Mikhail Kalashnikov: Mbunifu wa kifo au shujaa wa Urusi?

Coolant

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
1,190
Reaction score
2,031
Habari za jumapili wana jamvi, naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Moja ya habari kubwa iliyotawala vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifafa mwanzoni mwa wiki hii ni uzinduzi wa sanamu (statue) ya Mikhail Kalashnikov uliofanyika jijini Moscow Urusi.

Mikhail Kalashnikov, mbunifu wa AK-47 silaha maarufu na moja ya silaha hatari zaidi duniani (world's deadliest guns) ambae kwa sasa ni marehemu, ametunukiwa tuzo ya sanamu katika jiji la Moscow. Ila sio kila mtu kaifurahia tuzo hiyo.

d1810ce63d13ebc3da81464d7c4b58e0.jpg

Luteni Generali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov

Mara baada ya kuzinduliwa kwa sanamu yake mnamo September 19 kuliibuka maandamano ya wanaopinga tuzo hiyo kutokana na ukweli kwamba ubunifu wake umesababisha vifo visivyo na idadi. Na ndio maana wanaopinga uwepo wa sanamu yake wanasema Kalashnikov ni mbunifu wa kifo na sio shujaa wa taifa hivyo serikali haikupaswa kumtunuku.

4f12e2a58492489acfd18783f2f1e6c2.jpg

3032eb43aadd756a2bd14b11b3b9961e.jpg

Sanamu ya Kalashnikov ikimuonyesha akiwa na silaha yake aliyo ibuni ya AK-47

Katika hafla ya uzinduzi wa statue ya Kalashnikov, Vladimir Medinsky ambae ni waziri wa utamaduni wa Russia amesema "Silaha ya Kalashnikov ni utambulisho/alama sahihi ya utamaduni wa Russia, kwa sababu hiyo, serikali imeamua kuziweka silaha zote za Kalashnikov kwenye makumbusho ya Kremlin". (Makumbusho ya Kremlin ni makumbusho makubwa sana Russia na duniani kwa ujumla, yanayotambuliwa na UNESCO na yapo kwenye list of world cultural and natural heritage).

Baadhi ya wanaopinga tuzo ya sanamu kwa Kalashnikov walikua na mabango yaliyosomeka;

"Mbunifu wa silaha ni sawa na mbunifu wa kifo"

Pia wapo waliotoa mitazamo yao juu ya tuzo hiyo kwa Kalashnikov kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter, na hii ni baadhi tu ya mitazamo yao;

"Ni Moscow ya Putin pekee ndio itakubali kumtuza mbunifu wa silaha inayouwa watu wengi kuliko zote"

" Kama mwenyewe angekua hai asingeipenda sanamu yake, kwakua aliwahi kukiri kua silaha yake umeharibu tawala za nchi nyingi na kusababisha maafa makubwa"

AK-47 ilibuniwa mwaka 1947 na katika miaka 60 iliyopita zimetengenezwa AK-47 zaidi ya milioni 70. Zinatumiwa na majeshi, makundi ya uhalifu, magaidi na waasi.

ec6af0523d6b40bf8b05b5e1cd8122d2.jpg

Kalashnikov akiwa na AK-47

AK-47 inauwa watu zaidi ya 250,000 kila mwaka. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kulinganisha na ile ya silaha zote za kisasa kwa ujumla wake.

Kalashnikov alifariki mwaka 2013, na hivi ndivyo alivyosema muda mfupi kabla hajafa , nanukuu "Can it be that I'm guilty for people's death?"

Bado swali linabaki pale pale "Kalashnikov ni mbunifu wa kifo au ni shujaa"?

Nawasilisha,
 
Simple answer: Ni shujaa over. Huwezi kuwa shujaa kama hujapigana vita yoyote iwe ya kiuchumi au ya ki-silaha. Na hiyo ilikuwa ni kutafuta mbinu za taifa lake kushinda vita kirahisi. Alikuwa sahihi kusema vile kabla hajafa kwa sababu matumizi aliyoyalenga yeye na jinsi ilivyotumika ni tofauti. Kadhalika sehemu au aliyotaka yeye ziwe, zikawa wrong.
 
Ni kweli usemavyo ila inasikitisha sana unapowaona IS wakiitumia hiyo silaha kuua watu wasio na hatia
 
Na hao wagunduzi wa kale wa madini ya chuma tuwaiteje, kila kilichopo duniani ni kizuri na ni kibaya pia.
 
Ni kweli usemavyo ila inasikitisha sana unapowaona IS wakiitumia hiyo silaha kuua watu wasio na hatia
Issue ya msingi kuangalia ni kutafuta lengo LA msingi alilokua nalk mbunifu WA hiyo siraha
 
Kama anajuta kuivumbua fanyeni maombi afufuke anipatie hatimiliki yake(AK-47)!!...
kila zama na kitabu chake hata alievumbua upanga na mkuki angejuta basi aaah!!..
 
Huyu jamaa ,,urusi wanamuhesabu kama Baba wa Siraha ..

Karibu bunduki nyingi zilizopo Urus nikutokana na ugunduzi wake.

Bongo Bahati mbaya.
 
Hivi Ak-47 ndio inayoua au binadamu anaitumia Ak-47 yeye mwenyewe kwa utashi wake kuangamiza binadamu wenzake?
 
Back
Top Bottom