kubaki kumlaumu bure yule manywele mvi. Lakini flood Mayweather hajui kusoma na kuandika na anakula bata vibaya anazidi kutajirika tu.
 
Yaani ndo ivo tu sisi wenye umaarufu na hela nyingi Bana!! hatutakiwi kuzurula hovyo ndo sheria ya umaarufu!!… wenye njaa, wivu, wenye kusaka umaarufu pia,, wanatutafuta kwa kiu kali sana kila kona

na kila Mtu anatutaka kwa hali zoote!! yaani aonekane tu kuwa na yeye kaguswa na mtu maarufu km mie, kwa hiyo Ulinzi kwetu ni kitu cha Lazima sana!!! usipo fanya hivo utalipa wengi mnoo!!

Juzi nilikuwa pale sinza kijiweni mtu kijana barubaru!! akagonga gari yangu maksudi akajilaza chini watu waka zunguka gari yangu!! eti nimlipe nikawaaambia twende Hospitali then polisi hawataki!

Faster tu!! gari zangu nyingine zilikuwa nyuma kwa mbaali zikaja, Nikamuacha hapo dereva amalizane nao!! ukipita sehemu tanguliza king'ora na Radio call fanya kustukiza tu! ...…

Kamwe usipange safari utakamo pita km imetokea umepanga basi badili gia angani!! umaarufu ni gharama sana! broo usiombe!lkn sasa wengine umaarufu unatutafuta tu hata ufanyeje unakuja wenyewe!!

Kama ukiwa na ule wa kulazimisha km Ule wa Wema! afande Sele! NK hakuna atakaye kusumbua Manjiani humo!

Tyson amepata umaarufu kitambo lkn sasa hajui kuishi kiu-maarufu km sie wenzake tunavyo fanya, nilikwenda ziara moja Mkoani Mara, watu walilala barabarani wanatamani kunishika tu Mkono!!!

So kwa masaada wa escort langu kabambe tukabadili njia ya kimya faster tukatokea Bunda fyuuum!! mpaka Musoma Mjini nika kwea zangu pipa! huyooooo!!..lazima uishi kwa mbinu za kiu-super star!!

vinginevyo iko siku utauawa! au kutekwa Mazima kabisaa!!…..Mashabiki wako wanakutamani lkn pia humo humo wenye nia mbaya pia wanakutamani!...ni Marufuku kupita /kukaa Uswahilini hii ndo siri ya u super star!

hiyo ni sheria! wala siyo ombi!......ukipuuza hili siku moja utanikumbuka na uta-tafuta njia ya kuchomokea huko!!
 
Back
Top Bottom